Japo ' Wanachukiwa ' na wengi ila hadi hivi leo bado sijaona Baba wa ' Promo ' Tanzania nzima kama Clouds Media Group

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Messages
36,469
Points
2,000

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined Jul 13, 2013
36,469 2,000
Hawa Jamaa kila ' Promo ' yako lazima itakuwa na Kishindo Kikubwa. Hongera sana Kwao Clouds Media Group kwani inaonyesha kuwa wana Vichwa hatari katika Masuala mazima ya ' Promo ' na sishangai Kuona kila Tamasha ambalo huwa wanaliandaa Wao basi ni lazima tu ' Nyomi ' lake litakuwa Kubwa na Ukumbi huwa hautoshi.

Nina uhakika wa 100% kwa Uimara walionao Clouds Media Group hasa katika Kufanya ' Promo ' hata lile Tamasha la Wasafi ambalo lilikuwa chini ya Msanii Diamond ( Chibu Dangote ) kama angeacha na ' Uswahili ' wake na angewapa Clouds Media Group wampigie ' Promo ' basi angepata Watu wengi pale Viwanja vya Posta Kijitonyama kuliko wale ' Kiduchu ' aliowaokota na kuwabahatisha.

Ushauri wangu mkubwa kwa Uongozi mzima wa Clouds Media Group kama itaona inafaa hebu fikirieni uwezekano wa Kuanzisha Chuo ' Maalum ' tu cha Kufundisha mambo ya ' Promo, PR, Marketing and Entertainment ' nchini Tanzania kwani nina uhakika kuwa mtawapata Watu wengi na mtaambukiza huo Uwezo wenu mkubwa kwa Kizazi cha Kitanzania.

Kuna muda hata Mimi huwa ' mnanikera ' kweli kweli ila sitaki nisiwape Pongezi zenu au niwe Mchoyo wa Kuwasifieni hasa pale ambapo naona kabisa kuwa mnafanya vyema na mpo vizuri sana. Ni kweli naweza nisikute Bachelor Degrees, Masters Degree na hata Doctorates nyingi hapo Clouds Media Group ila nikakutana na Watu wenye ' Vipaji / Talanta ' ambavyo vina Thamani na Umuhimu mkubwa kuliko hata Wanataaluma ( Academicians ) tunaojitapa ' Kipopoma ' zaidi.

Nawakubali mno na sana Clouds Media Group na kwa ' Promo ' hii nina uhakika hiyo Tarehe 8 December 2019 Uhuru patafurika!
 

naumbu

JF-Expert Member
Joined
Oct 28, 2010
Messages
4,630
Points
2,000

naumbu

JF-Expert Member
Joined Oct 28, 2010
4,630 2,000
Watu zaidi ya elfu 18 unawaita kiduchu ni zaid ya capacity ya Shamba la Bibi inakoenda kufanyika Fiesta
 

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Messages
36,469
Points
2,000

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined Jul 13, 2013
36,469 2,000
Watu zaidi ya elfu 18 unawaita kiduchu ni zaid ya capacity ya Shamba la Bibi inakoenda kufanyika Fiesta
Shamba la Bibi inaingiza Watu 18000? Acha Kunilazimisha nianze ' Kukudharau ' japo nilishakuwa na hilo wazo la ' Kukudharau ' Kitambo tu. Ninachojua kwa mujibu wa Takwimu za Mzee Matoke Shamba la Bibi ( Uwanja wa Uhuru ) unaingiza Watu takribani 39000 hadi 40000 hivyo kama Fiesta ikifanyika hapo Clouds Media Group watakuwa ' wameula ' na watapata Faida Kubwa mno kuliko hata lile Tamasha la Wasafi. Kataa uwezavyo ila kwa Tanzania nzima Baba na Mama wa ' Promo ' ni Clouds Media Group. Nimemaliza.
 

Root

JF-Expert Member
Joined
Jan 23, 2012
Messages
35,011
Points
2,000

Root

JF-Expert Member
Joined Jan 23, 2012
35,011 2,000
Ndio maana Watanzania mnaitwa matahira. Unadhani Uwanja wa Posta kwa akili ndogo unaweza ingiza 18000 pp waliokaa na kusimama?
Weka ushabiki pembeni tumia akili@naumbu,
 

Forum statistics

Threads 1,382,573
Members 526,405
Posts 33,831,728
Top