Jasusi nchini - utaratibu wa kuripoti ukoje? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jasusi nchini - utaratibu wa kuripoti ukoje?

Discussion in 'Jamii Intelligence' started by newmzalendo, Jan 2, 2010.

 1. newmzalendo

  newmzalendo JF-Expert Member

  #1
  Jan 2, 2010
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 145
  Happy New Year wana JF,

  Utaratibu ukoje wa kuripoti kuwa kuna jasusi au mtu unayeshuku au una uhakika kuwa ni spy anakusanya taarifa nchini kwa manufaa ya taarifa nchi anayoitumikia?

  Je usalama wa taifa una kitengo cha kudeal with such cases? If yes kinaitwaje?

  Nina taarifa muhimu. Police najua hawana jinsi ya kudeal na swala hili kwani wako bize sana na crime and ufisadi issues :(
   
 2. Jayfour_King

  Jayfour_King JF-Expert Member

  #2
  Jan 2, 2010
  Joined: Nov 15, 2009
  Messages: 1,142
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Ni vyema kama si rahisi kwako kupata access ya moja kwa moja na usalama wa taifa (hii ndiyo kazi yao hasa!) wasiliana moja kwa moja na RPC ambaye atajipima ubavu kwamba kama anaweza atawatuma vijana wake anao waamini, kama sivyo yeye atawasiliana na RSO ambaye anao vijana wajuvi kwa kazi hizi na kwazo wameajiriwa. Na ki mfumo anaweza kuomba hata makomandoo wa kijeshi walio katika kikosi cha jeshi kilicho jirani na sehemu husika kama issue ni dume.

  Si mjuzi sana, lakini naamini nitakuwa nimekujibu nina kaupeo kadogo ka uraia, naamini hiyo ndiyo real process.
   
 3. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #3
  Jan 2, 2010
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Nilipoiona hii nilidhani inanizungumzia mimi. Fuata maelekezo ya Jayfour King.
   
 4. Wacha

  Wacha JF-Expert Member

  #4
  Jan 2, 2010
  Joined: Nov 23, 2006
  Messages: 856
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  Wewe ni Jasusi kweli maana umeshituka.
   
 5. Kibunago

  Kibunago JF-Expert Member

  #5
  Jan 3, 2010
  Joined: Jan 11, 2008
  Messages: 288
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Kila wilaya ina ofisi ya usalama na yeyote mwenye taarifa kama zako anaruhusiwa kwenda na kuzitoa bila uoga. Kama unaona shida kuitafuta hiyo ofisi ya DSO ilipo nenda kituo cha polisi (sio kweli kwamba wako bize kwa hiyo hawawezi kudeal na suala hili); omba kuonana na Mkuu wa Polisi (W) au hata wa Mkoa kama uko Mkoani.

  kama uko nje ya nchi nenda ubalozini kwetu na utoe taarifa yako. Kama hutaki ufahamike pia waweza kuwaandikia niliokushauri kwa kuwaeleza wa ufasaha kupitia email zao.

  Ukishindwa kabisa hutakuwa umefanya kosa kumweleza DC wako au hata mwakilishi wako (Mbunge) wanajua watakavyoli handle maana wanajua miundo ya serikali na vitengo vinavyohusika katika kutafiti na kuzuia majasusi.

  Isipokuwa kama nia yako hapa ni kujua muundo wa UWT, chukua hatua mara moja kuokoa Taifa maana hakika kwa mapana ulinzi na usalama ni jukumu letu sote.

  Chanzo cha ushauri wangu ni somo la uraia.
   
 6. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #6
  Jan 3, 2010
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Mkuu newmzlendo kama ulivyoshauriwa hapo juu onana na Mkuu wa Wilaya yoyote iliyokaribu au Mkuu wa Kituo cha Polisi na utaona Milango ya Dola inavotoa ushirikiano.
   
 7. Mlango wa gunia

  Mlango wa gunia Senior Member

  #7
  Jan 3, 2010
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 123
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Suala la kumripoti jasusi ni vema kama unaweza kuripoti kwa afisa usalama wa wilaya au mkoa,Sina imani kama polisi yetu ina kitengo hicho cha counter intelligence za ya CID na hivyo polisi itawalazimu kuomba msaada kwa RSO au DSO,Usalama wa taifa wao watafuatilia kijasusi na kuthibitisha kuwa huyu mtu ni jasusi au la kwa kutumia counter intelligence technics/methods.Ni vigumu kwa jasusi mzuri kumtambua kirahisi na nirahisi kwa yeye kutambua/kuhisi kuwa anafuatiliwa hasa anapotumika agent ambae hana uzoefu wa kutosha.
  Ikishindikana kuwapata DSO/RSO basi polisi au mkuu wa wilaya pia inafaa.
   
 8. M

  Mbelakisa Member

  #8
  Jan 4, 2010
  Joined: May 22, 2009
  Messages: 17
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndugu kuwa mzalendo kwa Nchi yako kwani ni usalama wetu sote. Taarifa yako ina seheu nyingi ambapo unaweza kuzipeleka, kuanzia ngazi ya kitongoji hadi taifa, na kote huko bado unaongelea usalama wa taifa. kwa hiyo kama una nia njema huwezi kushindwa wapi kwa kupeleka habari hizi.
   
 9. Mponjoli

  Mponjoli JF-Expert Member

  #9
  Jan 4, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 668
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Kazi nzuri,usalama ni wetu sote
   
 10. R

  Renegade JF-Expert Member

  #10
  Jan 4, 2010
  Joined: Mar 18, 2009
  Messages: 3,768
  Likes Received: 1,073
  Trophy Points: 280
  Ni kweli kwamba Police wanadeal na crime zaidi, lakini inategemea wewe uko wapi? na unaweza kuwasiliana na nani? Maana yangu ni wilayani au Mkoani , Kijijini ? Kama uko kijijini unalazimika kufikisha taarifa zako kwa uongozi wa kijiji kutegemeana na usiri na unyeti wa taarifa zako. Vijijini kuna mgambo ambao wanaweza kutumika kwa urahisi , Japo inategemea pia kama unadili na watu au mtu wa aina gani, mfano Kama ni Jasusi mgambo si saizi yake ,lazima ufike ngazi ya juu zaidi.Majasusi ni watu wenye ujuzi sana kutegemea na ngazi na mafunzo aliyo nayo. Wilayani kuna ofisi za DSO ambao wao wanaweza ku-organise Attack Kwa kushirikana na OCD na OC-CID, Hivyo hivyo Mikoani nako kuna RSO ambaye anaweza shirikiana na RPC kuorganize attack kama muhimu.

  Hayo ni Maoni yangu tu kwa uzoefu wangu JKT na uelewa mdogo nilionao.
   
 11. Kwetunikwetu

  Kwetunikwetu JF-Expert Member

  #11
  Jan 4, 2010
  Joined: Dec 23, 2007
  Messages: 1,544
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Ujumbe wako umefika.....naimani hapa JF wamejaa kibao watakuwa washaku-PM
   
 12. Katibukata

  Katibukata Senior Member

  #12
  Jan 4, 2010
  Joined: Dec 27, 2007
  Messages: 183
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Newmzalendo,
  Inategemea na unyeti wa Taarifa uliyonayo. Nadhani kama ungepata mawasiliano (namba za simu) za RPC ingesaidia.
   
 13. P

  PUNJE JF-Expert Member

  #13
  Jan 4, 2010
  Joined: Jul 30, 2008
  Messages: 334
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 45
  .......peleka taarifa kwa kiongozi yeyote au hata polisi aliyekaribu nawe. wao watachukua hatua itayofaa; kwa kutoa taarifa kwa vyombo husika na kadhalika. Sina shaka hata mgambo aliyehitimu mafunzo kamili anafahamu nini la kufanya endapo mtu fulani anashukiwa dhidi ya usalama wa nchi yetu. Wnegi wa Watanzania wamepata elimu ya Ulinzi na Usalama wakiwa JKT na Mgambo. hususan wale wa miaka ileeeee!!
   
 14. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #14
  Jan 4, 2010
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Weweee ndugu ndugu PUNJE,taarifa kama hizo ni handle with care!!
  Hizo ni tuhuma nzito sana kupewa askari wa kawaida au hata mgambo, pengine kama wewe mwenyewe na hao mgambo huwatakii mema.
  Mtu jasusi ni hatari, na ili habari zake zisisambae yuko tayari kuzizima kama mtu azimae moto wa mbuga.
  Ushauri mahiri umetolewa na posts tofauti katika hii thread,katika counter-intelligence speed is the key.
   
 15. k

  kamaghe Member

  #15
  Jan 4, 2010
  Joined: Oct 30, 2009
  Messages: 14
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Je una uhakika kuwa hy ni spy. Evidence unazo? Maana bila evidence mh!
   
 16. K

  Kahinda JF-Expert Member

  #16
  Jan 5, 2010
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 849
  Likes Received: 133
  Trophy Points: 60
  hakika wewe si njuzi rpc hahusiki na maswala ya ujasusi yeye
  huhusika na usalama wa raia pamoja na upelelezi(cid).
  Hivyo taarifa za kiusalama hasa za kijasusi kama upo mkoani mtafute rso(mkuu wa usalama wa taifa mkoa) au mkabithi mkuu wa mkoa wako atajua mahali pa kufikisha taarifa yako.
  Kama uko dar-es-salaam mpelekee rso au mkuu wa mkoa wa dar.
  Au peleka taarifa yako pale ikulu kwenye gate kuu pale watajua mahali pa kuipeleka, angalia usijifanye shushushu hiyo kazi nasikia ina hatari zake kwani fikiria huyo unayemlipua akijua umefanya hivyo nini kitakupata ndo maana usimpe taarifa za jinsi huyo mtu yeyoye bila kuwa na uhakika naye.
  Hata mimi si mjuzi sana ila tulifundishwa enzi za mgambo somo la ulinzi na usalama.
   
 17. Modereta

  Modereta Senior Member

  #17
  Jan 5, 2010
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 163
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Kwa kufuata mfumo uliopo, vyombo vyote vya dola vinatakiwa viwe na uwezo na ufahamu wa kushughulikia mambo haya. Lakini hali halisi ya vyombo vyetu inasikitisha wakati mwingine.
  - Polisi wengi ngazi za chini wakipata taarifa hiyo wataanza kufikiria watapataje rushwa kwake na waendelee kumdai kila wakiishiwa. Yanaonyeshwa kila mara, kwani majambazi wengi wana mtandao wao na BAADHI ya polisi wetu. Sasa hii inaweza msitua Jasusi akaingia gizani au hata akahamishwa.
  - Ukitumia kitengo kisicho na utaalamu wa kutosha vilevile, inaweza mrusha ndege wetu tusimwone tena.

  Ushauri
  Nikianza na angalizo, jasusi hasa hatakwenda kufanya kazi yake kijijini, hivyo uwezekano wa kuwa huko ni mdogo. Kama hii ni kweli basi atakuwa mahali ambapo kuna vyombo vya ngazi nzuri tu ya kutoa taarifa (kama Mkuu Kibunago alivyoshauri)

  Ushauri
  - Mahali mwafaka ni ofisi za DSO (District Security Officer) zipo ofisi zote za wilaya, RSO, ofisi zote za mikoa. Usikatishwe tamaa na maswali utakayoulizwa na vipingamizi utakavyo wekewa kwani ndio usalama wenyewe huo, sema na tenda kwa uhakika watalifanyia kazi.
  - Vituo vikubwa vya Polisi, mahali kwenye OCD/RPC waliotulia (wako ambao nao wapo kutuliza fujo kwa nguzi/misuli, watamrusha ndege wetu) wape taarifa za uhakika, kwa ufasaha ili wajue waanzie wapi na vipi.
  - Ni vyema kutoa taarifa kwa mtu mmoja tu, akiwa pekee na taarifa ziwe kamili, kama vile umemwona wapi, kama anaishi au huonekana hapo, alama zipi ulihisi zinaashiria ujasusi, tahadhari gani ulichukua n.k. Yote ni kufanya mtu unayempa taarifa awe na nondo za kutosha kukuamini, la sivyo itakuwa mambo ya mnigeria wa marekani juzi.
  - Wewe mwenyewe endelea kumfuatilia kwa uangalifu, maana (kama alivyosema Mlango wa Gunia na Renegade) jasusi mzuri na mkubwa atakutambua haraka na ni hatari, waweza hata poteza maisha yako.

  Mwisho, Hiongera kwa kuwa Mtanzania mzalendo halisi na tunaomba wananchi wote tuwe hivyo, maana usalama wetu uko mikononi mwetu, na vyombo vyetu vinahitaji msaada wetu, kwani sisi ndio tunaishi na wote hao.
   
 18. M

  Mwanitu JF-Expert Member

  #18
  Apr 21, 2010
  Joined: Feb 19, 2010
  Messages: 634
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 80
  Hakika hii inaonyesha ombwe lililopo kwenye eneo ya elimu ya ushirikishwaji wa jamii katika ulinzi wa taifa.ie elimu ya jamii.
   
 19. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #19
  Apr 21, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  sorry wakuu... off point kidogo!!! kwetunikwetu na renegade avatar zenu zinafanana, ni bahati nzuri au intentional, hapo copyright laws inasemaje
   
 20. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #20
  Apr 22, 2010
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  THE TANZANIA INTELLIGENCE AND SECURITY SERVICE ACT, 1996

  Sn.14.-(1) It shall be the duty of the Service to collect, by investigation or otherwise, to the extent that it is strictly necessary, and analyse and retain information and intelligence respecting activities that may on reasonable grounds be suspected of constituting a threat to the security of the United Republic or any part of it.

  Sn. 15.-(1) The Service shall, subject to this Act, have power to investigate any person or body of persons whom or which it has reasonable cause to consider a risk or a source of risk of a threat to the state security.

  "security'' means the protection of the United Republic from acts ofespionage, sabotage and subversion, whether or not it is directed from or intended to be committed within the United Republic;

  ''threats to the security of the United Republic'' means-
  (a) espionage, sabotage or other activities which are against Tanzania
  or are detrimental to the integrity, sovereignty or other interests
  of Tanzania or activities directed toward or in support of such
  espionage or sabotage.
  (b) foreign influenced activities within or relating to Tanzania that
  are detrimental to the interests of Tanzania, are clandestine or
  deceptive or involve a threat to any person.
  (c) activities within or relating to Tanzania directed toward or in
  support of the threat or use of acts of serious violence- against
  persons or property for the purpose of achieving a political objective
  within Tanzania or a foreign state; and
  (d) activities directed toward undermining by covert unlawful acts,
  or directed toward or intended ultimately to lead to the destruction
  or overthrow by violence of, the constitutionally established
  system of government in Tanzania, but does not include lawful
  advocacy, protest or dissent, unless caried on in conjunction with

  any of the activities referred to in paragraphs (a) to (d).


  Fo the purposes of the National Security, you can report to any Government Machinery, be it Police, Mtendaji Kata, DC, RC, MP etc depending on where you are residing. Otherwise, if the matter is very serious, and you think that there is a possibilty of those guys at lower level will fail to take it as you perceive, you have can call any Senior Police official around there, and all procedures will be well explained to you in case. Just i case,you can contacts get through Police Website http://www.policeforce.go.tz/

  Othewise, infomred that, depending on the nature of suspicious information to be analysed, TISS is not involved in prosecution the matter than investigation and to some areas may let it at the hands of Police.
  There are alot of Laws regulating crimes of such nature of your suspicion in Tz, these include but not limited to:
  1. The Natonal Security Act 1970
  2. Prevention of Terrorism Act, No. 21 of 2002
  3. National Defence Act​

  4. Criminal Procedure Act

  5. Penal Code
  6. Refugee Act of 1998
  7. Immigration Act, No. 7 of 1995 etc.
  But for the case of who has to prosecute what matters and application of which law to what facts, normally depend upon the authority to define the nature of crime when the matter is reported to them.

   
Loading...