Mtoto wa Mkulima
JF-Expert Member
- Apr 12, 2007
- 681
- 126
Waungwana,
Mawazo ni mazuri sana, ila utekelezaji wake vipi? TANROADS wameshanunua viwanja 3 na wanataka kujenga makao makuu ya city center Wizara ya mambo ya ndani wankamilisha jengo lao City center, kila kitu city center.. nani wa kulisemea hili?? Je kusema tuu kwenye JF inatosha? mimi ni mgeni ila naomba mawazo yenu kwa nini Tanroad wajenge head office city center? kwani wakijenga kule mabibo au dodoma au arusha au mbeya itakuwaje?
Jamani Watanzania tuamkee
Mkuu unayouliza ni kweli na ni mambo ya msingi. Tatizo kubwa watu wa JF inapokuja issue ya maana na inayohusu maendeleo kama hii wanakaa kimya hamna wachangiaji ila ikija issue ya siasa au sijui mtu kapewa talaka utaona siku moja tuu post zimefika 1000.
Jaribu kuanzisha topiki ya maana hapa utaona watu wanavyoikimbia lakini sema sijui kinguke kafumaniwa etc.
Anyway hapa tunajadili mambo mengi sana na kuna wachangiaji wengi vichwa hapa naamini watachangia kwa hilo.
Mimi nadhani kama jamaa alivyosema hapo juu hili lakuhamia Dodoma ni gumu sana bora bagamoyo ndio maana naona kulikuwa na issue yakujenga International standard airport kule.