Mtemi mpambalioto
JF-Expert Member
- Aug 23, 2015
- 3,264
- 7,404
Waziri Makamba mie nakuomba sana huu mtego wa kulazimisha matumizi ya Gesi ya kupikia wakati hata sio Raslimali ya nchi yetu yaani inaletwa kutoka nje ni hatari sana kwa Ustawi na Usalama wa Taifa letu.
Ingekuwa hiyo gesi tunachimba wenyewe na tungeweka hata bei ya chini sana ambayo ingewafanya watumiaji wa mkaa waache wenyewe, lakini gesi hii hatuchimbi sisi, tena ipo chini ya mfanyabiashara fisadi mkubwa huoni unatuuza sisi Watanzania?
Mtungi wa kilo sita ni Tsh. 25,000, unafkiri watanzania wana hiyo hela ya kulipia gesi kwa mkupuo? hata hao wanaoweka sjui mita eti ukilipa mfano buku unatumia gesi ya buku, nani atavumilia gesi inakata ghafla mtu hajamaliza kupika?
Je, Bumbuli hawapikagi Maharage huko? wataweza kutumia gesi kupika maharage kwa bei hizo?
Unakataza mkaa halafu baadae gesi ije fika elfu 50 ndipo utakapowajua watanzania ni watu wa aina gani!
Je, baraka hizi za kifisadi na kuhatarisha usalama wetu kiuchumi anaubariki nani? ni RAIS au? daaaah mtuonee huruma jamani.