Je, Biblia ya ukweli/Halisi ni ipi?

Je, Biblia ya ukweli/Halisi ni ipi?

Ndio maana nikakwambia unamfanya Allah ni mjinga , anawezaje kusema kamsamehe dhambi zijazo na wewe unasema hakukua na dhambi zijazo , yani unathibitisha Allah alikuwa hajui yajayo,
Ndio aliambiwa amesamehewa dhambi zijazo japokuwa hakutenda dhambi...
 
UTANGULIZI
Historia ya Biblia ya kikristo ni ndefu jinsi vitabu vilivyopatikana lakini ntaandika kwa kifupi sana na mengine tutaandaika tunavyozidi kuchangia kwenye uzi huu. Na pia nitoe rai mapema kuwa uzi huu sio wa kidini bali wa kielimu/historia hivyo sitegemei watu kurushiana matusi ya kuhusu dini sijui Mungu yupo au hayupo!! N.k
View attachment 993939
Prologue
Biblia ya kikristo ni mjumuiko wa vitabu mbalimbali vya manabii/Mitume wa Mungu ambao vimejumuishwa pamoja ili kutoa muongozo wa kiimani kwa wakristo kote ulimwenguni. Biblia inatambulika kama iliandikwa na vitabu kujumuishwa kwa uweza wa MUNGU hivyo ni kitabu kitakatifu, lakini kilichonishtua ni kugundua kwamba kati ya wakristo wanatumia Biblia tofauti kabisa yaani Wakatoliki Biblia yao ina vitabu 73, waprotestant vitabu 66, Orthodox Tawahedo (Ethiopia) ina vitabu 81 hili limenifanya nifungue uzi ili tumalize mkanganyiko huu na naomba tusome taratibu na kwakuelewa mada inazungumzia nini kabla ya kuchangia kwa kuongozwa na ushabiki au mihemko.

Historia
Wayahudi (Israel) walikuwa wanaandika maandiko wanayovuviwa na Mungu wao Yahweh tokea miaka 600 kabla ya Yesu na walikuwa na fixed canon ya vitabu 24 (39 ukivigawa) mpaka kipindi cha nabii wa mwisho Malachi 400 BC hivyo inasemekana ndio vitabu pekee vilivyokuwepo. kufikia karne ya 4 kabla ya kristo (KK) wayahudi waliokuwa uhamishoni hasa misri walitafsiri vitabu vya agano la kale vilivyoandikwa kiebrania kwenda kigiriki na kuzaa Biblia iliofahamika kama ''Septuagint''.... Biblia hii ilipata ushawishi sana kuliko ya kiebrania na ieleweke kwamba ni Biblia hii ndio imetumika mpaka na Yesu alipokuwa akinakili maandiko ya agano la kale kiufupi 70% ya quotes kutoka agano la kale kwenye vitabu vya Agano jipya vimetolewa kwenye Greek Septuagint. Kufikia hapa kukawepo na Biblia mbili kuu hivyo twende pamoja.
View attachment 993940
Mgogoro
Ikumbukwe Septuagint ilijumuisha vitabu vya kimafundisho ambavyo Hebrew bible haikuvitambua vitabu hivi vinajumuisha Macabees, Sirach,Wisdom of solomon n.k. Sasa ikafika mahali Septuagint (kigiriki) ikawa inatumika zaidi kuliko maandiko ya kiebrania (wayahudi) hivyo kwa mujibu wa mwanahistoria Heinrich Graetz ikabidi kikundi cha wayahudi kikutane kwa kilichoitwa council of Jamnia kilichofanyika 70 Baada ya kristo ambapo ndio kiliweka msimamo wa vitabu gani vya biblia ya kiebrania ndio vitambulike kwa wayahudi wote yote hii ili kuzuia upepo wa Biblia ya Greek sepruagint na hivyo hapa wakawa na msimamo wa vitabu vichache hasa vya agano la kale 39 tofauti na 46 vya septuagint. Hivyo tokea hapa madhehebu tofauti ya kikristo yakachukua Biblia mojawapo ya pande hizi mfano RC wao waliendelea na Greek Septuagint ambayo ndio ilitumiwa na mitume ila waprotestant wao waliamua kuendelea na Hebrew Bible wakiamini ndio halali na haijachakachuliwa pia madhehebu mengine kma Tawahedo Orthodox na mengineo yalikuwa na misimamo yao juu ya vitabu fulani hivyo utakuta baadhi ya makanisa yana vitabu kati ya hivyo 39 hadi 46 vya agano la kale.

Martin Luther
Karne ya 16 kiongozi wa wanamabadiliko/protestants walioamua kujitenga na ukatoliki Dr. Martin Luther naye aliamua kufanya tafsiri ya Biblia kwenda lugha ya kijerumani. Kiliandikwa 1520-34 na katika kuifanyia majumuisho naye alitaka kupunguza vitabu 7 vya agano jipya vikiwemo Ufunuo,Yuda,Waebrania na Yakobo n.k kwa kile alichokiita kwamba "havikuwa na uvuvio wa Roho mtakatifu" na hata leo hii kwenye Luther bible cha waprotestant hivyo vitabu 4 vimewekwa vya mwisho kabisa katika biblia yao na nakala za mwanzoni viliwekwa kundi moja na vitabh vilivyoitwa ''apocrypha''.

Pia luther alikipinga vikali kitabu cha esther nakutaka kifutwe kutoka kwa Biblia. Alisema hakina uvuvio wa Roho mtakatifu maana hakuna mahala kinamtaja MUNGU!! Martin luther alipinga pia uwepo wa kitabu cha James/Yakobo kwenye Biblia sabau kwanza kiliandikwa karne ya 2 ambapo muandishi wanayedai ni Yakobo kaka yake yesu alishakuwa amekufa toka mwaka 67 BK hivyo aliona kma ni kilifojiwa tu.
View attachment 993938

HITIMISHO
Sasa baada ya kuwa nimepitia baadhi ya hoja za wana JF humu hasa zinazogusa maslahi ya kikristo huwa wana conclude kuwa Biblia haina makosa maana ilivuviwa na Roho mtakatifu sasa nilikuwa nataka wajuzi mnisaidia maswali yafuatayo

1.je kauli hii inapotolewa huwa ina maana ya Biblia ipi ambayo ilivuviwa na Roho?

2. Je Biblia gani ni halali

3. Manabii wanasema usiongeze au kupunguza neno kwenye Vitabu vyao sasa Je kama mmoja ndio yupo sahihi ina maana wengi wamepotoshwa??

4. Na kama wamepotoshwa je nini hatma ya ukristo kama wahuni wachache wanaweza ongeza maneno au kupunguza kwenye Biblia

5. Swali la mwisho naamini MUNGU anaona haya makosa Je ina maana karuhusu neno lake lipotoshwe?? Na kama sio kwanini mpaka sasa kaacha wahuni wachezee NENO lake.

Naomba kuwasilisha

Cc: ningeomba Moderator kina Active na Mhariri msihamishe uzi huu jukwaa la dini ili niweze kupata mawazo ya wana JF wote hta wasio na access na jukwaa la dini, nitashukuru kwa hilo.
Hongera sana Kiongozi kwa mada njema sana!

Kwa Utangulizi ni muhimu kuyachunguza maandiko kwa umakini na kuuliza kama jinsi ambavyo wewe unafanya - Mtume Paulo Aliwasifia sana WABELOYA ambao hawakuridhika tu na kumsikia Paulo akihubiri na kufundisha bali waliyachunguza maandiko kwa Umakini.

BIBLIA iliyosahihi na ya KWELI ni Biblia yenye Ujumbe wa KIFO cha YESU -UFUFUO na HUKUMU YA MILELE Na UZIMA wa MILELE.
Wazee wa kanisa la Mwanzo walibishana kuhusu baadhi ya Vitabu Wakapitia na kujiridhisha kuwa Habari za vitabu vile vilivyo "FICHWA" (APOCRYPHA.) kwamba habari zake zinakosa sifa za Kihistoria na Utamaduni wa KIYAHUDI - Ambako ndiko chimbuko la Imani yetu Wakristo.

Biblia iwapo ilikusudiwa kupotoshwa - just a simple Logic - Mistari hii TORATI 4:2 na Ufunuo wa Yohana - kama ilivyoelezwa na wachangiaji wengine Ingefutwa kwa Makusudi ili kuhalalisha Upotoshaji wa Maudhui makuu yalipo kwenye BIBLIA.

KJV,NIV na nk ukiondoa "KITABU CHA MORMON" ni Habari kamili za Tumaini letu - Hazijabadilishwa wala kupunguzwa la Hasha - Kilichofanyika ni Tafsiri zenye Ujumbe ule ule tu,Asomaye na afahamu.

Kuna Imani zingine sio tu kwamba waliviondoa Vitabu walivyovikataa bali walivichoma moto kabisa - Visiwepo katika sura ya nchi.

Lakini Vitabu vyote Vilivyosadikiwa kuwa ni Ujumbe uliofanana na Biblia VIPO mpaka leo na Vinasomwa wala hakuna wakukukataza usivisome bali kuna ONYO tu kwavyo kuwa sio Ujumbe wa Mungu.
Bwana Zitto Jr ! hebu fikiria Anatokea Mzanzibari anatunga Kitabu cha Habari za WAHA wa Kigoma ambao hajawahi hata kuishi nao bali alisikia habari zao tu - halafu akatokea MUHA ambaye anadai kwa maelezo ya kutosha kuwa Alivyoeleza Mzanzibari sio sahihi kulingana na mila na desturi za waha! Yupi tutamwamini?

Natumaini nimejaribu kiasi kuchangia.
Asante.
 
Nitaacha kujadiliana na nyie sasa mmekosa hoja na mnanipotezea muda..
Allah akimruhusu muhamad kula housegirl, na kumkaripia asirudie tena kuwaomba msamaha wake zake anapokamatwa na house girl

66:1 O Prophet! Why do you prohibit what God has made lawful for you in terms of your Coptic handmaiden Māriya — when he lay with her in the house of Hafsa who had been away but who upon returning and finding out became upset by the fact that this had taken place in her own house and on her own bed — by saying ‘She is unlawful for me!’ seeking by making her unlawful for you to please your wives? And God is Forgiving Merciful having forgiven you this prohibition. Tafsir al-Jalalayn
 
Good question
Biblia iliandikwa katika lugha tatu tofauti
Kiebrania( Hebrew), kiaramu (Aramaic), na kiyunani/ kigiriki (Greek) ,

Ni kitabu kilichoandikwa na waandishi said ya arobain kwa miaka 1500 walioishi kwa nyakati tofauti tofauti.

KWA NIN KUNA VERSIONS,
Kila biblia hupimwa authenticity yake kwa kulinganishwa na maandiko ya awali ambayo yaliandikwa katika lugha izo tatu.

Na Kama kuna utofauti wa kitafasri katika biblia iliyoandikwa kwa lugha yeyote kulinganishwa na lugha ya awali, huwa kuna mabadiliko yanafanyika. Na kufanya kuwa na versions tofaui tofauti lakn context huwa n ile ile

Ni kama waislam mnavodai kwambo Quran iloandkwa na wasaidiz wa Mohammad haijabidilishwa lakina kuna version tofauti tofauti za tafsir.
 
Nitaacha kujadiliana na nyie sasa mmekosa hoja na mnanipotezea muda..
Mada imesimama naomba kuku uliza maswali mawili.
1. Naomba kuoneshwa Aya inayowaruhusu kuadhimisha skukuu ya Maulidi.

2. Naomba Aya zinazo waamrisha Waislamu kutimiza Nguzo tano za Uislamu
Yaani
1. Kuhiji Maka
2. Kutoa Zaka
3. Kufunga mwezi wa Ramadhani
4. Kushahadia
5. Kuswali, (swala ngapi kwa siku moja)

Ndani ya Qurani.
Ili hata nikisilimu na kuwa Muislamu nijue kwamba mwongozo wangu ni Kitabu cha Qurani.

Naomba kuoneshwa Aya tu basi sitaki maelezo.
Karibu.
 
Mada imesimama naomba kuku uliza maswali mawili.
1. Naomba kuoneshwa Aya inayowaruhusu kuadhimisha skukuu ya Maulidi.
Haipo,,

N.B : Waislamu hatujaruhusiwa kusherehekea Maulidi
2. Naomba Aya zinazo waamrisha Waislamu kutimiza Nguzo tano za Uislamu
Yaani
1. Kuhiji Maka
Hii imepewa jina la sura kabisa katika Qur'an ( suratul Hajj) imeelezewa vzr humo..

Suratul Hajj ;
" Na watangazie watu Hijja, watakujia kwa miguu na juu ya kila ngamia aliyekonda, wakija kutoka katika kila njia ya mbali."

Surat al İmran ;
" Kwa hakika nyumba ya kwanza waliowekewa watu kwa ajili ya ibada ni ile iliyoko Bakka (Makka), iliyobarikiwa na yenye uongofu kwa walimwengu wote.
Ndani yake zipo aya zilizo wazi masimamio ya Ibrahim, na mwenye kuingia humo anakuwa katika amani. Na kwaajili ya Mwenyezi Mungu imewajibikia watu wahiji kwenye nyumba hiyo, kwa yule mwenye uwezo njia ya kwendea. Na atakaye Kanusha basi Mwenyezi Mungu si mhitaji kwa walimwengu. " ( 3: 96-97 )
2. Kutoa Zaka
Imetajwa katika aya tofauti tofauti,, mojawapo ni
Suratul Hajj,
41 : Wale ambao tukiwapa madaraka katika nchi husimamisha swala, na wakatoa ZAKA, na wakaamrisha mema, na wakakataza maovu. Na kwa Mwenyezi Mungu ndio marejeo ya mambo yote. "
4. Kushahadia
Shahada ina parts mbili
Part ya kwanza imeongelewa kwenye Surat Al Imran;
18: Mwenyezi Mungu, na Malaika, na wenye ilmu wameshuhudia kuwa hakika hakuna Mungu anayefaa kuabudiwa kwa haki isipokuwa yeye ( Allah), ndiye mwenye kusimamisha uadilifu hapana Mungu isipokuwa yeye, mwenye nguvu na mwenye hekima.

Part ya 2 kwenye Suratul Ahzab
40 : Si Muhammad baba wa yeyote katika wanaume wenu, bali ni mtume wa Mwenyezi Mungu na mwisho wa Manabii, na Mwenyezi Mungu ni mjuzi wa kila kitu.
5. Kuswali,
Imetajwa katika aya tofauti tofauti,, mojawapo ni
Suratul Hajj,
41 : Wale ambao tukiwapa madaraka katika nchi husimamisha SWALA, na wakatoa zaka, na wakaamrisha mema, na wakakataza maovu. Na kwa Mwenyezi Mungu ndio marejeo ya mambo yote. "
(swala ngapi kwa siku moja)
Surat Hud,
114 : Na shika sala katika ncha mbili za mchana na katika nyakati za usiku. Hakika mema huondoa maovu. Huu ni ukumbusho kwa wanao kumbuka.
 
3. Kufunga mwezi wa Ramadhani
Imeelezwa suratul baqara, kwanzia aya ya 183 mpka 185 kama inavoonekana hapa chini..
16238447812334744729919288721784.jpg
 
Hapo unathibitisha Allah hajui yajayo


Yesu ndio anajua hapa ??

Matthew 24:36 Jesus said "No one knows about that day or hour, not even the angels in heaven, nor the Son, but only the Father."
 
Yesu ndio anajua hapa ??

Matthew 24:36 Jesus said "No one knows about that day or hour, not even the angels in heaven, nor the Son, but only the Father."
Yesu Akasema
John 10:30 "I and my Father are one."
 
Yesu Akasema
John 10:30 "I and my Father are one."

29 My Father, which gave them me, is greater than all; and no man is able to pluck them out of my Father's hand.



This is verse 29, it comes right before verse 30, and in verse 29 Jesus says the Father is greater than ALL, this obviously includes Jesus since he is not the Father.

So therefore how to Christians try and assume that this verse shows equality between Jesus and the Father is beyond me, just a verse before it Jesus says the Father is greater than everyone!



In fact this is not the first time that Jesus says the Father is greater than him, he does it again later:



28

Ye have heard how I said unto you, I go away, and come again unto you. If ye loved me, ye would rejoice, because I said, I go unto the Father: for my Father is greater than I (John 14:28)
 
29 My Father, which gave them me, is greater than all; and no man is able to pluck them out of my Father's hand.



This is verse 29, it comes right before verse 30, and in verse 29 Jesus says the Father is greater than ALL, this obviously includes Jesus since he is not the Father.

So therefore how to Christians try and assume that this verse shows equality between Jesus and the Father is beyond me, just a verse before it Jesus says the Father is greater than everyone!



In fact this is not the first time that Jesus says the Father is greater than him, he does it again later:



28

Ye have heard how I said unto you, I go away, and come again unto you. If ye loved me, ye would rejoice, because I said, I go unto the Father: for my Father is greater than I (John 14:28)
UlItaka Asemeje Wakati Alipokuwa ktk hali Yake ya UBINADAMU KAMILI??
 
UlItaka Asemeje Wakati Alipokuwa ktk hali Yake ya UBINADAMU KAMILI??
kijana hajui chochote huwa ana copy paste , anashindwa kuelewa Yesu anapoongoe katika human flesh, hapo hapo ukimuuliza Allah aliwezaje kuwa mti nakuongea , lazima abadilishe mada
 
kijana hajui chochote huwa ana copy paste , anashindwa kuelewa Yesu anapoongoe katika human flesh, hapo hapo ukimuuliza Allah aliwezaje kuwa mti nakuongea , lazima abadilishe mada
Hapa Yesu Kristo anatenda akiwa katika hali ya Ki-Mungu.
Hakuna Binadamu anaweza kutenda hivi hadi jamaa zake walishikwa na Butwaa.

Sembuse Gavana,

Marko 2:5
Naye Yesu, alipoiona imani yao, akamwambia yule mwenye kupooza, Mwanangu, umesamehewa dhambi zako.
Marko 2:6 Na baadhi ya waandishi walikuwako huko, wameketi, wakifikiri mioyoni mwao,
Marko 2:7 Mbona huyu anasema hivi? Anakufuru. Ni nani awezaye kusamehe dhambi isipokuwa mmoja, ndiye Mungu?
Marko 2:8 Mara Yesu akafahamu rohoni mwake kwamba wanafikiri hivyo nafsini mwao, akawaambia, Mbona mnafikiri hivi mioyoni mwenu?
Marko 2:9 Vyepesi ni vipi, kumwambia mwenye kupooza, Umesamehewa dhambi zako, au kusema, Ondoka, ujitwike godoro lako, uende?
Marko 2:10 Lakini mpate kujua ya kwamba Mwana wa Adamu anayo amri duniani ya kusamehe dhambi, (hapo amwambia yule mwenye kupooza),
Marko 2:11 Nakuambia, Ondoka, ujitwike godoro lako uende nyumbani kwako.
Marko 2:12 Mara akaondoka, akajitwika godoro lake, akatoka mbele yao wote; hata wakastaajabu wote, wakamtukuza Mungu, wakisema, Namna hii hatujapata kuiona kamwe.

Mathayo 9:2
Na tazama, wakamletea mtu mwenye kupooza, amelala kitandani; naye Yesu, alipoiona imani yao, alimwambia yule mwenye kupooza, Jipe moyo mkuu, mwanangu, umesamehewa dhambi zako.
Mathayo 9:3 Na tazama, baadhi ya waandishi wakasema nafsini mwao, Huyu anakufuru.
Mathayo 9:4 Naye Yesu, hali akijua mawazo yao, akasema, Mbona mnawaza maovu mioyoni mwenu?
Mathayo 9:5 Kwa maana rahisi ni lipi, ni kusema, Umesamehewa dhambi zako, au ni kusema, Ondoka, uende?
Mathayo 9:6 Lakini mpate kujua ya kwamba Mwana wa Adamu anayo amri duniani ya kusamehe dhambi, (amwambia yule mwenye kupooza) Ondoka, ujitwike kitanda chako, uende nyumbani kwako.
Mathayo 9:7 Akaondoka, akaenda zake nyumbani kwake.
Mathayo 9:8 Makutano walipomwona, walishikwa na hofu, wakamtukuza Mungu, aliyewapa watu amri ya namna hii.


Mathayo 9:18 Alipokuwa akiwaambia hayo, tazama, akaja jumbe mmoja, akamsujudia, akisema, Binti yangu sasa hivi amekufa; lakini njoo, uweke mkono wako juu yake, naye ataishi.
Mathayo 9:19 Akaondoka Yesu, akamfuata, pamoja na wanafunzi wake.
Mathayo 9:23 Yesu alipofika nyumbani kwa yule jumbe, aliona wapiga filimbi, na makutano wakifanya maombolezo,
Mathayo 9:24 akawaambia, Ondokeni; kwa maana kijana hakufa, amelala tu. Wakamcheka sana.
Mathayo 9:25 Lakini makutano walipoondoshwa, aliingia, akamshika mkono; yule kijana akasimama.
Mathayo 9:26 Zikaenea habari hizi katika nchi ile yote.

( Leo Gavana, na wenzake Maamuma, wakisikia habari za Yesu wanacheka sana, kama wapigafirimbi walivyomcheka sana Yesu ktk Mathayo 9:24 )
 
Back
Top Bottom