Je, asili ya majini ni ipi?

Je, asili ya majini ni ipi?

Ingekuwa ni ibilisi ni malaika basi asingepambanuliwa kwa jina.Lakini ametajwa kwa jina ili atu wapambanukiwe ya kuwa ibilisi alikuwa katika kundi la malaika,yaani katika lile kundi la malaika naye ibilisi alikuwemo.Mfano sahali,ukiambiwa katika msafara wa mamba na kenge wamo,hii haimaanishi kenge nao ni mamba,bali umefafanuliwa tu ili upate kumakinika na kupata ujumbe uliokusudiwa.Mfano mwingine ni kuwa,chukulia ya kuwa kuna mbuzi anaitwa mkono,katika malezi mbuzi yule alikuwa pamoja na kondoo kadhaa,siku nilipowaswaga kwenda malishoni kondoo wote walienda kula isipokuwa mkono.Hapa katu huwezi kusema mkono naye ni kondoo kisa alikuwemo katika kundi la kondoo,achilia mbali hapo kabla ulishapewa habari ya kuwa mkono ni mbuzi.Sasa ukija kutuambia tena mbuzi huyo kaja kuwa kondoo,bila shaka wewe una elimu ya ziada juu ya mabadiliko hayo,na unatakiwa utueleze vipi mbuzi kawa kondoo.Ukishindwa kutuonyesha lazima utakuwa na ususuavu wa moyo na ufikiriaji wa kitoto.Wakiristo mjifunze kuweka kila kitu mahala pake.
Mbona Malaika alimtokea Muhammad na alitajwa kwa jina Gibril? Malaika wote kwa Mungu wanamajina yao siyo lazima Mungu awaambie majina ya wote. Na sikosei kuran inamtaja malaika Mikaeli.
Kama unadai Ibilis siyo jina ni maana nyingine kama mpinzani, basi malaika mmoja aliamua kuwa mpinzani katika hilo andiko. Au inabidi watafsiri wa Qur'an warekebishe pale lakini kwa bahati mbaya tafsiri za Qur'an kwa lugha ya kiswahili na kiingereza ziko nyingi tu na haiwezekani kubadilishwa.

Kwa kifupi, malaika wana majina kaka.
 
Ingekuwa ni ibilisi ni malaika basi asingepambanuliwa kwa jina.Lakini ametajwa kwa jina ili atu wapambanukiwe ya kuwa ibilisi alikuwa katika kundi la malaika,yaani katika lile kundi la malaika naye ibilisi alikuwemo.Mfano sahali,ukiambiwa katika msafara wa mamba na kenge wamo,hii haimaanishi kenge nao ni mamba,bali umefafanuliwa tu ili upate kumakinika na kupata ujumbe uliokusudiwa.Mfano mwingine ni kuwa,chukulia ya kuwa kuna mbuzi anaitwa mkono,katika malezi mbuzi yule alikuwa pamoja na kondoo kadhaa,siku nilipowaswaga kwenda malishoni kondoo wote walienda kula isipokuwa mkono.Hapa katu huwezi kusema mkono naye ni kondoo kisa alikuwemo katika kundi la kondoo,achilia mbali hapo kabla ulishapewa habari ya kuwa mkono ni mbuzi.Sasa ukija kutuambia tena mbuzi huyo kaja kuwa kondoo,bila shaka wewe una elimu ya ziada juu ya mabadiliko hayo,na unatakiwa utueleze vipi mbuzi kawa kondoo.Ukishindwa kutuonyesha lazima utakuwa na ususuavu wa moyo na ufikiriaji wa kitoto.Wakiristo mjifunze kuweka kila kitu mahala pake.
Kwani ukikubali mmoja wapo kati ya hao malaika aliasi kuna tatizo gani?
Mifano uliyotoa ya mamba, mjusi, mbuzi na mkono kwa kweli ni siyo ya lazima. Tujikite kwenye andiko siyo kuruka ruka kama chura!
Sura 2:34 imejitosheleza kwa kusema
" Na TULIPO WAAMBIA MALAIKA: MSUJUDIENI ADAM,WAKAMSUJUDIA WOTE ISIPO KUWA IBLIS, ALIKATAA..." Hapo inatosha kuelewa iblis asili yake ni nini! Kwa mifano yako unazidi kujichanganya!
 
Shetani Ni Nani?
Sisi hatujamwona Shetani ana kwa ana lakini ametolewa habari zake na wahyi. Kwa hivyo ni wajibu kusadiki kuwa yupo, na si wajibu kujua alivyo.
Mwenyezi Mungu (S.W) amemtaja katika Qur’an kwa sifa ya kupoteza watu na kuwaepusha na twaa ya Mwenyezi Mungu na amali ya heri. Kwa hiyo kila wazo linalokupitia moyoni au mtu anayejaribu kukuhadaa kukuweka mbali na twaa na kheri ya Mwenyezi Mungu, kukuhadaa kuasi sharia na kuuvika uovu na ubatilifu nguo ya uongofu, basi huyo ni Shetani wa hisia au wa kimaana.
Jambo la kushangaza ni kuwa “mashetani watu” nao wanaomba walindwe na shetani, hali wao wenyewe ni mashetani lakini hawajijui. Ni sawa na mtu anayesoma Qur’an na huku inamlaani mwenyewe; kama ilivyoelezwa katika hadith.
Qur’an inamlaani mwongo aliye haini. Kwa hivyo huyo mwongo anapoisoma huwa amejitamkia laana yeye mwenyewe.
Mwenyezi Mungu anasema:
ﺃُﻭﻟَٰﺌِﻚَ ﺟَﺰَﺍﺅُﻫُﻢْ ﺃَﻥَّ ﻋَﻠَﻴْﻬِﻢْ ﻟَﻌْﻨَﺔَ ﺍﻟﻠَّﻪِ ﻭَﺍﻟْﻤَﻠَﺎﺋِﻜَﺔِ ﻭَﺍﻟﻨَّﺎﺱِ ﺃَﺟْﻤَﻌِﻴﻦَ {87}
“Hao malipo yao ni kushukiwa na laana ya Mwenyezi Mungu na ya Malaika na ya watu wote.” (3:87)
Hukumu
Kusoma Au’dhu... kabla ya kusoma Qur’an ni sunna, wala si wajib; ni kama vile kuosha mikono na kusoma Bismillah kabla ya kula. Lau hiyo Au’dhubillahi ingelikuwa ni wajibu ingeliwajibishwa katika swala, mahali pa fatiha na Sura. Wanavyuoni wote wamesema kuwa si wajib.
Mwenye Miftaahul-Karaama amesema:”Hawakuhitalifiana katika hilo isipokuwa Ibn al-Junaid ambaye mafakihi wamemwita: ‘aliyejitenga’.”
Mantiki Ya Iblis
Kwa mnasaba wa Au’dhu (kujilinda na Shetani) nitadokeza vigano alivyonasibishwa navyo Ibilisi.
Kwa sababu ingawaje ni vigano, lakini vina picha wazi kwa watu wengi wa zama hizi; hasa wale wanaotaka kujinufaisha bila ya kuangalia maslahi ya wengine, kwa kufanya mbinu za kujaribu kila njia ya kucheza na maneno na kuficha haki.
Tutayaonyesha hayo kwa matamko tu; bila ya kudhihirisha madhumuni.
Inasemekana kuwa Ibilisi alimwambia Mwenyezi Mungu (s.w.t): “Haijuzu kuniadhibu kwa kuacha kumsujudia Adam.” Mwenyezi Mungu akamuuliza, “Kwa nini?”
Akajibu: “Kama ungelitaka hasa nimsujudie ungenifanyisha kwa nguvu.”
Mwenyezi Mungu (s.w.t.) akamuuliza: “Wakati gani ulijua kwamba sikukutaka umsujudie Adam? Je ulilijua hilo baada ya kukuamrisha na kuasi amri yangu? Au kabla ya kukuamrisha kusujudu?”
Akasema: “Ni baada ya kuniamrisha”.
Mwenyezi Mungu (s.w.t.). Akasema: “Basi umejishinda. Kwa sababu ulihalifu kabla ya kujua kuwa Mimi niliyataka yale uliyoacha kuyafanya. Zaidi ya hayo kama ningekufanyisha kwa nguvu, basi isingelikuwa amri.”
Utaona katika mantiki ya Ibilisi sura iliyo wazi kwamba Mwenyezi Mungu hawafanyishi wenye kuwajibikiwa na sharia kama vile anavyofanya katika kuumba kwa njia ya “kun fayakun” (kuwa, ikawa). Isipokuwa anawafanyisha kwa njia ya kuongoza matakwa ya mtu kwa sharia inayoelezwa ya kuamrisha mema na kukataza mabaya.
Inasemekana kuwa siku moja Ibilisi alikutana na Mtume Muhammad (s.a.w.) akamwambia: “Hakika Mwenyezi Mungu amekusifu kwa jina la kiongozi, na mimi amenisifu kwa jina la mpotezaji. Lakini uongozi na upotezaji vyote vinatokana na Yeye, kwa hiyo wewe na mimi hatuna chochote.”
Mtume akasema: “Hapana! Mimi hubainisha batili na kuikataza na kuitolea kiaga kibaya; hali wewe una unafiki na hadaa ya ubatilifu; na mtu ana uwezo, upambanuzi na hiyari. Kwa hivyo mwenye kufanya hiyari nzuri (akaongoka) anajifanyia mwenyewe, na mwenye kuifanya mbaya (akapotea) pia anajifanyia mwenyewe.”
Imesemekana kuwa Ibilisi alimwendea Nabii Isa (a.s.) akamuuliza: “Si unadai kuwa wewe una daraja kubwa kwa Mungu? Basi hebu jitupe kutoka juu tuone, je atakuokoa?”
Masihi akasema: “Hakika Mwenyezi Mungu ndiye anayemjaribu mja wake na sio mja kumjaribu Mola wake.” Imesemekana kuwa baada ya gharika na kukauka maji, Ibilisi alimwendea Nuh (a.s.) akamwambia: “Hakika wewe umenisaidia, kwa hiyo ninataka kukulipa.”
Nuh (a.s.): Akasema: “Mungu apishe mbali! kumsaidia na kiumbe kama wewe.”
Akasema Ibilisi: “Ndio hivyo.”
Nuh (a.s.): Akasema “kwa nimekusaidia nini?
Akasema Ibilisi:“Umewaapiza watu wako ili waangamie wakaangamia, na nilikuwa nikijishughulisha usiku na mchana kuwapoteza kwa muda huo. Baada ya kuaangamizwa watu wako, sina kazi ya kufanya; sipati wa kumpoteza.”
Nuh (a.s.) akasema: “Utanilipa nini?
Akasema: “Ninakunasihi usikasirike, kwa sababu hasira ya mtu inarahisisha kunifuata. Wala usihukumu kati ya watu wawili. Kama ukifanya hivyo, basi mimi nitakuwa wa tatu wenu. Wala usikae faragha na mwanamke kwani mimi hukuvutia kwake na yeye humvutia kwako.”
Kutokana na mantiki hii ya kishetani, inaonyesha kuwa Shetani ndiye mchochezi, na kwamba yeye huzipongeza silaha zenye kuangamiza.
Inasemekana kwamba Mtume (s.a.w.) na sahaba zake walimpitia mtu mmoja akirukuu na kusujudu kwa unyeyekevu. Wakasema: “Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Ni uzuri ulioje wa swala ya mja huyu!” Mtume akasema: “Huyu ndiye aliyemtoa baba yenu peponi.”
Lengo la hekaya hii ni kuwa haifai mtu kughurika na kuhadaika kwa zuhudi na ibada ya dhahiri.
Inasemekana kuwa Nabii Musa (a.s.) alikuwa akienda kuzungumza na Mola wake, ikatokea kukutana na Ibilisi, akamwambia “Unakwenda wapi ewe uliyezungumza na Mwenyezi Mungu?”
Nabii Musa (a.s.) akasema: “Ninakwenda kwa Mola wangu kupokea maneno kutoka kwake na niko tayari kukuombea akusamehe kama utaniahidi kuung’oa upotevu wako.”
Ibilisi akasema: “Mimi sina haja ya kuombewa na wewe wala mwingine, bali ni juu Yake Yeye Mungu kutaka radhi yangu.” (Mungu apishe mbali).
Musa (a.s.) akamwambia: “Kafiri mkubwa we Mwenye laana!”
Ibilisi Akasema: “Kwani nina dhambi gani mimi? Mungu alinitaka nimsujudie Adam, na mimi kwa iIkhlas yangu, siwezi kumsujudia asiyekuwa Mwenyezi Mungu. Sasa tangu lini Ikhlas ikawa ni dhambi?”
Musa (a.s.) akamjibu: “Hii ni kuchezea maneno tu nako hakuwezi kukufaa wewe hata chembe, utaona yatakayokupata Kesho (Kiyama).” Ibilisi akasema: “Na wewe utaona nitakavyofanya kesho.”
Akasema: “Utafanya nini?”
Ibilisi akajibu: “Nitamtaka Mwenyezi Mungu atimize ahadi Yake na nitamtolea hoja kwa kauli Yake:
ﻭَﺭَﺣْﻤَﺘِﻲ ﻭَﺳِﻌَﺖْ ﻛُﻞَّ ﺷَﻲْﺀٍ ۚ {156}
“Na rehema yangu hukienea kila kitu.” (7:156)
“Nami ni ‘kitu,’ kwa hiyo ni wajibu rehema Yake inipate (inienee). Kama mimi si chochote, basi sitahisabiwa wala kuadhibiwa.”
Akasema Musa (a.s.): “Hakika rehema ya Mwenyezi Mungu inamwenea yule mwenye mwelekeo nayo, na wewe uko mbali sana nayo.”
Ibilisi akasema: “Basi nitafanya njia nyingine. Nitawaita wafuasi wangu waliopotea na nitamtaka Mwenyezi Mungu (s.w.t.) naye awaite wafuasi Wake waumini, halafu ipigwe kura. Hapo atajulikana nani mshindi mwenye sauti ya wengi. Kama Mwenyezi Mungu akikataa kura, nitafanya maandamano makubwa mpaka nipate ninayotaka.”
Kigano hiki kina lengo la kwamba watu wa batili ni wengi zaidi kuliko watu wa haki, kwa sababu haki ni nzito na batili ni nyepesi; kama alivyosema Amirul Muminin, Ali (a.s.): “Yapasa mwenye akili kutoangalia wingi kuwa ni kipimo cha haki, wala uchache kuwa ni kipimo cha batili.”
Katika Nahjul-Balagha, amesema: “Hakika kundi kubwa ni watu wa batili hata wakiwa wengi; na kikundi kidogo ni watu wa haki hata wakiwa wachache.”
Qur’an tukufu nayo inasema: “Na wengi wao ni wenye kuchukia haki.”( 23:70)
ﻭَﻟَٰﻜِﻦَّ ﺃَﻛْﺜَﺮَ ﺍﻟﻨَّﺎﺱِ ﻟَﺎ ﻳَﻌْﻠَﻤُﻮﻥَ {21}
“Lakini watu wengi hawajui.” (12:21)
ﻭَﻟَٰﻜِﻦَّ ﺃَﻛْﺜَﺮَ ﺍﻟﻨَّﺎﺱِ ﻟَﺎ ﻳَﺸْﻜُﺮُﻭﻥَ {38}
“Lakini watu wengi hawashukuru.” (12:38)
ﻭَﺃَﻛْﺜَﺮُﻫُﻢْ ﻟَﺎ ﻳَﻌْﻘِﻠُﻮﻥَ {103}
“Na wengi wao hawatumii akili.” (5:103)
ﺑَﻞْ ﺃَﻛْﺜَﺮُﻫُﻢْ ﻟَﺎ ﻳُﺆْﻣِﻨُﻮﻥَ {100}
“Bali wengi wao hawaamini.” (2:100)
Kuna Hadith inayosema: “Wakikutana wasaidizi wa Ibilisi wanaweza kujaza Mashariki na Magharibi.”
Ni kwa madondoo haya, na mengineyo mengi, ndipo Shia wakasema: Khalifa wa Mtume ni kama Mtume; huchaguliwa na Mwenyezi Mungu; siye yule anayechaguliwa na watu.
Huyo anayechaguliwa na watu ni Mfalme wa watu; si Khalifa wa dini. Ama mkuu wa dini, kwa Shia, ni yule mwenye sifa zilizoelezwa. Sio yule anayechaguliwa na watu wala si yule anayewekwa na kiongozi wa kidunia.
Na kwa nini isiwe hivyo? Je, watu wenye matamanio ya dunia wanaweza kuaminika kuongoza dini ya Mwenyezi Mungu? Basi kama ni hivyo na wawachague na kuwapigia kura Mitume, na walifaradhishe hilo kwa Mwenyezi Mungu. Ametakata kabisa Mwenyezi Mungu na yale wayasemayo madhalimu.
Natija ya kimantiki ni kwamba Khalifa wa Mtume hawi, na hatakuwa, isipokuwa kwa usimulizi unaotokana na Mtume mwenyewe, na kwamba mkuu wa dini ni yule mwenye sifa zilizosimuliwa.
Mwenye kujipachika ukuu wa dini bila ya kuwa na sifa zilizotajwa, basi atakuwa amemzulia Mwenyezi Mungu na Mtume Wake, na ameruka patupu mwenye kuzua.
Kwa hivyo basi, yote hayo yanafahamisha kuwa suala lolote haliwezi kuwa la kweli mpaka liwe limefuata haki; na kwamba mbinu za kucheza na maneno, haziwezi kuifanya batili iwe haki, au haki iwe batili, wala kisichoingia akilini kiingie akilini; hata kama hizo mbinu zitakuwa za hali ya juu kiasi gani.
Tutakalolifahamu ni kuwa mwenye mbinu hizo ni mwanafunzi hodari wa Ibilisi katika kuificha haki, na kuifunika na moshi wa hadaa.
Assalaam alaykum
Maneno mengiii yasiyo na kichwa wala miguu. Nani amekwambia anataka kusoma vitabu hapa? Jaribu kufupisha unayo elezea. Biblia inasema penye wingi wa maneno pana uwongo na uovu!
 
Aliitwa shetani na kama msemavyo kuwa mashetani ni malaikà waliyoasi.
Ndio aliitwa shetani, kwani shetani ni malaika!!!???.aliitwa shetani sababu alionekana anamawazo kinyume na mpango wa Mungu.

Sasa mjue shetani kuanzia hapo.
 
Hivi mnao amini Quran mumelogwa au ni kitu gani yaani na usomi wenu mnaweza mkamchambua Mwanasiasa kua ni mwongo papo kwa papo lakini maandishi yaliyopo kwenye Qura yapo tangu hamjazaliwa mnashindwa kuichambua? Yaani nimepitia kwa dakika kadhaa hii Quran nimeona bora nifunike maana inajichanganya yenyewe. Mfano katika elimu ya majini inakuambia chanzo cha Mungu kuumba majini ni baada ya ibilisi kujitapa kua yeye kaumbwa kwa moto halafu binadamu kaumbwa kwa udongo basi Mwenyezi Mungu akaamua kuwaumba Majini kwa moto hapohapo unaambiwa Majini yalikuwepo yakiishi ardhini .unambiwa kabla ya kuumbwa binadamu kuna viumbe vilikuwepo ambavyo vilikua vinafisadi na kuua ,sasa najiuliza hivi viumbe vilikaa muda gani na kwenye ardhi ipi ikiwa hii dunia Mwenyezi Mungu aliiumba kwa siku saba anga, ardhi ,binadamu na vitu vingine vya dunia hii sasa hao majini walikaa chini ya ardhi gani au Mungu alifanya repair ya ardhi? Kwamba aliibadilisha ya zamani akaweka mpya? Pia humo humo kwenye Quran unaambiwa majini yalikua yanapata taarifa ya mbinguni Mara ghafla yakawa yanakosa taarifa za mbinguni eti ikabidi yaende kuangalia ni kipi kinaendelea yakakuta kuna vimondo vya moto hivyo ikabidi yarudi kuwapasha habari wenzao baada ya kufanya research ikabidi yasilimu sasa ndugu zetu waislam je kwa sasa majini yanapata habari za Mbinguni? Kama yanapata tujuzeni nini kinaendelea huko? Hiki sio kitabu kimejaa uongo mtupu
 
Wakiristo muwe waoga na haya mnayoyazusha wazee.Vipi hamna mbawa na mnataka kupaa ? Ipitie tena na tena kauli yako ya mwisho.Hivi unaijua Qur'an mzee au unaiskia ? Je unaujua uislamu wewe au unausikia ? Allha aliyetukuka ana sema katika surat al-Maida "Leo hii nimewakamilishieni dini yenu,na nimetimilza neema zangu kwenu na nimeuridhia uislamu kuwa dini yenu" au kama alivyosema Allah.
Nawewe Soma Quran 2:113 uone ipi ni dini maana mnatuulizaga kila siku ukristo ni dini
Hapa kazi ipo.
 
Tuwaulizeni nyie ndugu mnasema majini yalikua ardhini kabla ya binadamu vitabu vinasema Mungu aliumba dunia hii kwa siku saba ikiwemo ardhi na anga , binadamu na viumbe vingine. Sasa majini yalikaa muda gani ardhini maana Quran inasema majini yaliumbwa baada ya ibilisi kujitapa yeye kaumbwa kwa moto na binadamu kaumbwa kwa udongo ndipo Mungu akayaumba majini kwa moto. Hii Quran kituko hapohapo yaani inavyo onyesha baada ya Adam kuumbwa ndipo majini yakaumbwa Mara majini yalikuwapo ardhini kabla ya kuumbwa Adam hahaaa Mud apigiwe simu ahojiwe
 
Kaka nimeisoma vizuri sana makala,ila nimehitimisha ya kuwa unaelimu ndogo sana juu ya viumbe hao japokuwa umejaribu kunukuu katika baadhi ya vitabu vya waandishi wa kiislamu.Kaka kwanza kabisa umeogea uongo uliopetuka mipaka.Majini hawajawahi kuwa malaika.na huwezi kulithibitisha hilo popote uendapo.Majini ni viumbe walioumbwa kwa moto na malaika ni viumbe walioumbwa kwa nuru.

Malaika hawamuasi Mola mlezi,sasa unavyosema ya kuwa majini ni malaika walio muasi Mola mlezi,inabidi utuambie ya kuwa maneno haya umeyapata wapi ?

Naona maneno majini na mashetani yanakuchanganya sana katika kuyatumia,hii inatokana na wewe kutokuyajua vyema maneno hayo,nakupa faida,tamko shetani ni sifa,kwayo anaweza kuwa nayo binadamu au majini vile vile.Kwahiyo hapa tunahitimisha ya kuwa kuna shetani wa kijini na kuna shetani ya kibinadamu.Sasa unaposema "Majini yanatumiwa na shetani kuwatumiksha watu",unakuwa unamaanisha nini ?

Unaposema hakuna ushirika kati ya majini na ukiristo huu unaoleta ni ushabiki mahali ambapo si pake.Thibitisha kielimu madai yako hayo.

Mimi situmii qurani ili ni pate elimu na tumia Biblia kwa kuwa ndiyo kitabu sahihi na cha kwanza ambacho hata Qurani inataka mkisome. Pili Qurani yenyewe inasema kuna aya zinazo babaisha sasa nitaiyaminije?
soma:-
katika Qur’an 3:7 “Yeye ndiye aliyekuteremshia kitabu (hiki Qur’an) ndani yake zimo aya Muhkam (nyepesi kufahamika) ambazo ndizo msingi (asili) wa kitabu (hiki) na ziko nyingine Mutashabihat (zinababaisha kama habari za akhera,za peponi na motoni na mengine ambayo yamekhusika na Roho).Wale ambao nyoyoni mwao mna upotofu wanafuata zile zinazo babaisha kwa kutaka kuwaharibu watu na kutaka kujua hakika yake vipi; na hakuna ajuaye hakika yake vipi ila Mwenyezi Mungu. Na wale waliozama katika ilimu husema:”Tumeziamini,zote zimetoka kwa Mola wetu.”Na hawakumbuki isipokuwa wenye akili.”
 
kwa akili za kawaida hapo anamaanisha hizo zilizo za kubabaisha ni aya za kutunga hakuna mwenye uhakika nazo.

Halafu bwege mmoja anakuja kusema quran haina shaka.sjui ni bangi au mapepo.
 
Kaka unaweza kuniorodheshea tata na uongo upatikanao katika uislamu ?
Kiutendaji kauli yako ipo tofauti na matendo,umesema upo katika safari ya kuitafuta kweli ili ikuweke huru,wakati huo huo kwamba unaupigia chapuo ukiristo kwa ndio wa kweli,hivi unafikri utaifikia ile safari yako ya kuipata hiyo kweli unayoitafuta mzee ? Kwa ufupi huwezi kuifikia,utaishia kuwa mshabiki mpaka mauti yanakufika.

soma hii hapa :-
katika Qur’an 3:7 “Yeye ndiye aliyekuteremshia kitabu (hiki Qur’an) ndani yake zimo aya Muhkam (nyepesi kufahamika) ambazo ndizo msingi (asili) wa kitabu (hiki) na ziko nyingine Mutashabihat (zinababaisha kama habari za akhera,za peponi na motoni na mengine ambayo yamekhusika na Roho).Wale ambao nyoyoni mwao mna upotofu wanafuata zile zinazo babaisha kwa kutaka kuwaharibu watu na kutaka kujua hakika yake vipi; na hakuna ajuaye hakika yake vipi ila Mwenyezi Mungu. Na wale waliozama katika ilimu husema:”Tumeziamini,zote zimetoka kwa Mola wetu.”Na hawakumbuki isipokuwa wenye akili.”
 
Unaposema Qur'an imesema kulikuwa na mmoja wapo miongoni mwa malaika,kauli hii si sahihi.Na si sawa kusema kusema shetani tu,kusema hivyo haitoshi,pambanua ya kuwa shetani wa kijini au shetani wa kibinadamu.Ibilisi ni shetani wa kijini.

Halafu sina uhakika ya kuwa jini,shetani ni mapepo.Kama unaweza kulithibitisha hilo kielimu itakuwa bora zaidi ili tupate faida.Nithibitishie ya kuwa pepo ni jini mzee.

Pia mimi sio kwamba nakubali tu ya kuwa ibilisi ndio jini,bali mimi naamini kabisa ibilisi ni jini na huo ndio ukweli wenyewe,kwahiyo kushukuru kwako hakuna maana katika hili,kwani nimekutangulia katika hili kwa umbali mrefu sana.
Mkuu wangu hakuna shetani wa kijini

Bali kaa ukijua jini ndo shetan ,satan ,pepo ,lucifer ambaye ni muisilamu mwenzenu anayemwababudu allah na mda mwingine nyie waisilamu kwenda kusali hadi mlazimishwe na lucifer ,satan ambayo ndo majin

Mda mwingine had huwa mnayatolea sadaka kama kuyachinjia mbuz na kuku na huwa mnayatumia kuzulu watu waisilamu ndo wafuga majin wakubwa ambayo hayana nafasi ya kutubu mbele za mungu ndo maana hakuna utofauti kati ya lucifer na allah
 
Muislamu mwenzenu ndiye alidai hivyo na yuko humu humu na siitaji kumjadili zaidi sababu alikuwa na lugha mbaya na alikosa adabu. Hatahivyo, yeye huyo nafikiri ni muislamu koko maana alikuwa more interested na kulemba Kiingereza chake zaidi ya maandiko yenye ushaidi wa kimaandiko. Yeye alidai kwa lugha ya Kiingereza kwamba "In Islam there's truth and untruth." sasa sijui je hiyo untruth ni hipi, maana waislamu wote wana amini uislamu ni dini ya mienyezi Mungu Allah. Na Allah hawezi kuwa na dini ya uwongo au hisiyo kweli.
I hope utaweza jibu hilo swali maana muhusika alishindwa jibu!

nikweli alisoma hapa:-
katika Qur’an 3:7 “Yeye ndiye aliyekuteremshia kitabu (hiki Qur’an) ndani yake zimo aya Muhkam (nyepesi kufahamika) ambazo ndizo msingi (asili) wa kitabu (hiki) na ziko nyingine Mutashabihat (zinababaisha kama habari za akhera,za peponi na motoni na mengine ambayo yamekhusika na Roho).Wale ambao nyoyoni mwao mna upotofu wanafuata zile zinazo babaisha kwa kutaka kuwaharibu watu na kutaka kujua hakika yake vipi; na hakuna ajuaye hakika yake vipi ila Mwenyezi Mungu. Na wale waliozama katika ilimu husema:”Tumeziamini,zote zimetoka kwa Mola wetu.”Na hawakumbuki isipokuwa wenye akili.”
 
soma hii hapa :-
katika Qur’an 3:7 “Yeye ndiye aliyekuteremshia kitabu (hiki Qur’an) ndani yake zimo aya Muhkam (nyepesi kufahamika) ambazo ndizo msingi (asili) wa kitabu (hiki) na ziko nyingine Mutashabihat (zinababaisha kama habari za akhera,za peponi na motoni na mengine ambayo yamekhusika na Roho).Wale ambao nyoyoni mwao mna upotofu wanafuata zile zinazo babaisha kwa kutaka kuwaharibu watu na kutaka kujua hakika yake vipi; na hakuna ajuaye hakika yake vipi ila Mwenyezi Mungu. Na wale waliozama katika ilimu husema:”Tumeziamini,zote zimetoka kwa Mola wetu.”Na hawakumbuki isipokuwa wenye akili.”
Umenukuu aya mzee,hujaleta tata na uongo.Embu leta tata upewe majibu.Pia nakupa faida katika Qur'an pia zipo aya nasih na mansukh,iliyopo na aliyofuta,yaani ipo aya ambayo inasomwa lakini hukumu yake haifanyiwi kazi sababu ilifutwa na aya nyingine kihukumu na mfano wake.
 
Back
Top Bottom