January Makamba: Natafakari kuwania urais 2015

January Makamba: Natafakari kuwania urais 2015

Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba amesema kuwa anatafakari iwapo awanie urais katika Uchaguzi Mkuu wa 2015, kutokana na kuwapo kwa watu wengi hasa ndani ya CCM, wanaomtaka kugombea nafasi hiyo ya juu ya uongozi wa nchi.

Makamba ambaye pia ni mjumbe wa Halmashauri Kuu (NEC) ya CCM alisema: “Kwanza ni kweli kwamba kuna ushawishi kuhusu suala hilo kutoka kwa vijana walioko nje na ndani ya chama, wanataaluma, baadhi ya wazee na watu wengine iwe kwa makundi au mtu mmoja mmoja wamekuwa wakinishawishi kugombea kwa muda sasa.”

Aliongeza: “Mwanzoni sikuona uzito sana, yaani sikuzingatia sana, lakini kwa kadiri siku zinavyokwenda ni kwamba ushawishi umekuwa mkubwa na hivyo niseme ni jambo ambalo sasa ninalitafakari kwa kina”.

Alisema ikiwa ataamua kuwania urais, atafanya hivyo wakati mwafaka kwa kuzingatia utaratibu utakaowekwa na chama hicho, lakini akasema kwa sasa si wakati wake. Makamba alikuwa akijibu hoja za gazeti hili lililotaka ufafanuzi wake kutokana na kuwapo kwa taarifa kwamba ameanza harakati za kuusaka urais katika Uchaguzi Mkuu wa 2015.

Gazeti hili lilidokezwa kuwa hatua yake hiyo imemwingiza katika mvutano usio rasmi na wanasiasa ambao tayari wameonyesha nia ya kuwania nafasi hiyo ya juu ya uongozi nchini, wakiwamo wale wa kambi ya urais aliyokuwa akidaiwa kuwa mmoja wao.

Awali iliaminika kuwa Makamba alikuwa katika kambi ya Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, lakini wachambuzi wa masuala ya kisisa wanasema ‘katika siku za karibuni mwenendo wake unaashiria kwamba si mmoja wa wanaomuunga mkono kiongozi huyo, bali ni mtu mwenye mipango yake binafsi ya kisiasa”.

Ana nini kipya cha kuutaka urais na atafanya nini kulisogeza taifa mbele?

Msimamo wake kuhusu sera ya Elimu ni nini hasa kipindi hiki ambacho taifa limegubikwa na udanganyifu kwenye mitihani na kushuka kwa kasi kwa kiwango cha Elimu nchini?
 
=> Mayai viza anafaa kuwa rais...??

=> FUTA HATA WAZO LA KUUPATA tena UNAIBU WAZIRI KTK MAISHA YAKO.....hivi January unaota au
ur talking this shit at the club...?? Hivi kweli dunia imekwishaaaa....

=> DON*T EVEN THINK OF THIS....**to be a president**....either at home or at Bumbuli....
 
Ana haki ya kugombea,lakini sina hakika kama ni muda muafaka kwake,anahitaji kujifunza zaidi.
 
Hata menzese nasikia kuna Rais wa watuma salam kunamfaa aende........................... still searching.........
 
....Poor Them Wapambe wanaokushawishi, Poor them....and You, my MP!:nimekataa
 
eti ooh kuna msukumo wa makundi mbalimbali kumtaka agombee! ni kina nani hao wanaomshawishi? mbona hawataji?

Siku hizi taasisi ya rais imekua chaka la makanjanja kila mtu anataka kuwa rais, si lazima uwe na chama.
 
Kwa heshima ya babaake wamemzawadia Ubunge na Unaibu Waziri sasa anaona anaweza kuwa Rais. Tanzania sasa tumeisha kama tuna manaibu waziri kama huyu ambae anaweza kufikiria kuwa Raisi, amshukuru Rais kumwonea kumpa hiyo kazi na akae kimya maana hafaikuwa hata mweyekiti wa mtaa. Acha watanzania tunajua mnavyopeana hivyo vyeo ila usione umepewa sentimiter sasa unataka meter you are a joke.
 
Pole sana Makamba naona vijana Wako hawataki kukunga mkono kwenye hili.
Jipange 2025 unaweza ukatosha.
 
Kwani John Komba ameshajiuzulu urais wa bendi ya ToT? Kwani katiba ya ToT inasemaje?
 
Nimekuwa nikijiuliza bila kupata jibu la uhakika kwamba Mhe Drx5 JK ataacha legacy gani. Nilikaribia kujiridhisha kuwa atakumbukwa kwa kuruhusu mchakato wa Katiba mpya (japokuwa awali alipinga) lakini baadaye nimejiridhisha kuwa hiyo itakayotoka ni katiba mpya mbovu. Itabidi tuanze upya. Sasa nimeipata legacy ya uhakika ya Mhe Drx5 - amerahisisha urais wa Tanzania. Nami MPIGA ZEZE sasa natangaza nia🙂 Naomba mnipige tafu wana JF.
 
Kwa lipi hasa we Makamba Jr? Ama kweli uraisi umefanywa rahisi sana na JK. Ptuuu......
 
Kwa taarifa yako wewe Makamba na wenzako huko CCM; kuhusu nani atawekwa na CCM kugombea kiti cha uraisi 2015 ni njia mojawapo ya CHADEMA itakayofanya mgombea wao wa uraisi apite. Sasa acha nikuambie wazi, wewe kuwa mgombea uraisi wa CCM ni ticket mojawapo ya CHADEMA kushinda uraisi. Salaam kwa Lowasa.

Hahhah, kuna members wamenifurahisha uchambuzi wao: 1. Kumbe kashawishiwa hajaamua mwenyewe? aendelee kushawishiwa. This is a very well thought comment. Hatufai kabisa mtu ambaye ana kuwa na dream kubwa hivyo a few months before tena as a result of kushawishiwa na wanaofaidika na kumpamba! He should be advised to read biographies of leaders. JK mwenyewe tu had a dream since he was a boy. 2. Nyingine naiacha kwa sasa!
 
Akiwa rais naomba operation kimbunga (sjui itakua awamu ya ngapi) wanifurushe wanipeleke watakapoona nafaa!
 
Kupata Ubunge tu huko Bumbuli anadhani anaweza kuiongoza nchi...

Sitaki kuzuia ndoto zake...lakini nafikiri anaota ndoto za mchana kweupe akiwa anatembea.
Anafikiri Uraisi ni mchezo siamini wakati huu ni muafaka kwake kiota ndoto ya Uraisi,tunataka kuona tija kwenye ubunge wake kwanza.Huku Bumbuli kuna matatizo lukuki ambayo yanamhimtaji sana na hajayakamilisha,Maji safi kwa wanainchi;Madawati ktk shule za msingi;Soko la mazao ya wakulima kama Chai,Kahawa n.k sasa iweje mara hii anahitaji Ukuu wa Kaya...????

Asidanganywe na hao wanaomshawishi, bali ajipambanue na kujipima mwenyewe asipoteze muda wa kuwatumikia wana-Bumbuli.
 
Well kama kasema seriously Chadema jiandaeni kuchukua hii nchi bila jasho!!!!!

Kama wapambe wake wanapima upepo basi huu uzi utawapa sehemu ya majibu muhimu!!!!!!
 
Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba amesema kuwa anatafakari iwapo awanie urais katika Uchaguzi Mkuu wa 2015, kutokana na kuwapo kwa watu wengi hasa ndani ya CCM, wanaomtaka kugombea nafasi hiyo ya juu ya uongozi wa nchi.

Makamba ambaye pia ni mjumbe wa Halmashauri Kuu (NEC) ya CCM alisema: “Kwanza ni kweli kwamba kuna ushawishi kuhusu suala hilo kutoka kwa vijana walioko nje na ndani ya chama, wanataaluma, baadhi ya wazee na watu wengine iwe kwa makundi au mtu mmoja mmoja wamekuwa wakinishawishi kugombea kwa muda sasa.”

Aliongeza: “Mwanzoni sikuona uzito sana, yaani sikuzingatia sana, lakini kwa kadiri siku zinavyokwenda ni kwamba ushawishi umekuwa mkubwa na hivyo niseme ni jambo ambalo sasa ninalitafakari kwa kina”.

Alisema ikiwa ataamua kuwania urais, atafanya hivyo wakati mwafaka kwa kuzingatia utaratibu utakaowekwa na chama hicho, lakini akasema kwa sasa si wakati wake. Makamba alikuwa akijibu hoja za gazeti hili lililotaka ufafanuzi wake kutokana na kuwapo kwa taarifa kwamba ameanza harakati za kuusaka urais katika Uchaguzi Mkuu wa 2015.

Gazeti hili lilidokezwa kuwa hatua yake hiyo imemwingiza katika mvutano usio rasmi na wanasiasa ambao tayari wameonyesha nia ya kuwania nafasi hiyo ya juu ya uongozi nchini, wakiwamo wale wa kambi ya urais aliyokuwa akidaiwa kuwa mmoja wao.

Awali iliaminika kuwa Makamba alikuwa katika kambi ya Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, lakini wachambuzi wa masuala ya kisisa wanasema ‘katika siku za karibuni mwenendo wake unaashiria kwamba si mmoja wa wanaomuunga mkono kiongozi huyo, bali ni mtu mwenye mipango yake binafsi ya kisiasa”.

Tanzania ni nchi ya ajabu sana, ndiyo nchi pekee ambayo kila mtu anahisi anaweza kuwa rais wa nchi.
 
Back
Top Bottom