Japo mie UKAWA, CCM nimewakubali

Japo mie UKAWA, CCM nimewakubali

Ta Muganyizi

R I P
Joined
Oct 19, 2010
Posts
5,355
Reaction score
2,737
Nakubali mie UKAWA, lakini ni lazima tukubali kitendo cha nchi hii kukabidhiana madaraka kwa njia ya amani namna hii ni suala la kujivunia.

Hata kama wanaokabidhiana ni wezi wanakabidhiana kuendelea kutuibia kwa njia ya amani. Ujinga unabaki kwetu sisi wananchi. namkumbuka mbunge wangu wa Shinyanga wa zamani Leonard Derefa(RIP) akiwa madarakani, alisema achaguliwe ili nayeye AHONDOMOLE

Kuhondomola ni kuendelea kula uhondo. Ukiangalia nchi jirani za Uganda, Rwanda, Burundi na Kenya hata kule Congo DRC hawajaweza kukabidhiana namna hii. Hongera CCM kwa hilo. Si vyema kukalili visasi na chuki na hasira. Nasema hivi japo mnakabidhiana vijiti kwa amani na kuendelea kutuibia, mnajua kula na kipofu.

Hongereni kwa kuendelea kutu "KWATUA" kama JK alivyosema wajinga ni sisi ila manatukwatua kisha mnatupa ICE.

Hongereni. Hii nimeandika mwenyewe wala siajaibiwa Password.!!!!!

Ta Muganyizi.
 
Mambo mengine sio mbaya kukubali. Hamna jinsi

Ubabe ukiendelea sidhani kama ni afya kwa chama.Anyway kila nyani na mbuyuwe.Mbuyu huo nimefurqbia walivyomalizia,maana huku wakidhani wametoka wazima kumbe njiani wamekumbana na ebola.

Hongereni wanaccm kwa kumaliza salama mkiwa vipande sita.
 
Mkuu ungewapongeza tu CCM na kuwadharau wananchi lakini katika hili la kuiingiza UKAWA sidhani kama ni sahihi maana inaonekana kama kampeni kwa CCM waendelee kutuibia kwa wewe kuendelea kuwapumbaza wananchi kwa gear ya wewe kuwa ni UKAWA.
 
Kiongozi ungesoma vizuri ungenielewa nimetumia neno hili "Ujinga unabaki kwetu sisi wananchi"

Muda mwingine tusijidanganye
 
Mkuu Wangu nimekusoma vizuri sana nilichotofautiana na wewe ni kutubakiza wananchi na matope katika macho yetu.Adui yako hautakiwi kumkatia tamaa ni kupambana nae mpaka tone la mwisho sasa unapokubali kirahisi wewe kama wewe ni nani wa kumtoa mwananchi tongotongo katika macho yake na na kkt akili zake ?.

Wape wananchi matumaini ya kushinda walau wakeshe wakilinda kura(haki zao)pengine hiyo itabadili hali ya mambo .Kumbuka haki haiji kirahisi rahisi ni lazima uvuje jasho ,tujitahidi kujifunza kushinda sio kukata tamaa kwa maana ya kushindwa.
 
Yaani unaandika na kujijibu mwenyewe. Habari yenyewe nyepesi kama hewa ya Hydrogen.

Lini wewe ulikuwa UKAWA? Na matusi yote uliyokuwa unatoa?
 
Tukitoa ushauri wa kupambana hatupati suport. Nilipo hapa BKB mjini nilishaandika kuwa kuna mgogoro CDM waje wautatue lakini wameuchuna..................matumaini tunatoa lakini tukiulizwa mbona hapa hamrekebishi hamna jibu.
 
Yaani unaandika na kujijibu mwenyewe. Habari yenyewe nyepesi kama hewa ya Hydrogen.

Lini wewe ulikuwa UKAWA? Na matusi yote uliyokuwa unatoa?

Hadi leo hii mie UKAWA, we nisome vizuri, yaani ni kwamba mwizi aliyekuvamia na kukuibia nyumbani mwako hajatumia Silaha ,,,,kabeba kilaini...ila bado siku inayofuata unaacha mlango wazi. Ila aliyekwibia ni mwizi simtetei ila kaiba bila kukuua. Sasa ufanyeje ili asikuibie tena ndo ujinga huo wa kuacha mlango wazi na kuwapigia kura ccm......nimetumia fasihi usiponielewa basi.
 
Mambo mengine sio mbaya kukubali. Hamna jinsi
Ta Muganyizi, labda sikuelewi hivyo naomba nikuulize, unaposema kukabidhiana una maana gani? Nani anamkabidhi nani? Ninavyojua CCM haijawahi kukabidhi madaraka na sana sana wameendela kuyang'ang'ania, je si hivi karibuni tu wametamka wazi kabisa kuwa hawako tayari kuyaachia madaraka hata kwa miaka mia.

Yawezekana mimi ni mzito kuelewa lakini ukweli ni kwamba nguvu nyingi sana zimetumika na zinaendelea kutumika kulinda huo uroho wa madaraka. Nadhani tatizo letu Watanzania ni kuwa tu wepesi kukubali kudanganyika, kuhadaika na kusahau mateso tunayopitia katika harakati zetu za kupinga ufisadi kwa kuudai mabadiliko.

Nasikitika nawe ni katika wale waliokata tamaa na kuweka silaha chini ukidhani iko siku utaonewa huruma...CCM ingekuwa na huruma Tanzania ingepaa. Hebu jiulize hizo sifa anazotafutiwa Magufuli je zinazidi alizopewa Kikwete mwaka 2005 alipotuahidi kuwa hangekuwa na ubia katika utawala wake, so sad, so pitiful.
 
Ndugu yangu kwanza nikushukuru kwa kunielewa. Ukisoma vizuri utaona nilivyosema wajinga ni sisi. Hata Wachawi hurithishana uchawi, kundi la wezi pia hukabidhiana mikoba pale mmoja wao anapojeruhiwa na risasi au kuchoka. Nimetumia sataha kidogo. Yaani wezi wetu wanakabidhiana mikoba pasipo kugombana, wanakula na kipofu. Soma uzi wangu bila pre conceived prejudice.

Juzi na jana nimeshinda na hasira weeeee kama Pasco japo yeye hakuwa UKAWA ila nimerudi normal. Wezi wanakabidhiana kijiti kwa AMANI.
 
wewe ni mwanachama mtiifu wa ccm ulieamia ukawa na watu sample kama yako ndo tunao wengi sana leo magufuli utaona hata wanachama wa ukawa anapongeza Toka lini mwanachama wa ccm akamkubali mtu wa upinzani?

tumezidiwa na wana ccm yani kuna wengine mpaka wazazi wao wameonekana hawana akili kwa kusema ccm ndo baba na mama yao wanachama wa ccm wanamapenzi makubwa na chama Chao kwani unadhani awajuhi ccm ni chama cha mafisadi? wanajua sana bt they are ready to die kwa chama Chao tena wanachama wengi ni maskini wa kutupwa nyumba ya udongo bt bendela ya chama mpya.

cc wa upinzani tunakuwa kama mtoto anae waona wazazi wake wazembe kisa baba wa rafiki yake wamenunua gari bt kasahau kuwa utajili c kama matako ambayo kila mtu anayo

leo unadhani wakina maita kova na wengine awajuhi some time upinzani unaonewa? lakini wa sababu ya kadi zao mfukoni na crown kichwani wanatumia vijana wao watupige mabomu ya machozi tu
fanya utafiti leo viongozi wote wa vyombo vya dola kama police, jeshini, tiss wakistaafu wakataka siasa wanakwenda kagombea chama gani kama si ccm? wakuu wa mkoa na wilaya ni wanajesh wastaafu so jiulize uanachama wamepata lini walikuwa na kadi za chama mfukoni na crown kichwani
leo ukiangalia lumumba alivyofanywa fanywa mbagala na police wakati wanaandamana kama ww ni ukawa kweli kweli usinge andika thread ya kuisifia ccm hapa
 
Soma with positive mind. Nasema hata majambazi hukabidhiana vyeo na kuachina madaraka japo kazi yao ni wezi. Ni sawa na Mwizi aliyekuja kwako kukwibia akaiba lakini akaondoka bila kukuua. Badala ya kutengeneza mlango imara wewe unalala mlango wazi kesho yake kisa hujauliwa.

Hao wezi wamekabidhiana matunguli ya kuendelea kutuibia lakini kwa amani. Nimesema wajinga ni sisi wananchi. Soma vizuri. Badala ya kufanya skimming hebu fanya scanning.
 
Back
Top Bottom