Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 50,468
- 113,583
Wanabodi,
Kwa maslahi ya taifa, leo naomba kuendesha somo kuhusu kitu kinachoitwa ubatili na haramu.
Ubatili ni kitu ama kilichofanyika kinyume cha sheria, taratibu na kanuni hivyo jambo likifanyika kwa ubatili jambo hilo linakuwa ni batili.
Haramu ni jambo ambalo limefanyika kinyume cha imani na sio lazima iwe ni kinyume cha sheria.
Huu ubatili na uharamu unafanyika katika nyanja nyingi za maisha yetu, kisiasa, kiuchumi na kijamii.
Sasa ili batili iwe ni batili kweli, lazima batili hiyo ibatilishwe, batili isipobatilishwa inakuwa ni halali!. Vivyo hivyo kwa haramu, ili jambo fulani kuwa ni haramu, lazima haramu hiyo iharimishwe, haramu isipoharimishwa inakuwa ni halali.
Mada kuu ya bandiko hili ni maswali kuhusu uchaguzi mkuu uliopita wa 2020, kuna watu mpaka leo zaidi ya miaka miwili imepita, bado hawataki kukunali matokeo, bado wanaamini uchaguzi ule haukua huru na wa haki hivyo kwao matokeo ya uchaguzi huo sio halali na wengine hata kuuita ulikuwa sio uchaguzi bali ni uchafuzi na matokeo yake ni haramu, hivyo kuendelea kususa hadi leo, hawayatambui matokeo, hawamtambui rais, hawalitambui Bunge hadi kususia nafasi za viti maalum!, hivyo nina viswali kidogo kwako, kuwa japo uchaguzi wa 2020 ni Uchaguzi halali, kwa kanuni ya "the end justifys the means", aliyetangazwa mshindi ndie mshindi halali, jee ushindi wa kishindo wa CCM wa kukomba kila kitu ni ushindi halali au batili na haramu?. Wapinzani ni wameshindwa kihalali kwa kukataliwa na wananchi au ni wameshindwa kwa kudhulumiwa na kufanyiwa Figisu hivyo kushindwa kwao sio halali ni wameshindishwa kwa ubatili na haramu?.
Naomba kukiri nimekuwa inspired kupandisha bandiko hili baada ya kusoma hoja hii ya mwana jf huyu
Ili jambo lolote haramu liwe ni haramu kweli ni lazima liharimishwe, ukifanya jambo la haramu, lisipo harimishwa linakuwa ni halali, yaani kitendo cha kutoiharimisha haramu yoyote, kunakuwa ni kuihalalisha hiyo haramu inakuwa halali mpaka pale yule YEYE anapoingilia kati kwa karma ama kuibatilisha haramu hiyo ama kuiacha na hivyo kuibariki.
Kwa vile issues zs uhalali na uharamu ni issues ngumu kueleweka kirahisi, naomba nifungie darasa kabisa niwapige shule kwa kutoa mifano ila pia kwa vile humu tuna simple readers na deep readers, simple readers hawataki vitu virefu, wanataka vitu short, simple and clear, hawa wanaweza kuishia hapa na ku jump kwenye conclusion, wale ma deep readers, tuendelee.
Vivyo hivyo kwa haramu ya demokrasia na ubakwaji wa demokrasia, ili haramu iwe ni haramu kweli lazima haramu hiyo iharimishwe, haramu isipoharimishwa, na batili isipo batilishwa inageuka halal!.
Swali la kujiuliza kuhusu uchaguzi wa 2020 jee kuna mgombea yoyote aliyelalamika rasmi popote kuhusu uchaguzi huo?. Jibu ni hakuna!. Hivyo kwasababu hakuna mtu yoyote aliyelalamika popote, then kumehalalisha kila kilichofanyika kwa kuitumia ile kanuni ya "the end justifies the means" kwa hoja hizo, na kwa muktadha huo, Uchaguzi wa 2020 ni uchaguzi halali, na sio uchafuzi kama unavyodaiwa na baadhi ya walioshindwa!, CCM imeshinda ushindi wa kishindo kihalali, na wapinzani wamekataliwa na wananchi na kushindwa kihalali!, the winner takes it all!, the looser standing small.
Paskali

Mkuu WALOLA VUNZYA kwanza naomba kukiri post yako hii imenimotivate kupandisha bandiko linalojitemea, thanks for motivation.Pascal ana shida sana kuhalalisha haramu kuwa halali.
Ili jambo lolote haramu liwe ni haramu kweli ni lazima liharimishwe, ukifanya jambo la haramu, lisipo harimishwa linakuwa ni halali, yaani kitendo cha kutoiharimisha haramu yoyote, kunakuwa ni kuihalalisha hiyo haramu inakuwa halali mpaka pale yule YEYE anapoingilia kati kwa karma ama kuibatilisha haramu hiyo ama kuiacha na hivyo kuibariki.
Kwa vile issues zs uhalali na uharamu ni issues ngumu kueleweka kirahisi, naomba nifungie darasa kabisa niwapige shule kwa kutoa mifano ila pia kwa vile humu tuna simple readers na deep readers, simple readers hawataki vitu virefu, wanataka vitu short, simple and clear, hawa wanaweza kuishia hapa na ku jump kwenye conclusion, wale ma deep readers, tuendelee.
ConclusionMfano wa Nyama Halal na Haramu
Ndugu zetu Waislamu wanapaswa kula nyama halal ambayo mnyama amechinjwa kwa Kiislam kwa kutazamishwa kibla, ukila nyama ambayo haikuchinjwa Kiislamu ni haramu. Nchi nyingi za Afrika Tanzania tukiwemo hili tunaliheshimu, hivyo wachinjaji katika machinjio zote ni Waislamu na nyama zote za public inchini Tanzania ni halal. Mtu ukiwa na sherehe yako, ukajochinjia utakavyo, Waislamu wakala, wanakuwa wamekula haramu!, lakini kwasababu hakuna mtu yoyote aliyeuliza kama hiyo nyama ni halal, hao Waislamu wote waliokula haramu hiyo, bila kujua ni haramu, wanakuwa wamekula halal!.
Muislamu Kula Kitimoto Bila Kujua, Sio Haramu!
Nyama ya mkuu wa meza, kitimoto ni haramu tena sio kwa Waislamu tuu, hata kwa Wakristo, kitimoto ni haramu na kwenye Biblia imeharimishwa!. Ukifanya sherehe ukaweka kitimoto bila kusema ni kitimoto, Waislamu wakala bila kujua wamekula kitimoto, then wanakuwa wamekula haramu, ila kwa vile hawakujua ile ni haramu, wanajihesabu wamekula halali!, kitendo cha kutokujua kuwa nyama hiyo ni haranu, kunaihalalisha haramu ile kuwa halali!.
Kubakwa na Kunyamaza ni Kuridhia Ubakwaji!.
Kubaka ni kosa kubwa la jinai na adhabu yake ni kifungo cha miaka 30 jela. Mwanamke akibakwa, asiposema kuwa amebakwa, kile kitendo cha kunyamazia kubakwa ni kuuhalalisha ubakaji ule na kuufanya kuonekana ni consensus hivyo ni tendo halali.
Mfano wa Ndoa Halalu, Ndoa Batili na Ndoa Batilifu.
Ndoa ni mahusiano ya mume na mke. Uhalali wa ndoa sio ile shahada ya ndoa au cheti cha ndoa, ni lile tendo la ndoa, liitwalo consumation, ambapo uhalali huo hupatikana by perfomance ya lile tendo!.
Wanandoa baada ya kufunga ndoa ya kidini Kanisani, au Msikitini, ndoa ya kiserikali kwa DC au ndoa ya kimila kwa Mwenyekiti wa Kijiji, na kukabidhiwa cheti chenu cha ndoa au shahada ya ndoa, uhalali wa ndoa hiyo hupatikana kwa consumation.
Ukitokea wanandoa hao wameshindwa kufanya lile tendo kwa sababu yoyote, then, ndoa hiyo inakuwa ni ndoa batilifu, na itakiwa ndoa halali baada ya perfomance kufanyika.
Ikitokea tendo limeshindikana kabisa kufanyika, then ndoa hiyo inakuwa ni ndia batili ila vile vyeti vya ndoa ni vyeti halali na ndoa hiyo itahesabika ni ndoa halili hadi mwandoa mmoja atakapo toa siri kuwa hakuna performance, na kuiomba mahakama kuibatilisha. Hivyo ndoa batili isipobatilishwa itaendelea kuwa ni ndoa halali!.
Mfano wa Mkataba na makubaliano Halali, Batili na Batilifu.
Mikataba na makubaliano, yaani contracts na agreements iko kama ndoa, kuna mikataba halali, batili na batilifu, void contracts na voidable
Kwanza sio kila makubaliano ni mkataba, ila kila mkataba ni makubaliano!. Yaani not every agreement is contract, but every contract is agreement.
Tofauti ya contact na agreement, contract no kisheria zaidi na agreements ni makubaliano tuu ambayo sio lazima yawe ya kisheria.
Mfano mzuri ni makubaliano ya muungano, artcles of union, zina kipengele cha muungano kuridhiwa pande zote. Tulipoungana ile April 26 1964 muungano ule ulipaswa uridhiwe na ma Bunge ya pande zote, kwa a process inayoitwa ratification. Kwenye muungano wetu ni Bunge tuu la Tanganyika ndilo liliridhia na kutunga sheria ya muungano, lakini kwa Zanzibar ratification haikufanyika, bali Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi aliwaita mabalozi na kuwaeleza Zanzibar imeridhia!. Hivyo makubaliano ya muungano yalikuwa ni voidable, na yalihalalishwa by perfomance ya utekelezaji wa vifungu vya mkataba. Kwasababu hakuna yeyote aliyelalamika rasmi popote, Muungano wetu ni halali licha ya Zanzibar kutoridhia kwa ratification.
Mfano wa Kufuta Uchaguzi Zanzibar ile 2015 ni Haramu ila Uchaguzi wa Marudio ni Halali
Kitendo cha Mwenyekiti wa ZEC kufuta matokeo ya uchaguzi wa Zanzibar ile 2015, kitendo kile ni haramu na kufuta kule no batili kwasababu Jecha hakuwa na mamkaka ya yeye kujigeuza ZEC!. Ili haramu iwe ni harami, haramu hiyo lazima iharimishwe na batili hiyo ni lazima ibatilishwe!. Kwa vile hakuna yeyote aliyepinga rasmi haramu ile na kuibadilisha batili ile, then iligeuka halali hivyo uchaguzi wa marudio ilikuwa halali!. Haramu isipiharimishwa, na Batili isipo batilishwa, hugeuka halali Zanzibar Issue: Kwanini watu wanapiga kelele tu bila kuchukua hatua zozote na Kuna haja ya kuhofia kurudiwa Uchaguzi Zanzibar?
.