January Makamba: Natafakari kuwania urais 2015

January Makamba: Natafakari kuwania urais 2015

Wana Bodi,

Msinitupie mawe naweka habari hii kama nilivyo ipata.

january.jpg


Naibu Waziri wa Mawasiliano Sayansi na Teknolojia January Makamba, amesema:

anatafakari iwapo awanie urais katika Uchaguzi Mkuu wa 2015 na hii ni kutokana na kuwepo kwa watu wengi hasa ndani ya CCM wanaomtaka kugombea nafasi hiyo ya juu ya uongozi wa nchi.
Makamba ambae pia ni mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM alisema: “Kwanza ni kweli kwamba kuna ushawishi kuhusu suala hilo kutoka kwa vijana walioko nje na ndani ya chama, wanataaluma, baadhi ya wazee na watu wengine iwe kwa makundi au mtu mmoja mmoja wamekuwa wakinishawishi kugombea kwa muda sasa.”
Source : Mwananchi


My Take:

Mustakabali wa Taifa letu uko mikononi mwetu.














 
Kesho Kimbunga atakutana na waandishi wa habari kuonesha nia yake ya kugombea Urais. Nasema hivyo kwa sababu kuna watu wa rika mbalimbali kuanzia wazee, wanawake, vijana na watoto wameniomba nigombee. Kuna makundi ya wakwezi, wafugaji na wakulima wameniomba nigombee. Mke wangu na watoto wangu wamenitaka nigombee. Bahati mbaya sijapata mfanyabiashara hata mmoja aliyeniomba nigombee. Nimepima na kutafakari maombi ya hawa watu nimeamua nisiwaangushe, hasa mke wangu na wanangu, hivyo nitagombea.
 
JK kaufanya urais umekuwa mwepesi mno kuufikiria
 
JK kaufanya urais umekuwa mwepesi mno kuufikiria

Kwa kweli hata muuza nyanya sokoni anaweza kufikiria na kutangaza nia kwa hali hii ilimradi aombwe na watu....
 
Aaaaa ndo aliekuwa akimsema mhe J.K kuwa anatamani amwachie urais kijana. Ndo huyu ni nini?

Ushauri wangu kwa CCM, kama wanataka anguko kuu wampitishe huyu agombee.
 
Urais siku hizi ni fashion kama ilivyo Bongo Flavour!!
 
mtu hujawahi kuchaguliwa kuwa hata diwani wa kata utaweza kuchaguliwa kuwa rais!? Nchi haiishi vituko
 
Ahakikishe TTCL serikali inamiliki 100% kwanza kabla ajatangaza nia yake hadharani mara baada ya kutafakari. akifanya hivyo tu nampa KURA yangu kwa moyo mmoja.
 
Comrades, huyu jamaa hafai hata chembe tu kugombea- hana uwezo wa kuongoza nchi, ni mchanga sana kisiasa, mnafiki mkubwa sana, afu ni mla rushwa huyu balaa! Alipokuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Madini na Nishati alikuwa anampigia kelele waziri wa wizara hyo huku janja yake ikiwa ni kujenga mazingira ya kuomba na kujipatia mrungula(rushwa). Taarifa zake tunazo kuhusu alivyowafanya Barrick na makampuni ya mafuta, yeye na kagenge kake!

Pia fuatilieni yaliyompata wakati akiwa Form 4 pale Moro

CCM kama wanataka Rais kijana ni bora mara 100 kuwafikiria akina Ngeleja, Nchimbi na Dr Hussein Mwinyi, cyo huyo selule!

Wakati ukifika data zitaanikwa hapa kwenye jamvi
 
Mzee Yusuph ameufanya urais wa JAHAZI MODERN TAARABU kuwa simple kwa kila mtu.
 
kwani ule urais wa miss utalii GIDEON CHIPUNGAHELO si ndio nasikia anaukbalika
 
Its funny mbeba mafaili wa jk na yeye anataka kuwa raisi?dunia imeisha
 
Haaa jamani huu urais wanauchukuliaje wamejisahau wanahisi wapo wenyewe tu wanaoishi hapa Tz kufanya wanayotaka 2015 Hawezekani kuongozwa kama vichaa.
 
Chuoni na kitaani kwetu pamoja na rafiki zangu wa fb vilevile wananiomba nigombee urais mwaka 2015 nikifika salama ila tatizo sina chama.
 
Back
Top Bottom