Mwakalinga Bujo
JF-Expert Member
- Oct 22, 2008
- 2,718
- 1,443
Hata January wa Makamba! Kweli JK amefanya ikulu iwe rahisi kwa kila mtu kukaa pale kama mkuu Wa nchi.
Mi naona makamba yupo kwenye category ya hao marais wazuri coz kwa uthubutu wake wa kutangaza hadharani kuwa anahitaji kuwatumikia watanzania kama rais na kutupa sisi fursa ya kumpima kwa kina ni jambo ambalo linaonyesha uzalendo, uadilifu, na nia ya dhati ya kuwatumikia watanzania
Hivi mlitaka awafanyie nini? hivi wewe umeifanyia Tanzania?
Mtu ana nia ya kugombea Urais ili awatumikie Watanzania, wewe unauliza "umewafanyia nini watanzania".
Kwani kumpa mtu Urais ni fadhila kwa alichowafanyia? au ndiyo fikra za kirushwa-rushwa, hutoi kura mpaka ufanyiwe?
Hivi uko sawa?
Kuna uzi unasema 2015 ni Zamu ya Wakristo kwa sababu wamechoka kulazimishwa kuchinjiwa kuku wao kwa Ibada za Kiislamu ambazo kwa Wakristo ni sawa na kuabudu Miungu.Je Makamba ni Mkristo?
Kuna uzi unasema 2015 ni Zamu ya Wakristo kwa sababu wamechoka kulazimishwa kuchinjiwa kuku wao kwa Ibada za Kiislamu ambazo kwa Wakristo ni sawa na kuabudu Miungu.Je Makamba ni Mkristo?
Kuna uzi unasema 2015 ni Zamu ya Wakristo kwa sababu wamechoka kulazimishwa kuchinjiwa kuku wao kwa Ibada za Kiislamu ambazo kwa Wakristo ni sawa na kuabudu Miungu.Je Makamba ni Mkristo?
Kuna uzi unasema 2015 ni Zamu ya Wakristo kwa sababu wamechoka kulazimishwa kuchinjiwa kuku wao kwa Ibada za Kiislamu ambazo kwa Wakristo ni sawa na kuabudu Miungu.Je Makamba ni Mkristo?
Wewe ni agent Wa udini?
Mkuu, hizo ni propaganda tu; hatuwezi kusimamia hoja hiyo kwa masuala makubwa kama haya ya kumpata rais.
Rais atakayechaguliwa ataongoza watu wa dini zote, na katiba ya nchi pia haitoi mashiko kwa hoja ya udini. Naona kwa mambo nyeti kama haya tusimamie misingi ya umoja na kitaifa zaidi badala ya kugawanyika kwa tofauti kama hizo za kidini.
Tutalumbana na kufarakana sana, lakini hatima ya yote rais atakayechaguliwa hatauliza dini zetu; kama itakuwa kheri ni kwa wote, na kama ni shari ni kwa wote pia. Kwa maana hiyo faraka hizi tunazozijenga hazitakuwa na manufaa kwa yeyote, awe Mkristo, Muislamu au mwingine yeyote.
Vita ya panzi furaha kwa kunguru. Tunapolumbana, wachache wanajiandaa na namna ya kunufaika na mgogoro wetu!
Ni wazo nzuri na Mh; January anakiu na tanzania lakini ukweli nikwamba muda wake bado, ajafanya kitu cha kuweza kutushawishi vijan wenzake tumuunge mkono bado aridhike na unaibu waziri pia ashukur kwa kubebwa hadi alipofikia ajitumi tena na tena na mda ukifika hatosema anataka urais bali ni watanzania ss wenyewe tutamuomba agombee urais ila kwa sasa akitulize tu...!
Ndugu yangu JM wazo lako zuri sana, lakini omba kwanza ushauri jipime Mara Saba then amua.kuna wengi wametoa comments zao. Zipitie tena na tena. Ukiona kama kweli una fit kuwa Rais endelea lakini kama ni mihemuko ya ujana endelea kujiandaa. Wakati ukifika utaona tu wewe mwenyewe unaombwa au unaarifiwa kufanya hivyo. JM sio kama ulivyojieleza kwenye utangulizi wako ikionesha uzoefu wako Ikulu na ziara mbalimbali duniani. Watu uliokutana nao nk. Jipime tena na tena then go headDar es Salaam. Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba amesema hatakatishwa tamaa na hatorudi nyuma katika harakati zake anazoziita za fikra mpya na mawazo mapya za kushika dola na kwamba wazee wakae kando.
Hata hivyo, Makamba ambaye pia ni mbunge wa Bumbuli (CCM) amewashukuru watu wanaozungumzia nia yake ya kuwania urais mwaka 2015 na kutengeneza mjadala unaoendelea nchini, jambo ambalo alisema linaashiria kuwa dhamira yake imeeleweka.
Akiwa London nchini Uingereza mapema mwezi huu, Makamba alitangaza nia hiyo na kusema amefikia uamuzi huo kwa asilimia 90 lakini bado asilimia 10 katika baadhi ya mambo anayoendelea kuyatafakari, yakiwamo ya kuzungumza na makundi mbalimbali ya wazee, viongozi wa dini na viongozi waliopita ili apate ushauri wao kuhusu namna ya kufanya jambo hilo.
Julai 9, mwaka huu, Rais Jakaya Kikwete, ambaye anamzidi januari kwa miaka 24, alisema kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Kata ya Soni, Bumbuli mkoani Tanga kuwa Makamba anataka mambo makubwa, lakini hajamshirikisha.
Rais Kikwete alimtaka Makamba asilazimishe kwa kuwa wakati ukifika atapata kile anachokitaka. Mie hajaniambia na mie nasikia, alisema Kikwete.
Akizungumzia na gazeti hili jana kuhusu kauli ya Rais Kikwete, Makamba alisema: Ni kweli sijamwambia. Siku itakapofika yeye ni mwamuzi na mwenyekiti wa chama hivyo nitamweleza. Sitaki kumkwaza kwani na yeye ni wale waliopo katika kundi la asilimia kumi, alisema.
Zama za kizazi kipya za kutatua changamoto kwa kipindi cha miaka 30 hadi 50 ijayo zimewadia. Nitahakikisha mabadiliko ya haraka katika ardhi ya Tanzania kwani inawezekana rasilimali za kutosha zipo kilichobaki ni kuweka nidhamu katika nyanja zote.
Aliwashangaa wanaombeza akisema kuwa hawamkatishi tamaa kwa hilo.
Chanzo;Mwananchi
kila mtu kwa nafasi yake amuunge mkono kijana na kama tulivyoshauriwa na maaskofu jana kuwa kijana yeyote mwenye uwezo ni wakati wake sasa.2015 Ni mwaka wa kizazi kipya.
Kuna uzi unasema 2015 ni Zamu ya Wakristo kwa sababu wamechoka kulazimishwa kuchinjiwa kuku wao kwa Ibada za Kiislamu ambazo kwa Wakristo ni sawa na kuabudu Miungu.Je Makamba ni Mkristo?
Mawazo yako ni Mazuri sana na ndivyo tulivyolelewa Watanzania.Tatizo lilianza kwenye Uchaguzi wa 2010 wakati kampeni za udini zilipopigwa waziwazi Misikitini.Profesa Lipumba ni Shahidi kwa hili.Hivi sasa Viongozi waandamizi wanatukana Viongozi wa Kikristo hadharani,Makanisa yanachomwa Moto mchana na hakuna anayepatikana na hatia ilhali Wachaga na watu wa Kaskazini wanatukanwa kwa sababu ya kabila lao.Katika hali kama hii ni Lazima wakristo na wachaga wachukue hatua za haraka ili kujinusuru.