Je, bado kuna umuhimu wa kuhamisha makao makuu ya nchi Dodoma? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je, bado kuna umuhimu wa kuhamisha makao makuu ya nchi Dodoma?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Game Theory, Jul 3, 2007.

 1. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #1
  Jul 3, 2007
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 0
  Wa kwanza alikuwa MWALIMU akatuyeyushaweeee kumbe naye alikuwa anapenda kuishi Dar.Wanajeshi wakamjengea bonge la HEKALI huko BUTIAMA lakini wapiiii, Mwalimua aliamua kuishi butiama ya DAR

  Akaja MWINYI, na kama jina lake lilivyo, huyu yeye ni MWINYI sasa nadhani mnaelewa kuwa mamwinyi sikuzote hawajiwezi kwenye miji isiyo na bahari.

  Akaja MKAPA, huyu alikuwa anajidai ana mambo ya KIZUNGU na vile vile ile mitikasi ya mkewe MAMA ANNA MKAPA kuwatapeli wazungu na NGO za kimataifa zisingewezekana kama MKAPA angehamia DODOMA

  JK of course huyu naye ni MWINYI na mtoto wa MJINI na nina hakika huko Dodoma hawana SAIGONI hivyo lest rule him out kuhamia huko

  MZEE KINGUNGE ndio nasikia peke yake ndio yuko huko.

  Lawama zaidi nazielekeza kwa MZEE MALECELA alitakia apush zaidi lakini wapi!

  WAPINZANIA nao wote wako mjini Dar wanazuga tuuu
   
 2. KadaMpinzani

  KadaMpinzani JF-Expert Member

  #2
  Jul 3, 2007
  Joined: Jan 31, 2007
  Messages: 3,749
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  baada ya kuongelea mambo yatakayowezesha watanzania kunufaika, ndio kwanza serikali inafikiria starehe zao wenyewe, kwani wakihama huko au wakibaki Dar kuna nini, sasa mimi nashauri kokote wakibaki ni fresh tu ! waache starehe zao !
   
 3. KadaMpinzani

  KadaMpinzani JF-Expert Member

  #3
  Jul 3, 2007
  Joined: Jan 31, 2007
  Messages: 3,749
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  ndio zao hao kuongelea kujenga maofisi yao, kuwaambia waandishi wa habari waweke ukurasa wa watz waliopo nje kwenye site ambayo imechukua muda wooote huo tokea waingie madarakani, lakini ukiwaambia kwenda kwenye semina nchi ya nje wanafanya fasta fasta !
   
 4. D

  DAR si LAMU JF-Expert Member

  #4
  Jul 3, 2007
  Joined: Mar 31, 2007
  Messages: 2,942
  Likes Received: 286
  Trophy Points: 180
  ....inakumbukwa na kupewa bajeti itakayowezesha kutoa ajira mpya,vifaa na kuendeleza miradi iliyokufa...ooh...kufufua.

  ....baada ya hapo,pale mheshimiwa rais atakapoamua kukaa dom angalau kwa miezi sita solid!

  ....inahitaji kukaza msuli though!
   
 5. S

  Samvulachole JF-Expert Member

  #5
  Jul 3, 2007
  Joined: Oct 22, 2006
  Messages: 410
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 45
  NA ILE cda SIJUI IKUFIA WAPI

  AMA KWELI NJI HII IMEKUWA YA KUSADIKIKA
   
 6. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #6
  Jul 3, 2007
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,364
  Likes Received: 6,394
  Trophy Points: 280
  inaonekana wote mmemiss jibu la Waziri Mkuu jana.. kasema watahamia Dodoma kwa awamu..! (whatever that means)
   
 7. D

  DAR si LAMU JF-Expert Member

  #7
  Jul 3, 2007
  Joined: Mar 31, 2007
  Messages: 2,942
  Likes Received: 286
  Trophy Points: 180
  ...kila anachosema kinaaminika?

  ...wote husema hivyo hivyo,halafu CDA haikatiwi mafungu!
   
 8. Mtoto wa Mkulima

  Mtoto wa Mkulima JF-Expert Member

  #8
  Oct 11, 2007
  Joined: Apr 12, 2007
  Messages: 687
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Jamani kuuliza si ujinga.

  Mimi nijuavyo Ofisi ya waziri mkuu iko Dodoma na Ministry of Regional Administration and Local Government ambayo pia iko chini ya waziri mkuu iko dodoma. Kwa ninavyojua ni kuwa wizara zote zilikuwa haziruhusiwi kujenga Dar mimi nina muda sijafika Tz muda ila nasikia Hazina wamejenga jengo zuri sana, wizara ya aridhi nao, Utumishi nao kule magogoni pia makamu waraisi nae anajengewa Dar.

  Sasa nachouliza ni kwanini serikali isihamie Dodoma kwa kuanzia na raisi? Au

  Kwanini Bunge na wizara mbili zilizoko Dodoma zisihamishiwa Dar?

  Naauliza hivi kwa sababu swala la serikali kuwa nusu Dar nusu Dodoma ni gharama kubwa sana kwa serikali.

  1. Unajua makatibu wakuu wote, wakurugenzi, makamishina, wakuu wapolisi na magereza, na maofisa wa serikali wanalipwa Per diem kwa kipindi choote cha Bunge?

  2. Unajua magari karibu yote ya serikali yanakuwaga Dodoma kwa kipindi chote cha bunge na madereva wote wanalipwa per diem?

  3. Unajua maofisa wa wizara zilizoko dodoma kila mara wapo Dar kwa vikao na walipwa na kodi za wananchi?

  4. Unajua oofisi zote za sirikali kukaa posta kunachangia sana foleni Dar? na hili ukitaka kujua wakati wabunge barabara ni nyeupe.

  5. Wizara ya East Africa community iko dar lakini zaidi ya robo tatu ya mwaka shughuli zake zinafanyikia Arusha?


  Nilikuwa naongea na jamaa ananiambiua nasubiri kuweka nyumba bati ni kienda dodoma bungeni. Na kila wizara inatuma karibu maofisa 50. kwa wizara zote zidisha na posho ya 50,000 kwa siku kwa muda wote wa bunge.


  Hili nimelifikiria kwa sababu matumizi yetu ya kawaida ni makubwa sana ukilinganisha na matumizi ya maendeleo. Mfano 80% ya matumizi ya maendeleo yanafadhiliawa na DOnors (Development budget) nna 20% ni kutoka pesa za ndani zikiwemo mikopo. Wakati huo huo budgeti yote zaidi ya 40% inategenmeea wafadhili.
   
 9. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #9
  Oct 11, 2007
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,690
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Mtizamo Mwingine,

  Nadhani tufuate Africa Kusini (South Africa) Wanavyofanya!!! Tuachane na Dhana ya kuhamisha kila kitu Dodoma!!! Badaya lake tuangalie namna gani tutaweza tawanya Makao Makuu ya mihili mitatu ya Jamhuri!

  BUNGE --- DODOMA
  SERIKALI KUU --- DAR ES SALAAM (Maana hapaonyeshi kwamba wanataka kuhama)

  MAHAKAMA --- MWANZA/ARUSHA

  SERIKALI ZA MITAA --- DODOMA

  Kwa maoni yangu hii inatekelezeka na haitaicost serikali Hela Nyingi, lakini pia ina faida ya kuijenga miji yote hence kufanya kasungura kagawanywe vizuri,,, South Africa Wanafuata Mfumo huo...

  AIDHA Nakubaliana kwamba Wizara Ya Afrika Mashariki, Makao Makuu yawe Arusha
  Naomba kuwasilisha
   
 10. Mtoto wa Mkulima

  Mtoto wa Mkulima JF-Expert Member

  #10
  Oct 11, 2007
  Joined: Apr 12, 2007
  Messages: 687
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0

  Mkuu mawasiliso yako yamefika JF na yamepokelewa.:rolleyes:
  Mkuu sio siri hii issue inakula pesa hata kuliko hayo mashangingi ya serikali. By the way nilisiki chuo kikuu cha Dodoma kingeanza kazi vipi kimeshaanza?
   
 11. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #11
  Oct 11, 2007
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,690
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Chuo kikuu cha Dodoma kimeanza kwa wanafunzi 1000 kama sikosei na mkuu wa chuo ni HE. Ben Mkapa...


  sijui website yao well hii inawezakukusaidia kidogo

  By the way mtoto wa mkulima, ulikuwa maeneo ya mwenge ukifanya shughuli zako miaka 3-5 iliyopita? kidogo kama na-recall kitu kuhusu wewe!
   
 12. Mtoto wa Mkulima

  Mtoto wa Mkulima JF-Expert Member

  #12
  Oct 11, 2007
  Joined: Apr 12, 2007
  Messages: 687
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Hapana mkuu nimeondoka nyumbani kama miaka sita sasa. Ila kuna jamaa zangu mwenge wengi tuu maana nilikuwa nafanya reseach ya cluster development kwa washona nguo wa mwenge mkuu nilikuwa nakusanya data na soon nitarudi nyumbani pia ku revisit pale pia.
   
 13. Idimi

  Idimi JF-Expert Member

  #13
  Oct 11, 2007
  Joined: Mar 18, 2007
  Messages: 10,222
  Likes Received: 2,088
  Trophy Points: 280
  Nakubaliana na wewe Mtoto wa Mkulima. Hili suala tumeliongelea sana sisi wataalamu wa mipango miji, lakini naona 'watawala'wetu hawataki kabisa kutuelewa na wameziba masikio. Suala la kujaza kila ofisi ya umma pale katikati ya jiji linaboa sana! Mfano, makao Makuu ya jeshi la polisi yako huko, wizara za maji, elimu, afya, kazi, nishati na madini nk zote zinapatikana huko, hospitali zote kubwa ziko huko, huduma za vizazi na vifo ziko huko. Sasa suala hili linaongeza uwingi wa watu na magari usio wa lazima katikati ya jiji. Baada ya kukosa maegesho, baadhi ya wenye magari huegesha popote palipo na uwazi, na matokeo yake magari yao huburuzwa bila huruma na mawakala wa watawala. Tunalalamika kwa sababu iwapo majengo mengi ya wizara yapo posta na magogoni inamlazimu kila mtu kwenda huko katika muda wa kazi (saa 2 asubuhi hadi saa 10 jioni, kwa hiyo hii huongeza msongamano. Jiji lina wataalamu wa mipango miji, kila manispaa Dar ina wataalamu wa mipango miji, kwani kazi yao ni ipi hasa?
  Kwanza, tunataka majengo kama 'Ubungo Plaza' na 'Millennium tower' yajengwe mengi sana maeneo kama Bunju, Tegeta, Boko, Mbweni, Bagamoyo, Chanika, Mbezi, Kibamba na kadhalika, ili kupunguza msongamano. Suala hili litawafanya watumishi katika majengo haya kupishana nyakati za asubuhi na na jioni kunapokuwa na pilika, kwamba mtu anaishi Mbagala, anakwenda kazini ama kufuata huduma za wizara Boko, mtu anaishi Mwenge, anakwenda kazini Kibamba nk, tofauti na sasa ambapo watu wengi sana wanafuata huduma hizi katikati ya jiji.
  Pili, nakubaliana na hoja ya Mtoto wa Mkulima kuhusu 'Decentralization' yaani mgawanyo wa madaraka. Kwamba, kuwe na mawakala wa ofisi zote kuu mikoani ama baadhi ya wizara ziwe mikoa mbali mbali ili kupunguza msongamano jijini. Tufanye kama walivyogawanya matawi ya Benki Kuu na Mahakama Kuu za kanda, kwamba watu sasa hawalazimiki kufuata huduma za taasisi hizi jijini Dar. Inawezekana pia kuwa viongozi wanagoma kuhamia Dodoma ili waendelee kujilipa per diem kwa 'kusafiri'. Huu ni uhuni na ni usanii. Nadhani tumuulize muungwana kuwa ni lini atahamishia Ikulu Dodoma ili kila mtu amfuate?
   
 14. Mtoto wa Mkulima

  Mtoto wa Mkulima JF-Expert Member

  #14
  Oct 11, 2007
  Joined: Apr 12, 2007
  Messages: 687
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  mkuu akihamia DODOMA wengine watafuata ila sasa Dar ni kama administration cluster maana mashirika yote kama UN,Labour, WB & IMF, Balozi zote ziko Dar sasa kama serikali ikihamia kule transaction cost nazo zitakuwa kubwa sana.
   
 15. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #15
  Oct 11, 2007
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,690
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  As said before siungi mkono serikali yote kuhamia Dodoma, it is expensive and it is not priority now!

  BUNGE- DODOMA
  MAHAKAMA - ARUSHA/MWANZA
  SERIKALI KUU - DAR ES SALAAM
  SERIKALI ZA MITAA - DODOMA

  WIZARA YA AFRIKA MASHARIKI - ARUSHA....  Issue ya cost ya wakati wa vikao vya bunge,,, ni ujina wetu tu,,, kama kungekuwa na shutle busses first class za serikali za kuondoka kila baada ya saa 3-4 nne, tungekataa kabisa zaidi ya mawaziri watu wengine kuwa na magari ya serikali wakati wabunge period,,, problem ya nchi yetu watu wetu wakigombea ubunge wazuri baada ya hapo wanatusahau!!!
   
 16. Mtoto wa Mkulima

  Mtoto wa Mkulima JF-Expert Member

  #16
  Oct 11, 2007
  Joined: Apr 12, 2007
  Messages: 687
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Mkuu nimekuelewa kabisa na hapa kunaishue ya kumake shure bara bara iko safi kabisa na pia reli ya kati ikiwa inafanya kazi freshi nadhani usafiri wa mabasi unaweza kuwa bomba tuu ila kwa hali kama sasa nasikia kunawakati hata kupata tiket ni shida maana tren ya kati (Mwanza,tabora na Kigoma) huwa inaanzia Dom kwa hiyo watu wanakuwa wengi sana. Unajua kweli mambo mengine ni aibu yaani reli iliyojengwa na Mkoloni mjerumani zaidi ya karine moja tunashindwa hata kuikarabati? kweli we are not serious. Unajua ukitoka Dar ukifika Mezani kibaha unakuta foleni kubwa ajabu ya malori na hakika reli ingefanya kazi hili lisingekuwepo na hata bara bara zisingechakaa haraka vile maana magari yanabeba mizigo mikubwa kuliko uwezo wa bara bara na ajili za magari pia zingepungua. (sorry ni nnje ya topic ila wazo limenijia tuu)
  Aisee kunakitu sielewi kidogo naombeni mnijulishe. Hivi hata wabunge nao wanalipiwa mafuta ya mashangingi yao na serikali? Halafu ile issue ya Constuency Fund ilifikia wapi?
   
 17. Madela Wa- Madilu

  Madela Wa- Madilu JF-Expert Member

  #17
  Oct 11, 2007
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 3,074
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  Siku Bahari ikihamia Dodoma
   
 18. Mtoto wa Mkulima

  Mtoto wa Mkulima JF-Expert Member

  #18
  Oct 12, 2007
  Joined: Apr 12, 2007
  Messages: 687
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  kwi kwi kwi kwi! nakupata hapo najua umetumia lugha ya picha Madilu ni kwamba haitakaa ihamie Dodoma maana ni jambo lisilo wezekana. Nilipokuwa nasoma geografia nilia mbiwa nchi ya Duch ilijengwa na waduch (Reclaimed land) na hicho kitendo kinaitwa land reclamation je kitendo cha kujenga bahari tuite je? au ni sea reclamation? joke.
   
 19. M

  Msesewe Senior Member

  #19
  Oct 12, 2007
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 102
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Waungwana,
  Mawazo ni mazuri sana, ila utekelezaji wake vipi? TANROADS wameshanunua viwanja 3 na wanataka kujenga makao makuu ya city center Wizara ya mambo ya ndani wankamilisha jengo lao City center, kila kitu city center.. nani wa kulisemea hili?? Je kusema tuu kwenye JF inatosha? mimi ni mgeni ila naomba mawazo yenu kwa nini Tanroad wajenge head office city center? kwani wakijenga kule mabibo au dodoma au arusha au mbeya itakuwaje?

  Jamani Watanzania tuamkee
   
 20. K

  Kithuku JF-Expert Member

  #20
  Oct 12, 2007
  Joined: Nov 19, 2006
  Messages: 1,395
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 145
  Hawahamii Dodoma hawa jamaa. Labda ungezungumza kuhamia BAGAMOYO kidogo wangekuelewa!
   
Loading...