jmushi1
Platinum Member
- Nov 2, 2007
- 24,989
- 22,521
Wakuu, sina hata haja ya kuelezea sana! Wote tunafahamu maisha ya viongozi wakuu wa nchi akiongozwa na rais wa nchi!
Sijatumia neno “wanyonge”, kwasababu huo unyonge ndo umetumika kuwafanya wananchi wazidi kuwa masikini wa kutupwa!
Nimetumia neno masikini, kwasababu wako wengi pamoja na utajiri wa rasilimali tulio nao. Na hata rasilimali watu ni utajiri mkubwa sana kwa mataifa yenye kujielewa!
Lakini kwetu, sidhani kama tunafahamu mishahara ya viongozi, lakini nafahamu wanatutegemea wananchi kwa kila kitu! Kuanzia kuvaa, kula, kunywa, kulala, kusafiri, nyumba, magari ya kifahari, vinywaji! Na bado wanajijengea makasri pamoja na mapesa mengi kwenye akaunti za nchini na nje ya nchi!
Huyu kiongozi wa sasa, anasema yeye anapenda wanyonge na kuwatetea. Hivi kweli bado anakula pale ikulu na chakula inateremka kabisa?🤦🏾♂️Wakati kila siku kuna watu wanakufa kwa “malnutrition’s”, pamoja na magonjwa yenye kuzuilika.
Kuna member aliweka post hapa, ambapo waziri mkuu anasalimia masikini wa Tanzania, ambao ni wengi sana, lakini ukimtizama, utadhani ni kiongozi aliyetokea kwenye mataifa tajiri kabisa duniani. Ndiyo sisi ni matajiri kwa rasilimali, lakini viongozi ndo wamezuia utajiri huo usionekane kwa wananchi.
Nina amini tutapata insight nzuri zaidi hapa kwa wenye kufahamu zaidi. Lakini ni wazi kuwa hili wimbi la watia nia, wananchi wameona ndo njia pekee ya kujiingizia kipato cha uhakika kabisa bila hata jasho.
Ni wakati wetu sisi wananchi kubadili huu mfumo, ili kuhakikisha tunapata watumishi wa kweli. Isiwe faida ama utajiri tu kujiingiza kwenye siasa na uongozi, bali iwe utumishi wa kujitolea.