Je, bado kuna umuhimu wa kuhamisha makao makuu ya nchi Dodoma?

Waungwana,
Mawazo ni mazuri sana, ila utekelezaji wake vipi? TANROADS wameshanunua viwanja 3 na wanataka kujenga makao makuu ya city center Wizara ya mambo ya ndani wankamilisha jengo lao City center, kila kitu city center.. nani wa kulisemea hili?? Je kusema tuu kwenye JF inatosha? mimi ni mgeni ila naomba mawazo yenu kwa nini Tanroad wajenge head office city center? kwani wakijenga kule mabibo au dodoma au arusha au mbeya itakuwaje?

Jamani Watanzania tuamkee

Mkuu unayouliza ni kweli na ni mambo ya msingi. Tatizo kubwa watu wa JF inapokuja issue ya maana na inayohusu maendeleo kama hii wanakaa kimya hamna wachangiaji ila ikija issue ya siasa au sijui mtu kapewa talaka utaona siku moja tuu post zimefika 1000.

Jaribu kuanzisha topiki ya maana hapa utaona watu wanavyoikimbia lakini sema sijui kinguke kafumaniwa etc.

Anyway hapa tunajadili mambo mengi sana na kuna wachangiaji wengi vichwa hapa naamini watachangia kwa hilo.

Mimi nadhani kama jamaa alivyosema hapo juu hili lakuhamia Dodoma ni gumu sana bora bagamoyo ndio maana naona kulikuwa na issue yakujenga International standard airport kule.
 
Mkuu unayouliza ni kweli na ni mambo ya msingi. Tatizo kubwa watu wa JF inapokuja issue ya maana na inayohusu maendeleo kama hii wanakaa kimya.

Mtoto wa mkulima unayozungumza yana ukweli. Lakini pamoja na hayo, topiki kama hizi zimezungumzwa sana hapa JF. Kwa hivyo, unapobaini kuwa watu hawachangii haina maana kuwa wamepuuza topiki uliyoanzisha. Wasomaji wengi tunasubiri kusoma mawazo mapya.

Mimi nadhani kama jamaa alivyosema hapo juu hili lakuhamia Dodoma ni gumu sana bora bagamoyo ndio maana naona kulikuwa na issue yakujenga International standard airport kule
.

Hilo la kuhamia dodoma halina ugumu wowote. Kama raisi mwenyewe akiamua kuhamia dodoma, wote watahamia dodoma. Hata hao mabalozi watajenga ofisi zao huko huko dodoma. Tatizo ni kwamba mkuu wa nchi hana mpango wa kuhamia dodoma, sembuse hao makatibu wakuu na mawaziri
 
Waungwana,
Mawazo ni mazuri sana, ila utekelezaji wake vipi? TANROADS wameshanunua viwanja 3 na wanataka kujenga makao makuu ya city center Wizara ya mambo ya ndani wankamilisha jengo lao City center, kila kitu city center.. nani wa kulisemea hili?? Je kusema tuu kwenye JF inatosha? mimi ni mgeni ila naomba mawazo yenu kwa nini Tanroad wajenge head office city center? kwani wakijenga kule mabibo au dodoma au arusha au mbeya itakuwaje?

Jamani Watanzania tuamkee

Pia makao makuu ya mpango wa vitambulisho kwa raia ambao wanategemea kuanzisha pia yatakuwa city centre, Dar es salaam...

Sijui wanafikiria nini hawa... bora hata kama wangekuwa wanapanua mji na kujenga sehemu kama Chanika, Goba na kwenye outskirts nyinginezo, lakini hivi sasa kila kitu city centre..city centre. Inakasirisha kwa kweli.

SteveD.
 
Labda ili wajipitishe pitishe kule kwenye mitaa ya magogoni ili ikiwizekana prezida na waziri mkulu awakumbuke kwenye ufalme wa duniani! tehetehe ...
 
Tatizo kubwa watu wa JF inapokuja issue ya maana na inayohusu maendeleo kama hii wanakaa kimya hamna wachangiaji ila ikija issue ya siasa au sijui mtu kapewa talaka utaona siku moja tuu post zimefika 1000.

Hii ndio JF bwana, ukitaka watu wachangie hoja, i-link na Waziri Mkuu au Rais au na Personality yoyote,,, hapo Hoja zitakushuka kama mvua...
Kwa mfano kwenye hoja hii hii ungesema kigogo mmoja amepata xx,xxx ungeona mambo!!!

Lakini ati unasema unaleta hoja ambayo ni ya maendeleo tu na hutaji mtu...sahau!!!
 
Waungwana,
Mawazo ni mazuri sana, ila utekelezaji wake vipi? TANROADS wameshanunua viwanja 3 na wanataka kujenga makao makuu ya city center Wizara ya mambo ya ndani wankamilisha jengo lao City center, kila kitu city center.. nani wa kulisemea hili?? Je kusema tuu kwenye JF inatosha? mimi ni mgeni ila naomba mawazo yenu kwa nini Tanroad wajenge head office city center? kwani wakijenga kule mabibo au dodoma au arusha au mbeya itakuwaje?
Jamani Watanzania tuamkee

Raisi jakaya mrisho kikwete anayo nafasi kubwa ya kubadilisha haya mambo. Pamoja na ukweli kuwa Jakaya ametembea sehemu nyingi duniani na kujionea mwenyewe kwa macho yake, Lakini inaonekana ameshindwa kujifunza!!! Jakaya haitaji washauri katika hili jambo.
 
kwi kwi kwi kwi! nakupata hapo najua umetumia lugha ya picha Madilu ni kwamba haitakaa ihamie Dodoma maana ni jambo lisilo wezekana. Nilipokuwa nasoma geografia nilia mbiwa nchi ya Duch ilijengwa na waduch (Reclaimed land) na hicho kitendo kinaitwa land reclamation je kitendo cha kujenga bahari tuite je? au ni sea reclamation? joke.

Unanikumbusha jografia ya sekondari.
Hii tutaita 'sea channeling' ama?
 
Raisi jakaya mrisho kikwete anayo nafasi kubwa ya kubadilisha haya mambo. Pamoja na ukweli kuwa Jakaya ametembea sehemu nyingi duniani na kujionea mwenyewe kwa macho yake, Lakini inaonekana ameshindwa kujifunza!!! Jakaya haitaji washauri katika hili jambo.

Hatembei kujifunza, anatalii. Sio unaona watalii wanaokuja bongo kuangalia MBUGA ZA WANYAMA hakuna anayejenga ZOO kwao.
 
Viongozi wa Tanzania wakienda nje huwa hawajifunzi lolote, kuna wanaofurahia vyakula na starehe na banquets, lakini hawajifunzi wenzetu wamefanya nini na kuwa walipo. Noana ni mabingwa wa kusifu wenzetu wamefika wapi, lakini hawajiulizi sisi tumeachwa vipi.
 
Mkuu hii ni kweli kabisa na si kwa viongozi tuu bali hata kwa maofisa waserikali wa ngazi zote. Nakuambia mtu anaenda nnje akirudi anajisifia viwanja alivyokuwa etc. Wenzetu wazungu na wajapan, etc wao wakienda nnje wanabeba hadi Kamera zao na wanatumia kuibia technology. Mimi nasemaga hivi kiongozi anajisikia je wakati anawakilisha nchi masikini kuliko zote duniani? Hivi huwa hawana wivu wa kuwa kama wengine?
 
Ndio pale wanaposema akili ni za kuzaliwa na kila mtu ana zake, hata kama ukimsomesha fungo namna gani yeye ni fungo tu hawezi kubadilika. Hawa viongozi wetu ni wababaishaji na kamwe hawawezi kuhamia Dodoma kwa sababu katika maisha yao wamezoea kupewa peremende na mafisadi kubuhu waliopo Dar es Salaam, wanaogopa wakihamia Dodoma nani atawapa peremende.
 
Ina wezekana Tangu siku nyigi Serikali ipo Dodoma!! au Mpaka Ikulu I-hamie DODOMA?-Itawezekana Indapo Mipango wa Chuo Kikuu Cha Dodoma itafikiwa kwa wakati!!

Uwanja wa Ndege wa DODOMA-(Msalato) Uanze Kutenge nezwa Leo!!
 
Gharama za kuhamia Dodoma ni kubwa mno. Sasa hivi kuna wizara nyingi zina gharama mbali mbali katika miji miwili, Dar na Dodoma, na hivyo kuongeza gharama kubwa ya uendeshaji wa serikali. Pesa hiyo inaweza kutumika katika mambo mengine muhimu badala ya huu usanii wa kuhamia Dodoma ambao hautatekelezeka daima, maana sasa hivi ni zaidi ya miaka 30 bado 'tunahamia' Dodoma tu!!!

Kuhamia Dodoma kujadiliwa kitaifa
Shadrack Sagati, Dodoma
Daily News; Monday,June 23, 2008 @18:01

Waziri Mkuu Mizengo Pinda amesema serikali itaendesha mjadala wa kitaifa utakaowashirikisha wadau mbalimbali juu ya suala la kuhamishia Makao Makuu kutoka Dar es Salaam kwenda Dodoma.

Katika hotuba yake ya makadirio ya matumizi yake aliyoisoma bungeni jana, Pinda alisema baada ya majadala huo serikali itaandaa mapendekezo ya kutunga sheria mpya ya kutambua rasmi Dodoma kuwa Makao Makuu ya Serikali.

Pinda pia alizungumzia maslahi ya Madiwani na kueleza kuwa katika mwaka ujao wa fedha Sh bilioni 4.8 zimetengwa kwa ajili ya posho za madiwani. Alisema Serikali itaandaa muswada wa marekebisho ya

Sheria ya Bima ya Afya utakaowezesha madiwani kupata matibabu kupitia mfuko huo na pia itaandaa marekebisho ya sheria ya fedha yatakayofanyika ili madiwani wafaidike na msamaha wa kodi kwa vyombo vya usafiri.

Waziri Mkuu pia alizungumzia muundo wa Jiji la Dar es Salaam ambalo lina manispaa tatu zinazojitegemea na kueleza kuwa uzoefu wa miaka minane wa utekelezaji wa mpango huo umeonyesha kuwa muundo huo una matatizo ya uendeshaji na hivyo kutokidhi matarajio yaliyokusudiwa ya kutoa huduma bora kwa wananchi.

Alisema Jiji la Dar es Salaam kwa sasa linakabiliwa na miundombinu ya barabara isiyokidhi mahitaji yanayopanuka kila siku na miundombinu ya maji safi na taka na ukuaji wa jiji usioenda sambamba na utoaji wa huduma kwa wananchi.

“Hali hii inalifanya jiji lisionekane kama kioo cha nchi yetu,” alisema Pinda na kuongeza “Kuna haja ya kuliangalia kwa namna ya pekee.” Alisema kwa kuzingatia hali hiyo serikali imeunda Kamati Maaluu ya kuangalia, kuchambua na kutoa mapendekezo ya namna ya kuboresha muundo wa halmashauri za

Dar es Salaam na uendeshaji wake ili wananchi wafaidike na huduma bora zinazopaswa kutolewa na mamlaka hizo za Serikali za Mitaa. Kuhusu usafiri wa Jiji la Dar es Salaam, alisema fidia kwa wananchi ambao wameathirika na upanuzi wa miundombinu kwa ajili ya mradi wa mabasi yaendayo kasi itakamilika kulipwa mishoni mwa mwezi huu.

Alisema ujenzi wa miundombinu utaanza katika mwaka ujao wa fedha na utachukua miezi 24. Waziri Mkuu pia alizungumzia uchaguzi wa vitongoji ambao utafanyika Oktoba mwakani na kueleza kuwa Sh bilioni 4 kwa ajili ya maandalizi ya uchaguzi huo ikiwamo kuhakiki mipaka ya vitongoji, vijiji na mitaa, kufanya mapitio ya kanuni za uchaguzi na kufanya mikutano ya ushauriano na vyama vya siasa.

Kuhusu mapambano dhidi ya rushwa, Pinda alisema katika mwaka ujao wa fedha uchunguzi wa tuhuma mbalimbali utafanyika na mkazo zaidi utawekwa kwa tuhuma za mikataba mikubwa ambayo inaiingizia serikali hasara.

Akizungumzia sekta ya madini, Pinda alisema migodi mingi ya madini hasa ya wachimbaji wadogo haiko salama hivyo akatoa mwito suala hilo kutafutiwa ufumbuzi wa kudumu kwa kuhakikisha kwamba wamiliki wa migodi hiyo wanafuta kanuni zilizopo za usalama migodini kuepuka maafa kama yaliyotokea Mererani.

Kuhusu chakula, alisema katika bajeti ya mwaka ujao wa fedha zimetengwa Sh bilioni 26.3 kwa ajili ya kununua tani 100,000 za mahindi na tani 5000 za mtama utakaofanywa na kitengo cha hifadhi ya chakula.

Pia amekiagiza kitengo hicho kununua nafaka kutoka kwa wakulima kwa wakati kuzuia uwezekano wa wakulima kuuza chakula kwa walanguzi na nje ya nchi na baadaye kukinunua kwa bei kubwa zaidi.

Waziri Mkuu pia alisema kituo cha uwekezaji katika mwaka unaomalizika Julai kimesajili miradi 902 yenye thamani ya Sh bilioni 8.1 ambayo imetoa ajira kwa Watanzania 127,588. Alisema kati ya miradi hiyo miradi 483 ni ya Watanzania na 196 ni ya wageni huku miradi 223 ni ya ubia.

Kwa upande wa ofisi za wabunge, Pinda alisema ofisi 40 zitakamilika kujengwa katika mwaka ujao wa fedha katika awamu ya kwanza na ofisi nyingine 10 zitaanza kujengwa. Sh bilioni moja zimetengwa kwa ajili ya kumalizia ofisi za awamu ya kwanza na kuanza ujenzi wa ofisi zilizoko katika awamu ya pili.
 
bado mpango huo unatekelezeka kabisa.tatizo ni kuwa watendaji hawataki kuutekeleza mpango huu.Nadhani kuwa na dhana kuwa mpango huo hautekelezeki ni moja ya njia ya kutotaka kuutekeleza mpango huo.Nadhani jitihada za makusudi zinahitajika kuutekeleza mpango huo na kuhamishia makao makuu rasmi mjini Dodoma.miaka 30 sio hoja ya kuachana na mpango huo ila serikali ni lazima ijipange rasmi kuhakikisha kuwa makao makuu ya nchi yanahamia dodoma kwa kuanzia na kuhamishia ikulu ya raisi na ofisi yake huko Dodoma.Pia serikali iweke mkakati wa lazima wa kuzilazimisha wizara zake zijenge majengo yake huko Dodoma na sio kuendelea kurundikana huko jijini Dar kwani mji huo sasa umezidiwa na msongamano na unahitaji tiba maalum kuuweka katika hali ya kuwa jiji.Naipongeza pia serikali kwa kuamua kuanzisha chuo kikuu cha kisasa huko Dodoma (UDOM).Pia nazipongeza taasisi za kidini kama kanisa la Anglikana kwa kuanzisha Chuo kikuu cha st.John huko na hata serikali kukipandisha hadhi ya chuo kikuu chuo cha mipango.Nadhani hiyo inaweza kuwa moja ya njia za kuufanya mji huo ukalike kwa kwani mzunguko wa pesa utaongezeka na hata idadi ya wakazi itakuwa kubwa hivyo soko la bidhaa litaongezeka na hata mabanks mengi yaenda huko hivyo wafanya kazi wengi na mwisho uchumi wa mkoa huo utapanda na kuufanya kuwe na miundombinu ya kuweza kupata hadhi ya jiji na hatimaye kuwa makao makuu kikwelikweli ya nchi yetu.
 
Bora waseme sasa, kama wanahama wahame au kama hawahami waseme, sio kudanganyana kama watoto.

Mji wa dodoma umekuwa ukipewa bajeti tofauti na miji mingine kwa miaka mingi sasa katika CDA, ni muda muafaka kusema ukweli,
 
Watupe na tarehe, ya kuhamia wizara hadi wizara.
 
Nielewavyo mimi, ni kuwa yameisha hama.

Very trenchant point. Kila siku hii ishu inakuja na kuondoka. Hakuna anaeuliza kwani mara ya mwisho tulikubaliana nini kuhusu Dodoma. Yani tunapelekeshwa tu.

(Ni sawa sawa na sasa hivi all of a sudden tunaambiwa na Mkulo eti ishu ya uchunguzi wa EPA tunasubiri Rais atamke. Wait a minute, I thought ilikuwa kwenye tume ya uchunguzi wanakusanya hela zilizoibiwa, whatever the heck that means. Sasa lini wamemaliza na lini imeenda kwenye deski la Rais tayari? Damn kuna madness Bongo.)
 
  1. Kwa msongamano uliopo DSM hivi sasa, sababu za kuhamia Dodoma zinakuwa zimeongezeka kuzidi zile za miaka 30+ iliyopita. Bado nchi yetu inahitaji Dodoma ili kutawanya maendeleo yake hasa katika kuboresha miundo mbinu yake kufikia kona zote za nchi, japokuwa kumekuwa na mabadiliko ya Teknolojia ambayo hayajali sana mahali miji ilipo ili kufanikisha utendaji.
  2. Pesa nyingi hivi sasa zinatumika kujaribu tu kulishikilia jiji la DSM kumudu msongamano uliopo. Kwa mfano, lau kama tu 50% ya magari yanayoelekea central business distrct (CBD) ya Dar kila asubuhi, maana mengi yake yanahusiana na uwepo wa ofisi za serikali, yakihamia Dodoma, pesa nyingi pia zitakuwa zimeokolewa kila mwaka, sio tu kwenye mafuta yanayotumika kukaa kwenye foleni, bali pia kwenye upanuzi usiohitajika wa baadhi ya miundo minu ya DSM.
  3. Pia, zaidi ya hapo, maisha ya watakaobakia Dar yataboreka na efficient kuongezeka, na wa Dodoma nao vile vile watafaidika na huduma mpya zitakazokuja na uwepo wa serikali hapo Dodoma.
  4. Kwa hiyo, unless mawaziri na raisi wawe wanaamkia Dodoma kuanza shughuli zao kila siku, (a) Ukuzaji wa uchumi wa mikoa mbalimbali na hatimaye nchi nzima, (b) Uboreshwaji wa miundo mbinu na hatimaye (c)Uboreshwaji wa maisha ya wananchi wa mikoa ya pembezoni, liitakuwa jambo gumu kufikiwa.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom