January: Sitorudi nyuma kuhusu urais 2015

January: Sitorudi nyuma kuhusu urais 2015

FIZI KALI

Senior Member
Joined
Jul 9, 2014
Posts
120
Reaction score
23
Dar es Salaam. Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba amesema hatakatishwa tamaa na hatorudi nyuma katika harakati zake anazoziita za fikra mpya na mawazo mapya za kushika dola na kwamba wazee wakae kando.

Hata hivyo, Makamba ambaye pia ni mbunge wa Bumbuli (CCM) amewashukuru watu wanaozungumzia nia yake ya kuwania urais mwaka 2015 na kutengeneza mjadala unaoendelea nchini, jambo ambalo alisema linaashiria kuwa dhamira yake imeeleweka.

Akiwa London nchini Uingereza mapema mwezi huu, Makamba alitangaza nia hiyo na kusema amefikia uamuzi huo kwa asilimia 90 lakini bado asilimia 10 katika baadhi ya mambo anayoendelea kuyatafakari, yakiwamo ya kuzungumza na makundi mbalimbali ya wazee, viongozi wa dini na viongozi waliopita ili apate ushauri wao kuhusu namna ya kufanya jambo hilo.

Julai 9, mwaka huu, Rais Jakaya Kikwete, ambaye anamzidi januari kwa miaka 24, alisema kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Kata ya Soni, Bumbuli mkoani Tanga kuwa Makamba anataka mambo makubwa, lakini hajamshirikisha.

Rais Kikwete alimtaka Makamba "asilazimishe" kwa kuwa wakati ukifika atapata kile anachokitaka. "Mie hajaniambia na mie nasikia," alisema Kikwete.

Akizungumzia na gazeti hili jana kuhusu kauli ya Rais Kikwete, Makamba alisema: "Ni kweli sijamwambia. Siku itakapofika yeye ni mwamuzi na mwenyekiti wa chama hivyo nitamweleza. Sitaki kumkwaza kwani na yeye ni wale waliopo katika kundi la asilimia kumi," alisema.

"Zama za kizazi kipya za kutatua changamoto kwa kipindi cha miaka 30 hadi 50 ijayo zimewadia. Nitahakikisha mabadiliko ya haraka katika ardhi ya Tanzania kwani inawezekana rasilimali za kutosha zipo kilichobaki ni kuweka nidhamu katika nyanja zote."

Aliwashangaa wanaombeza akisema kuwa hawamkatishi tamaa kwa hilo.

Chanzo;Mwananchi
 
Attachments

  • maka.jpg
    maka.jpg
    16.6 KB · Views: 632
Tumesikia ila kuona ndio bado!!!!

Yaani "tangibles" ndio tunaulizia zilipo!!!!
 
January, umewafanyia nini watanzania hadi uukomalie URAIS namna hii?
 
Rais wa Akudo impact huyo.......eti ni strategy yake ili atafutwe na aweze kuweka masharti kuwa nikikuunga mkono ntakuwa PM wako .......teehee. M.
 
kamanda tuendelee na mapambano ya kwenda kwenye mabadiliko.
 
bado tuko na escrow na IPTL wasitupumbaze ili tusahau, watanzania wanajua kuwa makamba hawezi kuwa rais otherwise awe rais wa masharobaro
 
bado tuko na escrow na IPTL wasitupumbaze ili tusahau, watanzania wanajua kuwa makamba hawezi kuwa rais otherwise awe rais wa masharobaro

wewe kama nani useme makamba hawezi kuwa rais?kUNA WENZAKO WALISEMA OBAMA HAWEZI KUWA RAIS NA LEO HII YUPO STATE HOUSE
 
Pambana tu January ukipata usinisahau.

kila mtu kwa nafasi yake amuunge mkono kijana na kama tulivyoshauriwa na maaskofu jana kuwa kijana yeyote mwenye uwezo ni wakati wake sasa.2015 Ni mwaka wa kizazi kipya.
 
Vijana wengi walioko CCM wanadhani wa tz wa sasa ni kama wale wa mwaka 47 ambao walikuwa wanalipigia hata jiwe ilimradi liwe limeandikwa CCM.Watanzania wa sasa wameelevuka tofauti na Makamba anavyo dhani.Zaidi ya ubunge ambao ni faida kwa wanabumbuli hakuna kitu chochote alichokifanya kwa Taifa zaidi ya kutegemea kubebwa na CCM ambayo imechokwa na wananchi wengi mpaka atake kupewa urais.Vinginevyo Makamba pamoja na CCM watapigwa za uso mpaka watapoteana.
 
kila mtu kwa nafasi yake amuunge mkono kijana na kama tulivyoshauriwa na maaskofu jana kuwa kijana yeyote mwenye uwezo ni wakati wake sasa.2015 Ni mwaka wa kizazi kipya.

Kwani kikwete alivyoingia hakuwa kizazi kipya...au alikuwa wa zamani?
 
Kuna mahali Januari anapotoka, huwezi kujenga nchi kwa kuwaweka wazee pembeni. Labda kama 'kuwaweka pembeni' inamaanisha kushirikisha wazee kivingine. Istoshe, kuwaweka wazee pembeni wakati ambao tayari serikali ya CCM haiwajali wazee ni kujiundia laana zisizo za lazima
 
wewe kama nani useme makamba hawezi kuwa rais?kUNA WENZAKO WALISEMA OBAMA HAWEZI KUWA RAIS NA LEO HII YUPO STATE HOUSE

Mkuu, uko sawa .............. nafikiri kila mtu anaweza kuwa Rais, given a chance!! Nafikiri hapa watu wanazungumzia uwezo wa kuifanya vema kazi hiyo. Ndiyo maana kuna marais ambao huwa wanaonekana ni bora kuliko wengine. Hata University huwa wanakwenda wengi tu lakini siyo wote wanatoka na First class .............. kuna Pass vilevile. Sasa hapa mjadara ni kuwa huyu Makamba yuko kwenye category ipi!!??
 
Dar es Salaam. Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba amesema hatakatishwa tamaa na hatorudi nyuma katika harakati zake anazoziita za fikra mpya na mawazo mapya za kushika dola na kwamba wazee wakae kando.

Hata hivyo, Makamba ambaye pia ni mbunge wa Bumbuli (CCM) amewashukuru watu wanaozungumzia nia yake ya kuwania urais mwaka 2015 na kutengeneza mjadala unaoendelea nchini, jambo ambalo alisema linaashiria kuwa dhamira yake imeeleweka.

Akiwa London nchini Uingereza mapema mwezi huu, Makamba alitangaza nia hiyo na kusema amefikia uamuzi huo kwa asilimia 90 lakini bado asilimia 10 katika baadhi ya mambo anayoendelea kuyatafakari, yakiwamo ya kuzungumza na makundi mbalimbali ya wazee, viongozi wa dini na viongozi waliopita ili apate ushauri wao kuhusu namna ya kufanya jambo hilo.

Julai 9, mwaka huu, Rais Jakaya Kikwete, ambaye anamzidi januari kwa miaka 24, alisema kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Kata ya Soni, Bumbuli mkoani Tanga kuwa Makamba anataka mambo makubwa, lakini hajamshirikisha.

Rais Kikwete alimtaka Makamba “asilazimishe” kwa kuwa wakati ukifika atapata kile anachokitaka. “Mie hajaniambia na mie nasikia,” alisema Kikwete.

Akizungumzia na gazeti hili jana kuhusu kauli ya Rais Kikwete, Makamba alisema: “Ni kweli sijamwambia. Siku itakapofika yeye ni mwamuzi na mwenyekiti wa chama hivyo nitamweleza. Sitaki kumkwaza kwani na yeye ni wale waliopo katika kundi la asilimia kumi,” alisema.

“Zama za kizazi kipya za kutatua changamoto kwa kipindi cha miaka 30 hadi 50 ijayo zimewadia. Nitahakikisha mabadiliko ya haraka katika ardhi ya Tanzania kwani inawezekana rasilimali za kutosha zipo kilichobaki ni kuweka nidhamu katika nyanja zote.”

Aliwashangaa wanaombeza akisema kuwa hawamkatishi tamaa kwa hilo.

Chanzo;Mwananchi

Labda awe rais wa wanyoa unga!
 
Labda awe rais wa wanyoa unga!

kweli kabisa kila mtu ccm anataka kuwa raisi duh ccm hawajiwezi hata kujiongoza kwenye chama ukawa ni sumu ya kuuwa ccm pamoja na wapambe wake wote
 
Back
Top Bottom