Je, Askofu Malasusa anamchukia Mchungaji Kimaro?

Sep 17, 2021
39
84
Nimeona mahubiri Ya Askofu Malasusa akiwashambulia watumishi wa Mungu ambao kwa madai yake yeye, waanaminiwa sana na waumini wao.

Askofu Malasusa anadai wachungaji hao wanaamini sana na watu kuliko Yesu.

Mahubiri haya yanayoonesha chuki ya Askofu Malasusa kwa watu kama Kimaro (wengine kama kina Mbiso wa Mbezi Beach, mchungaji wa Kariakoo na yule wa Kimara wanaweza kuingia kundi hili), hayashangazi kwa sabababu Malasusa anajulikana kuwa mtu wa ugomvi na visasi.

Ogopa sana Askofu ambaye alisema maaskofu na wachungaji wa Dayosisi ya Konde wafukuzwe kwenye msiba baba yake, mtu anayeweza kufukuza watu msibani ni wa kuogopwa kama Wafilisti.

Hajanishangaza ila amenisikitisha kwa sababu; Ameonesha wazi kuwa na shida na wachungaji aina ya kina Kimaro, na bila shaka mahubiri yake yalimlenga Kimaro.

pia, Askofu aelezwe kwamba hicho ambacho yeye anakiita kwamba “waumini wanamuamini mchungaji kuliko Yesu” hakijatengenezwa na hao wachungaji. Waumini hawaamini wachungaji kuliko Yesu, lakini wanaamini hao wachungaji ni viongozi wema kuwaongoza kumuendea Yesu, na hiyo ndiyo maana ya Kanisa.

Nadhani alipaswa kushangilia kwamba waumini wanaelewa sana hao wachungaji badala ya kununa, na kukuza maneno kwamba eti wachungaji wanaaminiwa kuliko Yesu.

aidha. Malasusa anataka kupuuza haja ya mioyo ya waumini kuishi na mchungaji wanayemuelewa?


Anataka kupuuza haja ya mioyo ya Wakiristo kwenda katika makanisa ambayo yanawapa upako kwa sababu watendaji wa Bwana katika mashamba hayo wanafanya kazi njema?

Aambiwe kwamba Waumini wakimpenda Mchungaji, mchungaji anapaswa kuachwa hapo na kusifiwa sio kupigwa vita.
 
we stand with him
FB_IMG_1673946261123.jpg
 
Nakuunga mkono sana... huyu baba amenifanya nikaacha kwenda kanisani kkkt kabisaaa... Kwanza alikua na kashfa ambazo hatukupewa hata majibu... amebadilisha katiba ili atawale na hii dayosis ameifanya kama Saccos yake
 
Unapo kuwa muongo.. Usiwe msaulifu. Mwenye asili..haachi asili yake. Ukiwa mroho usiwe mchoyo. HAYA yote yanatokana na utashi wa mwanadamu, pale anaposikia ukweli na akawa yupo kwenye kundi mojawapo lazima aje juu. Kwa sababu ukweli unauma hata mimi nasema kweli waizi mbona sadaka zinafichwa mbona michango inazidi.
 
Malasusa anajihisi ndiye Baba Mtakatifu wa KKKT! Si alishastaafu huyu! Apumzike huko aache watendakazi shambani mwa Bwana watende kazi zao kadiri ya wito walioitiwa bila kuonewa kijicho!
 
Niseme tu, hakuna marefu yasiyo na ncha.
Kilichokuwa kinatakiwa kufanyika ni kum demolish Kimaro tangu akiwa Usharika wa Kariakoo.

Kwa miaka mingi tumefanya mbinu na njama mbalimbali kumuondoa lakini hazikuwq na matokeo tuliyo yatarajia. Hivyo tukajaribu mbinu nyingine na nyingine tena, hatimaye leo mbuyu haujaanguka ila umemwagika.

Mara ya kwanza tulipofanya yetu akiwa pale Kariakoo alikimbia usharika na kwenda kujificha kwa Mapadre, na mapadre ndio waliofanya jitihada hadi akarudi tena usharikani, ila hii ya sasa harudi, na akirudi basi itakuwa zamu yetu kusalimu amri.

Kimaro alipokuwa Kariakoo, sio kwamba aliharibu taratibu za ibada hapana, hii ni cover tu, tunayoitumia.

Kimaro alipokuwa Kariakoo aliharibu biashara za wengi kwenye ulimwengu wa roho.

Watu walikuwa na madhabahu zao kubwa ambazo ziliprovide ulinzi wa pesa na mali, pia zikikuwa zikivuta mali kutoka kwa maboya wengine.

Alipofika Kimaro, wale ambao tulikuwa tukizivuta mali zao, wakaanza kumiminika kule kila alfajiri, ulinzi wa mali zao ukaanza kuongezeka, na zile biashara zao ambazo tulizifanya zisionekane na wateja zikaanza kuonekana, na taratibu taratibu wakaanza kukua na kutupora wateja wetu.

Kwa msio na ufahamu wa biashara, hamna biashara isiyo na madhabahu (iwe ya asili au hizo kama za Kimaro), hamna biashara isiye na kuhani, na wala hamna biashara isiyotolewa sadaka/kafara.

Watu wakaanza kufundishwa kutoa sadaka za maneneo na manuizi kwa ajili ya biashara zao, tukapata upinzani sana.

Kwa kushirikiana na wenzetu ndani ya kanisa, tukaanza figisu. Ibada hizo mpya zifutwe na ikiwezekana Kimaro ahamishwe Kariakoo.

Tukafanya Kimaro apitie magumu, tukakausha kabisa hali ya utoaji wa sadaka hadi kanisa likashindwa kulipia umeme na maji, tukahakikisha wanapitia kwenye hali ya ugumu kweli kweli.

Baadae Kimaro anajua alichokifanya, akapindua meza, hali ya uchumi wa kanisa ikaimarika sana, likawa pigo lingine kwetu.

Kipindi kile mkuu wa kanisa alikuwa yule jamaa wa Mbeya, tukafanya kila liwezekanalo ahamishwe. Ndipo akapelekwa Kijitonyama.

Zama zile Kijitonyama alikuwepo dogo mmoja anaitwa Kinyaha, hayo mambo ya ibada za asubuhi yalikuwa hayapo au yamekufa kabisa.

Ibada ilikuwa ikihudhuriwa na vizee vienne, wakizidi sana sita. Sasa alipokuja Kimaro sijajua alikuja na mguu upi, akaleta ibada za asubuhi na usiku.

Watu wakaanza kufurika, akaanza kununua nyumba za watu wetu na kuzifanya kuwa za kanisa. Kijitonyama yote ilikuwa ni ngome yetu.

Kata ya Kijitonyama ndio kata ina vijiji viwili mjini kati Dar es Salaam. Kijiji cha Mwenge na Kijiji cha Makumbusho. Jina na asili Kijitonyama sitaki kulielezea leo, lakini kaa ukijua kuwa ile ni ngome yetu na sehemu yetu ya kulia nyama na vitu vyetu vya kutuongezea nguvu. Kijitonyama ndiko kwenye madhabahu ya kuteketeza, ndio maana hata Wahindi miili yao huchomewa Kijitonyama.

Pale tulijaribu mbinu za kishushu, kuna kipindi tulitaka kumfitinisha na serikali kwa kupitia kijana aliyejinyonga kwa madeni aliyokuwa nayo, lakini alikwepa vihunzi kwa namna ya ajabu kabisa.

Kwetu sisi ni furaha, watu waharibifu aina ya KIMARO hawafai, wakakae huko vyuoni wafundishe. Na tutammaliza kwa njia hiyo.
 
Kama uliyoandika kiranja mkuu ni kweli. Basi Waliomuondoa kimario ni genge hilohilo. Inashangaza mtu kandaa ibada ya kufunga na kuomba, kabla ya kuanza unamsimamisha. Kkkt ilipoteana sana katika mambo ya kiroho. Wachungaji kama kimario wameleta uamsho ndani ya kanisa.

Angalau Leo waumini wameanza kukua kiroho. Bwana akamheshimisha kimario. Lakini viongozi wakajaa chuki dhidi yake. Heri watubu, maana wayafanya yamwili kuliko wito walioitiwa.
 
Kuanzia kipindi cha Kikwete na Magufuli, siasa zililimeza kanisa. Wachungaji wenye asili ya Kaskazini walichukiwa sana, wakaonekana ni tishio kwa kanisa. Tena wakapewa jina eti ni Machadema.
 
Mchungaji Rich bilionear ana kwambia "binadamu wanatafuta majibu"
tatizo la makanisa na misikiti kwenye ibada wanatuongezea maswali sio jibu.
Rich Bilionea alishtuka mapema akaomba kustaafu kwa hiari sasa hivi yupo huru anahubiri injili na kusaidia makundi yaliyosahaulika huko KKKT
 
Nimeona mahubiri Ya Askofu Malasusa akiwashambulia watumishi wa Mungu ambao kwa madai yake yeye, waanaminiwa sana na waumini wao...
Askofu Malasusa na Dk. Shoo ndio mafisadi wakubwa wa Mali za kanisa, na wanashirikiana na kulindana.

Walienda Mbeya kutumia hoteli ya kanisa kukopa mabilioni wajenge chuo kikuu

Wakakopa, Hela wakabeba, chuo hawakujenga.

Baadae wanaenda mbeya na mteja wao wanamlazimisha Mwaikali auze hoteli ya kanisa, Mwaikali akakataa, mteja alishawaahidi ten pasenti, akaanzishiwa vita Kali kwelikweli mpaka akalazwa rumande.

Na hao maaskofu wanahonga kuliko inavyofikiria.

Dk Shoo ni askofu bilionea kuliko wote Afrika kwa wale wa KKKT, anachofanya ni kujificha Chadema ili wamtetee siku serikali ikianza kumuandama.

Na pia Kimaro alikuwa anaelekea kuwa Askofu wa Jimbo la Dsm, katika kulindana, mkuu wa kanisa na Malasusa wakaandaa njama hizo
 
FEDHA NDICHO CHANZO CHA HAYA YOTE, YESU ALIKEMEA SANA SUALA LA BIASHARA KATIKA MASINAGOG, TUTAZUNGUKA SANA LAKINI CHANJO CHA HAYA YOTE NI BIASHARA KATIKA NYUMBA ZA IBADA.
 
Kama uliyoandika kiranja mkuu ni kweli. Basi Waliomuondoa kimario ni genge hilohilo. Inashangaza mtu kandaa ibada ya kufunga na kuomba...

Ungeuliza sababu ya kwa nini kasimamishwa kwa siku sitini. Kimaro kaliita kanisa lake KKKT ni la madalali na Katoliti ndio misheni ya kweli. Hizo ngojera za kuleta watu hazitoi uhalali wa wewe kulitukana kanisa. Cha muhimu akafungue kanisa lake.
 
Back
Top Bottom