Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 50,530
- 113,665
Uhaini ulipangwa 1982, home kwetu ni Drive-in Estate, nyumba yetu na nyumba ya Banyikwa ziliuwa zimeungana tukitenganishwa na ukuta. Hapo ndipo ilipokuwa ikifanyika mikutano ya kupanga mambo!. PW No. 1 ni Hope Banyikwa, ambaye ndie binti mkubwa wa familia ya Banyikwa, hawa walikuwa ni Wahangaza, hao mabinti!, usipime!.Pasco tafadhali tudadavulie kidogo hapa.
Kesi ilivyoanza, ilikuwa na washtakiwa 46. Wote walishikiliwa Ukonga Maximum Prison, Kiongozi mkuu wa mpango huo ni komandoo wa JWTZ aliyeasi, Martin Tamimu aliyeelezewa kuwa ni mtu hatari sana na hashikiki kirahisi, hivyo wakati wa arrest vijana walipewa special instructions, hivyo askari 8 na magari 4 yalimzingira nyumba aliyokuwepo kwa kimada wake Kinondoni Mkwajuni, walipojiririsha yuko ndani ya "game", waliivamia nyumba!, alichomoka bila shati na kuchumpa darini!, jamaa kuingia ndani hayupo!. Huyo demu akawaelekeza askari kwa ishara, wakaizunguka nyumba, ile wanaanza tuu kumpandia, alitobokea kwenye siling board ya bafu la nje na kuruka ukuta hadi upande wa pili, kumbe nako kuna gari la "jamaa", wakamkimbiza, akarukia pick up iliyokuwa inakwenda race,"jamaa" wakaifuata ile pick -up ay very close range, wakamiminia za kutosha na kumaliza kazi!.
Baada ya sterling kuuwawa, Thomas Lugangira "Father Tom" au "Uncle Tom" ndiye alikuwa mshatakiwa wa kwanza Hatibu Macghee wa pili na wenzao 19.
Nitaendelea.
Pasco.