January: Sitorudi nyuma kuhusu urais 2015

January: Sitorudi nyuma kuhusu urais 2015

Mkuu, uko sawa .............. nafikiri kila mtu anaweza kuwa Rais, given a chance!! Nafikiri hapa watu wanazungumzia uwezo wa kuifanya vema kazi hiyo. Ndiyo maana kuna marais ambao huwa wanaonekana ni bora kuliko wengine. Hata University huwa wanakwenda wengi tu lakini siyo wote wanatoka na First class .............. kuna Pass vilevile. Sasa hapa mjadara ni kuwa huyu Makamba yuko kwenye category ipi!!??

Mi naona makamba yupo kwenye category ya hao marais wazuri coz kwa uthubutu wake wa kutangaza hadharani kuwa anahitaji kuwatumikia watanzania kama rais na kutupa sisi fursa ya kumpima kwa kina ni jambo ambalo linaonyesha uzalendo, uadilifu, na nia ya dhati ya kuwatumikia watanzania
 

Nitahakikisha mabadiliko ya haraka katika ardhi ya Tanzania kwani inawezekana rasilimali za kutosha zipo kilichobaki ni kuweka nidhamu katika nyanja zote.”


Chanzo;Mwananchi
Na yeye asije akasema "hajui ni kwa nini Tanzania ni maskini" Haya tulishayasikia.
 
Mi naona makamba yupo kwenye category ya hao marais wazuri coz kwa uthubutu wake wa kutangaza hadharani kuwa anahitaji kuwatumikia watanzania kama rais na kutupa sisi fursa ya kumpima kwa kina ni jambo ambalo linaonyesha uzalendo, uadilifu, na nia ya dhati ya kuwatumikia watanzania

Mkuu, uthubutu wa kutangaza pekee haumfanyi awe kiongozi bora!! Hata akina Lowasa, Sumaye na Membe walishatangaza ............although kwa namna tofauti. Anyway, hivi kweli unafikiria Makamba hapo alipo unaweza kumwamini kuliko watu kama Salim au Pombe Magufuli!!??
 
January, umewafanyia nini watanzania hadi uukomalie URAIS namna hii?

Hivi mlitaka awafanyie nini? hivi wewe umeifanyia Tanzania?

Mtu ana nia ya kugombea Urais ili awatumikie Watanzania, wewe unauliza "umewafanyia nini watanzania".

Kwani kumpa mtu Urais ni fadhila kwa alichowafanyia? au ndiyo fikra za kirushwa-rushwa, hutoi kura mpaka ufanyiwe?

Hivi uko sawa?
 
wewe kama nani useme makamba hawezi kuwa rais?kUNA WENZAKO WALISEMA OBAMA HAWEZI KUWA RAIS NA LEO HII YUPO STATE HOUSE

Jifunze kuheshimu maoni ya wenzio hata kama yanatofautiana na yako
 
Kusitaafu miaka 55-60 hapa tanzania sasa kijana anaposapoti kuongozwa na wastaafu badala ya kuwaunga mkono vijana wenzetu napata shaka na akili yake kama sio ya madafu basi tuharakishe kupiga marufuku viroba maana nchi imeharibikiwa hii. Leo hii wazee wenye kashifa za wizi wa waziwazi kabsa mchana kweupe kijana unakuja mitandaoni kuwapigia chepuo hawa wasitaafu. January ntakuunga mkono kwa nguvu zangu zote ni wakati muafaka kabisa kuleta fikra mpya kwenye ardhi aliyokabidhiwa enzi hizo kijana Mwl. Nyerere na Ndg Karume hawa walianza kubeba majukumu wakiwa vijana.
 
Mkuu, uthubutu wa kutangaza pekee haumfanyi awe kiongozi bora!! Hata akina Lowasa, Sumaye na Membe walishatangaza ............although kwa namna tofauti. Anyway, hivi kweli unafikiria Makamba hapo alipo unaweza kumwamini kuliko watu kama Salim au Pombe Magufuli!!??
Hoja apa ni kuleta fikra mpya za watu ambao wakiharibu kizazi cha miaka 30 ijayo kitawahoji maana kiumri bado wana safari ndefu hatutaki kutibu watu presure pale Ikulu tunahitaji watu wenye uwezo wa kuhimili mikikimikiki ila pole kama na wewe ni mstaafu yaani above 55 endelea kula mafao yako, saa kumi na mbili jioni hiyo sasa si mtatufikisha usiku wa manane au tutalala porini.
 
Makamba alibebwa na yusufu makamba wakati ule akiwa katibu mkuu wa ccm, sijui kwenye urais atabebwa na nani!
 
Ameshindwa kusimsmia mitandao ya simu inavyowaibia wananchi!! mf kukata hela hata usipotumia, unajiunga mb au dk ghafla zimepotea na pia kutuibia kodi nk. Kila mtandao sasa unaendeshwa kwa offer kosea upige hujajiunga, wababu vjjn lazima wapate mjukuu wa kuunga!!! Leo ndio tumuamini na kumpa nchi!!
"Kuwa mwaminifu kwa madogo nasi tutakuamini kwa makubwa"
 
Dar es Salaam. Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba amesema hatakatishwa tamaa na hatorudi nyuma katika harakati zake anazoziita za fikra mpya na mawazo mapya za kushika dola na kwamba wazee wakae kando.

Hata hivyo, Makamba ambaye pia ni mbunge wa Bumbuli (CCM) amewashukuru watu wanaozungumzia nia yake ya kuwania urais mwaka 2015 na kutengeneza mjadala unaoendelea nchini, jambo ambalo alisema linaashiria kuwa dhamira yake imeeleweka.

Akiwa London nchini Uingereza mapema mwezi huu, Makamba alitangaza nia hiyo na kusema amefikia uamuzi huo kwa asilimia 90 lakini bado asilimia 10 katika baadhi ya mambo anayoendelea kuyatafakari, yakiwamo ya kuzungumza na makundi mbalimbali ya wazee, viongozi wa dini na viongozi waliopita ili apate ushauri wao kuhusu namna ya kufanya jambo hilo.

Julai 9, mwaka huu, Rais Jakaya Kikwete, ambaye anamzidi januari kwa miaka 24, alisema kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Kata ya Soni, Bumbuli mkoani Tanga kuwa Makamba anataka mambo makubwa, lakini hajamshirikisha.

Rais Kikwete alimtaka Makamba “asilazimishe” kwa kuwa wakati ukifika atapata kile anachokitaka. “Mie hajaniambia na mie nasikia,” alisema Kikwete.

Akizungumzia na gazeti hili jana kuhusu kauli ya Rais Kikwete, Makamba alisema: “Ni kweli sijamwambia. Siku itakapofika yeye ni mwamuzi na mwenyekiti wa chama hivyo nitamweleza. Sitaki kumkwaza kwani na yeye ni wale waliopo katika kundi la asilimia kumi,” alisema.

“Zama za kizazi kipya za kutatua changamoto kwa kipindi cha miaka 30 hadi 50 ijayo zimewadia. Nitahakikisha mabadiliko ya haraka katika ardhi ya Tanzania kwani inawezekana rasilimali za kutosha zipo kilichobaki ni kuweka nidhamu katika nyanja zote.”

Aliwashangaa wanaombeza akisema kuwa hawamkatishi tamaa kwa hilo.


Chanzo;Mwananchi

komaa ndugu january makamba umeishapa baraka zote kutoka sehemu mbalimbali na wadau wapo tayari kukusupport kwa hilo.Ni wakati wa vijana kushika hatamu mbalimbali.
 
Vijana wengi walioko CCM wanadhani wa tz wa sasa ni kama wale wa mwaka 47 ambao walikuwa wanalipigia hata jiwe ilimradi liwe limeandikwa CCM.Watanzania wa sasa wameelevuka tofauti na Makamba anavyo dhani.Zaidi ya ubunge ambao ni faida kwa wanabumbuli hakuna kitu chochote alichokifanya kwa Taifa zaidi ya kutegemea kubebwa na CCM ambayo imechokwa na wananchi wengi mpaka atake kupewa urais.Vinginevyo Makamba pamoja na CCM watapigwa za uso mpaka watapoteana.

Umekalilisha brother,nenda bumbuli au waulize wanabumbuli watakuambia.Pia hiyo hoja yako haina mashiko Hata kidogo.Mbona rais kikwete alishinda urais akitokea jimbo LA chalinze ambalo lilikuwa Na changamoto Na had I Leo bado kuna changamoto.Au nenda masasi Kwa mkapa.Si kigezo cha kumfanya mtu asigombee urais.vinginevyo tutakosa marais Tanzania.
 
Ameshindwa kusimsmia mitandao ya simu inavyowaibia wananchi!! mf kukata hela hata usipotumia, unajiunga mb au dk ghafla zimepotea na pia kutuibia kodi nk. Kila mtandao sasa unaendeshwa kwa offer kosea upige hujajiunga, wababu vjjn lazima wapate mjukuu wa kuunga!!! Leo ndio tumuamini na kumpa nchi!!
"Kuwa mwaminifu kwa madogo nasi tutakuamini kwa makubwa"

Unahoja dhaifu sana.Rais kikwete aliingia ikulu akitokea wizara iliyokuwa Na changamoto nyingi Na had I Leo bado zipo.Pia jaribu kufuatilia mambo makubwa aliyoyafanya Makamba kusaidia wizara yake Na jimbo lake.Usiwe MTU Wa kukalilishwa.
 
Kuna mahali Januari anapotoka, huwezi kujenga nchi kwa kuwaweka wazee pembeni. Labda kama 'kuwaweka pembeni' inamaanisha kushirikisha wazee kivingine. Istoshe, kuwaweka wazee pembeni wakati ambao tayari serikali ya CCM haiwajali wazee ni kujiundia laana zisizo za lazima

Hakuna popote January kasema hatawaweka wazee pembeni.Wazee watabaki kuwa washauri
 
Back
Top Bottom