Je, asili ya majini ni ipi?

Kaka nimeisoma vizuri sana makala,ila nimehitimisha ya kuwa unaelimu ndogo sana juu ya viumbe hao japokuwa umejaribu kunukuu katika baadhi ya vitabu vya waandishi wa kiislamu.Kaka kwanza kabisa umeogea uongo uliopetuka mipaka.Majini hawajawahi kuwa malaika.na huwezi kulithibitisha hilo popote uendapo.Majini ni viumbe walioumbwa kwa moto na malaika ni viumbe walioumbwa kwa nuru.

Malaika hawamuasi Mola mlezi,sasa unavyosema ya kuwa majini ni malaika walio muasi Mola mlezi,inabidi utuambie ya kuwa maneno haya umeyapata wapi ?

Naona maneno majini na mashetani yanakuchanganya sana katika kuyatumia,hii inatokana na wewe kutokuyajua vyema maneno hayo,nakupa faida,tamko shetani ni sifa,kwayo anaweza kuwa nayo binadamu au majini vile vile.Kwahiyo hapa tunahitimisha ya kuwa kuna shetani wa kijini na kuna shetani ya kibinadamu.Sasa unaposema "Majini yanatumiwa na shetani kuwatumiksha watu",unakuwa unamaanisha nini ?

Unaposema hakuna ushirika kati ya majini na ukiristo huu unaoleta ni ushabiki mahali ambapo si pake.Thibitisha kielimu madai yako hayo.
 
Kaka naona umeamua kuubeba mzigo ambao huwezi kuubeba kamwe.Qur'an ina elimu yake,tena elimu yake hasa,Qur'an ina misingi yake ya kuitafsiri si kubabadua kama unavyofanya wewe,japokuwa umenukuu aya katika Qur'an na aya iko iwazi kabisa tena haihitaji akili nyingi kuielewa aya hiyo,Qur'an haisemi kama ibilisi alikuwa ni malaika,kama ulivyojitutumua kwa kuhitmisha kwa kusema ya kuwa kisa ibilisi alikuwa pamoja na malaika,kwahiyo ibilisi alikuwa ni malaika,bila shaka umeamua kupotosha ukweli ulio wazi kabisa.

Kisa cha ibilisi,kwa ufupi kipo hivi,Wao walivyokuwa wanaishi ulimwengu ilifikia kipindi wakafanya ufisadi na uharibifu mkubwa.Kipindi hicho ibilisi aliyelaaniwa alikuwa ni mwingi wa kuabudu,mpaka akapewa lakabu ya Aba Sajida (Yaani baba wa kusujudu) huku jina halisi likiwa ni Azaziri,kwa rehma zake Allah aliyejuu,akamchukua kiumbe wake huyo,kutokana wingi wake wa kufanya ibada akamuweka pamoja na kundi la majini wakawa wanaishi.Pindi Allah alipomuumba Adamu,na kutoa amri kwa malaika na ibilisi wampe heshima Adamu.Ibilisi aliyelaaniwa akakaidi amri,huku akisema haiwezekani mimi niliyeumbwa kwa moto nimsujudie kiumbe dhaifu kilichoumbwa kwa udongo.Kisa ni kirefu,kwa ufupi huo tunaona ya kuwa eidha ni kwa uchache wako wa elimu au kwa makusudi umeamua kuisemea uongo Qur'an,eti kwa mujibu wa Qur'an ibilisi ni malaika ? ! Wapi na wapi kasi na kusi ?

Ukiamua kusoma soma kweli kweli mzee.Ila kusoma ni jambo kando na kuelewa ni jambo lingine.
 
Waislamu hawajawahi kupata tabu juu ya malaika hata kwa bahati mbaya.Allah ametufunza kila kitu na hajacha kitu.
 
Majini hawawezi kuzaa na binadamu wala kuona bali wala kumuingilia binadamu.
 
Kaka umeanza vizuri sana kwa kunukuu aya kwazo zinathibitisha ya kuwa ibilisi ni jini,lakini nashangaa mwisho unanukuu aya na kuhitimisha ya kuwa ibilisi ni malaika.Nasikitika sana kwamba jambo dogo sana namna hii unashindwa kuling'amua.Msicho kijua nyinyi wakiristo ni kwamba Qur'an ni kitabu ambacho ndani yake kimetaja habari za watu wa kale na viumbe wa kale,yaani kimesimulia matukioa ya kihistoria,nawashangaa inakuwaje mnashindwa kuunganisha habari na matukio yake,umeshanukuu ya ibilisi ni jini,lakini ibilisi huyo huyo alikwa katika kundi la malaika,hapa hauthitaji hata kuwa bingwa katika lugha,laiti ibilisi angekuwa ni malaika,basi tamko la kundi la malaika lisingekuwepo,kilichofanyika hapo,katika ulimwengu wa lugha tunasema "Tamayyiz" yaani kutofautisha na kuvua.

Usiwe msahaulifu kiasi hicho mzee.
 
Kaka unaweza kuniorodheshea tata na uongo upatikanao katika uislamu ?
Kiutendaji kauli yako ipo tofauti na matendo,umesema upo katika safari ya kuitafuta kweli ili ikuweke huru,wakati huo huo kwamba unaupigia chapuo ukiristo kwa ndio wa kweli,hivi unafikri utaifikia ile safari yako ya kuipata hiyo kweli unayoitafuta mzee ? Kwa ufupi huwezi kuifikia,utaishia kuwa mshabiki mpaka mauti yanakufika.
 
Kuna baadhi ya waislamu wanadai eti ndani ya dini ya kiislamu hupo ukweli na uwongo. Nachojua wewe kama muislamu unaamini uislamu una ukweli mtupu kwa kuwa ni dini ya mwenyewe Mungu Allah. Sasa labda utanisaidia je ni uwongo hupi huo ambao hupo?
Embu jaribu kuwauliza hao waislamu wanao dai ya kuwa ndani ya uislamu kuna uongo na ukweli,wakisha kupa jibu tutakupa jibu la swali ulilouliza.
 
Wakiristo muwe waoga na haya mnayoyazusha wazee.Vipi hamna mbawa na mnataka kupaa ? Ipitie tena na tena kauli yako ya mwisho.Hivi unaijua Qur'an mzee au unaiskia ? Je unaujua uislamu wewe au unausikia ? Allha aliyetukuka ana sema katika surat al-Maida "Leo hii nimewakamilishieni dini yenu,na nimetimilza neema zangu kwenu na nimeuridhia uislamu kuwa dini yenu" au kama alivyosema Allah.
 
Hapa kazi ipo.
 
Embu jaribu kuwauliza hao waislamu wanao dai ya kuwa ndani ya uislamu kuna uongo na ukweli,wakisha kupa jibu tutakupa jibu la swali ulilouliza.
Muislamu mwenzenu ndiye alidai hivyo na yuko humu humu na siitaji kumjadili zaidi sababu alikuwa na lugha mbaya na alikosa adabu. Hatahivyo, yeye huyo nafikiri ni muislamu koko maana alikuwa more interested na kulemba Kiingereza chake zaidi ya maandiko yenye ushaidi wa kimaandiko. Yeye alidai kwa lugha ya Kiingereza kwamba "In Islam there's truth and untruth." sasa sijui je hiyo untruth ni hipi, maana waislamu wote wana amini uislamu ni dini ya mienyezi Mungu Allah. Na Allah hawezi kuwa na dini ya uwongo au hisiyo kweli.
I hope utaweza jibu hilo swali maana muhusika alishindwa jibu!
 
Kwahiyo umekubali kulingana na aya za quran kuwa ibilisi ni jini? Kama umekubali ni vizuri waislamu wenzako kwenye uzi huu wawe na taarifa. Na pia ingekuwa vizuri waislamu wakaelewa kuwa neno Jini, Ibilis, Pepo na Shetani/Satan ni kiumbe huyo huyo. Yeye ana majina mengi tu! Kwahiyo naomba uwaelimisha waislamu wenzako.

Mimi siko interested na watu wa kale, matukio, viumbe wa kale au historia. Mimi nilitaka kuthibitisha Shetani ni nani kulingana na Qur'an. Na kwa bahati nzuri Qur'an hiyohiyo ikatupa jibu ingawa siyo direct answer, lakini jibu lilikuwa la kuridhisha.
Qur'an ilitupa jibu kwamba kulikuwa na mmojawapo miongoni mwa malaika aliyekataa kusujudu, na malaika huyo alikuwa anaitwa iblis.
Wacha Qur'an itupe jibu katika Sura 2:34 ikisema " Na tulipo waambia Malaika: Msujudieni Adam, wakamsujudia wote isipo kuwa Iblis, alikataa na akajivuna na akawa katika makafiri."
Hapo ni wazi kabisa kwamba "Malaika waliambiwa." Siyo malaika na iblis waliambiwa! Kama malaika waliambiwa basi iblis alikuwa miongoni mwa malaika sijui ubishi wako wa kutoelewa unatoka wapi! Hamna obscurity wala confusion yeyote. Wala simuitaji imam, Sheik au scholar anisaidiye kwa hilo.

Na zaidi katika tafsiri ya Qur'an ya kiingereza pale kwenye iblis imeandika Satan. Tusome tena Al-baqara 2:34. "And We said to the angels, "Bow down to Adam." They bowed down, except for Satan. He refused, was arrogant, and was one of the disbelievers."
Mimi kwa hilo andiko niko satisfied kwamba Shetani alikuwa mmoja wa malaika aliyekatwa satan au iblis. Na kwa taarifa yako nina akili zangu timamu na wala siyo Mzee.
 
Uislamu ni mkweli mtupu....
 
Hujajibu swali la msingi kwanini binadamu anayeasi hamwiti shetani/jini?
Embu tumia akili sasa.

Binadamu ni malaika!!!, binaadam akikosa anapewa nafasi ya kutubu kwa gharama yoyote.

Malaika muasi hana nafasi hiyo, na kwa kujua hilo akaahidi kupoteza binaadam.
 
Unaposema Qur'an imesema kulikuwa na mmoja wapo miongoni mwa malaika,kauli hii si sahihi.Na si sawa kusema kusema shetani tu,kusema hivyo haitoshi,pambanua ya kuwa shetani wa kijini au shetani wa kibinadamu.Ibilisi ni shetani wa kijini.

Halafu sina uhakika ya kuwa jini,shetani ni mapepo.Kama unaweza kulithibitisha hilo kielimu itakuwa bora zaidi ili tupate faida.Nithibitishie ya kuwa pepo ni jini mzee.

Pia mimi sio kwamba nakubali tu ya kuwa ibilisi ndio jini,bali mimi naamini kabisa ibilisi ni jini na huo ndio ukweli wenyewe,kwahiyo kushukuru kwako hakuna maana katika hili,kwani nimekutangulia katika hili kwa umbali mrefu sana.
 
Umekosea, umesoma post yangu tu pasi na ya yule niliyemjibu au hukuzifatilia za nyuma. Nimesema " swala la uongo na ukweli ktk uislamu mm silizungumzii " Kaka uhuru nilionao naujua mm, na Kweli ninayoizungumza naijua mm pia, Kweli hii wala haitegemei kabisa hivyo imported Books zenu.

Mi naamini kweli iko wazi hata ndani ya nyoka unaiona, kwa simba, miti mawe nk. Sa ushabiki wangu juu ya Ukristu umeuona wapi hapo? Unajua naishije kiuhalisia? Ila logic ya Ukristu juu ya majini (mapepo waovu) ina mantiki sana kuliko hiyo ya kiislamu kuhusiana na majini, haieleweki. Iko tu kinadharia na kihadithi.

Swali kuu linaloumiza kichwa,ni kwanini uyahudi na ukristu uhubiri (vitangulizi vya uislamu) zihubiri tofauti kuhusiana na hivi viumbe ukilinganisha na uislamu?

Huoni hofu hapo hata kidogo kweli? Haya jumuisha na kauli za mtume alipotoka jabal hira kwa mkewe, bado tu huoni wenye hofu wanafikiri sana?

Ukristu na Uyahudi ungekuwa na hila gani ya kuvichukia viumbe vyema vilivyoumbwa na Mungu wao ili kwa pamoja vimuabudu? Haya maswali huwa hamjiulizi mnamezeshwa tu?

Vuta picha, kama kweli jini ni malaika muhasi, na ndiye aliyempa maelekezo Muhammad kule Jabal hira, unadhani angemwambiaje kuhusu race ya majini? Kweli hapo hamfiki ktk kufikiri?

Uwezi kufikia hapo kwakuwa hauko huru, una vifungo, funguka. Na ili ukamatike vizuri, kufunguka ni dhambi ktk uislamu, hata kuitafutatafuta kweli juu ya Mungu ni dhambi, tena mnaambiwa kuna mambo binadamu msijisumbie nayo, lock.

Haya, matendo si ya waumini mi si mdogo kihivyo, nazungumzia ya kidini. Yale yaliyohalalishwa na dini, yanalingana na mafundisho mengi juu ya wale malaika waovu aka majini. Mfano, mavazi, siku za ibada, manukato, vyakula na vinywaji, lugha kimaandishi, sherehe, nyakati na masaa, mauaji nk.

Najua unajua kuwa uislamu unatambua kuwa siku ya saba ya juma ni jumamosi, je unajua mantiki ya namba saba? Vipi kuhusu sita nayo? Kwanini ya kiislamu yatokee siku ya sita ktk maana ya hiyo namba?

Ashikwae na uislamu huwa mkatili sana, ready to Kill, unahisi wafuasi wa Yesu na wa mtume wapi walibananishwa pabaya sana? Yesu hakuwa tayari kuua, ndo mafundisho aliyokuja nayo, vipi Mungu kaona alikosea akabadili itikadi miaka mia sita baadae? Yapo mafundisho mengi aliyoyaleta nabii Issa ambayo mtume Muhammad amekwenda nayo kinyume, mfano adhabu na hukumu, je hawa ingewezekanaje wautoe ujumbe wao toka kwa Mola mmoja ktk mfululizo mmoja ulionyooka?

Ktk imani zote, hata ubuntu, ubudha nk unaonesha Mungu no Bwana wa UPENDO, hivyo Yesu (wa kibiblia) na mafundisho yake yanamuwakilisha Mungu zaidi.... hili haliwezi kupingwa na yeyote labda na mpinzani wa Mungu, nani huyu?

Kuna la uongo nimelinena hapo? Nisaidie niikaribie KWELI.
 
Nionyeshe wapi Qur'an imesema ibilisi ni Malaika ? Kusoma maandishi hakutoshi kuelewa ndio kitu cha msingi.Umetuthibitishia kabisa katika uislamu ibilisi ni jini na huku unatuambia ibilisi ni malaika.Muwe mnaelewa mambo jamaa.
 
Ingekuwa ni ibilisi ni malaika basi asingepambanuliwa kwa jina.Lakini ametajwa kwa jina ili atu wapambanukiwe ya kuwa ibilisi alikuwa katika kundi la malaika,yaani katika lile kundi la malaika naye ibilisi alikuwemo.Mfano sahali,ukiambiwa katika msafara wa mamba na kenge wamo,hii haimaanishi kenge nao ni mamba,bali umefafanuliwa tu ili upate kumakinika na kupata ujumbe uliokusudiwa.Mfano mwingine ni kuwa,chukulia ya kuwa kuna mbuzi anaitwa mkono,katika malezi mbuzi yule alikuwa pamoja na kondoo kadhaa,siku nilipowaswaga kwenda malishoni kondoo wote walienda kula isipokuwa mkono.Hapa katu huwezi kusema mkono naye ni kondoo kisa alikuwemo katika kundi la kondoo,achilia mbali hapo kabla ulishapewa habari ya kuwa mkono ni mbuzi.Sasa ukija kutuambia tena mbuzi huyo kaja kuwa kondoo,bila shaka wewe una elimu ya ziada juu ya mabadiliko hayo,na unatakiwa utueleze vipi mbuzi kawa kondoo.Ukishindwa kutuonyesha lazima utakuwa na ususuavu wa moyo na ufikiriaji wa kitoto.Wakiristo mjifunze kuweka kila kitu mahala pake.
 
Kuwa na akili timamu sio sababu ya kukufanya wewe uweze kung'amua mambo ya kielimu kama haya,na kuwa na akili timamu kwako ndio kumefanya uangukie pua katika jambo rahisi kama hili.Cha msingi ni kuwa na AKILI SALAMA sio AKILI TIMAMU mzee.Halafu ulivyopata mghafala eti "mimi ni akili timamu siyo mzee" kwa hiyo wazee hawana akili timamu wala akili iliyo salama.
 
Nakuambia kitu Mkuu! Hakuna mkristu anaeamini kwamba Mungu ameshawahi zaa mtoto biologically, bali yeyote amwaminie hufanywa kuwa mwana wa Mungu. Viumbe wote waaminifu kwake ni wana aka waja wa Mungu. Haya fananisha logic hiyo na mafundisho au upingaji ulioko kwenye Quran, ni Mungu huyo mwenye kuweza kupingana na hilo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…