January Makamba: Natafakari kuwania urais 2015

January Makamba: Natafakari kuwania urais 2015

Money Stunna

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2011
Posts
13,053
Reaction score
6,335
Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba amesema kuwa anatafakari iwapo awanie urais katika Uchaguzi Mkuu wa 2015, kutokana na kuwapo kwa watu wengi hasa ndani ya CCM, wanaomtaka kugombea nafasi hiyo ya juu ya uongozi wa nchi.

Makamba ambaye pia ni mjumbe wa Halmashauri Kuu (NEC) ya CCM alisema: “Kwanza ni kweli kwamba kuna ushawishi kuhusu suala hilo kutoka kwa vijana walioko nje na ndani ya chama, wanataaluma, baadhi ya wazee na watu wengine iwe kwa makundi au mtu mmoja mmoja wamekuwa wakinishawishi kugombea kwa muda sasa.”

Aliongeza: “Mwanzoni sikuona uzito sana, yaani sikuzingatia sana, lakini kwa kadiri siku zinavyokwenda ni kwamba ushawishi umekuwa mkubwa na hivyo niseme ni jambo ambalo sasa ninalitafakari kwa kina”.

Alisema ikiwa ataamua kuwania urais, atafanya hivyo wakati mwafaka kwa kuzingatia utaratibu utakaowekwa na chama hicho, lakini akasema kwa sasa si wakati wake. Makamba alikuwa akijibu hoja za gazeti hili lililotaka ufafanuzi wake kutokana na kuwapo kwa taarifa kwamba ameanza harakati za kuusaka urais katika Uchaguzi Mkuu wa 2015.

Gazeti hili lilidokezwa kuwa hatua yake hiyo imemwingiza katika mvutano usio rasmi na wanasiasa ambao tayari wameonyesha nia ya kuwania nafasi hiyo ya juu ya uongozi nchini, wakiwamo wale wa kambi ya urais aliyokuwa akidaiwa kuwa mmoja wao.

Awali iliaminika kuwa Makamba alikuwa katika kambi ya Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, lakini wachambuzi wa masuala ya kisisa wanasema ‘katika siku za karibuni mwenendo wake unaashiria kwamba si mmoja wa wanaomuunga mkono kiongozi huyo, bali ni mtu mwenye mipango yake binafsi ya kisiasa”.
 
Kwa taarifa yako wewe Makamba na wenzako huko CCM; kuhusu nani atawekwa na CCM kugombea kiti cha uraisi 2015 ni njia mojawapo ya CHADEMA itakayofanya mgombea wao wa uraisi apite. Sasa acha nikuambie wazi, wewe kuwa mgombea uraisi wa CCM ni ticket mojawapo ya CHADEMA kushinda uraisi. Salaam kwa Lowasa.
 
au Komba anataka amwachie urais kule T.O.T.
mi kura yangu nampa Mwigulu Nchemba.....
 
Last edited by a moderator:
Mie nilidhani ameamua mwenyewe kumbe ameshawishiwa!!!!!! Basi aendelee kushawishika
 
Kwanza mimi wananishangaza watu wanaojipambanua kuwa Marais kwa sasa wakati hata hatujafahamu baada ya 2014 nchi itakuwa na serikali ya aina gani. Kauli kama hizi zinaonyesha kama 'wenzetu' tayari wanaifahamu Tanzania ya baada ya 2014.

Kwa jinsi political trend ilivyo na inavyoelekea kwa sasa, CCM kupitia baraza la Wazee wanatakiwa wazicheze vizuri karata zao kuhusu mgombea kupitia CCM kama walivyozicheza kwenye msuguano and immense pressure kutoka kwa wajumbe wa mkutano mkuu wa CCM kutaka kofia za Mwenyekiti na Rais zitenganishwe kutokana na matatizo yanayojitokeza katika utekelezaji wa ilani ya uchaguzi na uwajibikaji ndani ya chama na serikali.

To be honest and fair. Ni kweli Makamba Jnr ana haki kama Mtanzania ya kuingia kwenye mchuano wa kuwania ofisi kuu ya nchi lakini ndani ya fikra na mtazamo wangu, January Makamba kwa sasa hajakomaa kisiasa kuweza kupambana na changamoto zinazoendelea kulikabili taifa hasa ikichukuliwa kuwa tunakoelekea Tanzania inakabiliwa na changamoto za mgawanyo wa raslimali na kipato kutokana na unemployment among young adults hasa ikichukuliwa kuwa 44.3% ya watanzania wote kwa sasa wana miaka kuanzia 17-59, huku 34.7 wana umri wa miaka 15-35 kama ilivyobainishwa kwenye sensa ya watu na makazi 2012. Kuna bomu hapa limetegwa na linasubiri kulipuka kama litatingishwa zaidi na Novice President.

Rais wa baada ya 2015+ anatakiwa awe mkali, firm and fair. Tanzania ya baada ya 2015 haitakuwa na room for manoeuvre kwa Rais kuwa inaction, flipping and flopping hasa ikichukuliwa kwa sasa tuko kwenye mapambano ya "scramble for Tanzania" huku raslimali ikiwa ni ile inayojulikana kama Resource curse na huku bunge litakuwa siyo la absolute majority with absolute one sided power.

Wale wanaomshauri, wanamshauri vibaya kwa sababu ni kupoteza muda and resources kuingia kwenye mpambano ambao unafahamu kuwa utashindwa kuuhimili otherwise, hizo resources siyo kutoka kwenye jasho lake otherwise, akamuulize Mzee Mapesa ambaye wapambe walishauri na kujikuta akitumia resource zake za mfukoni karibia zote na kuambulia 4% ya kura 7 milioni zilizopigwa na kuachwa na upepo wa uchaguzi near bankruptcy.

Kama kweli anaamini atashinda basi hayuko in touch and aware with the political reality ya Tanzania.
 
Nauliza tuu haihusiani na hii thread!!!hivi kwa mfano hapa tanzania tunaweza kuruhusu mtu sho-ga kuwa prezdaa wa kisiasa!!!maana jamaa mmoja anapiga piga kelele ya kutaka kuwania urais na ilhali anajua kabisa kuwa hawezi kuwa hata iweje na yeye ni shoga(kwa nnavyosikia)
 
Kupata Ubunge tu huko Bumbuli anadhani anaweza kuiongoza nchi...
 
Urais utake wewe halafu usingizie wananchi eti wanakuomba ugombee urais kwa kazi ipi uliolifanyia taifa ili watz wakutake ugombee urais na siyo kwamba unataka taifa ndilo likufanyie?.
 
Kweli kuishi kwingi kuona na kusikia mengi,na mimi natangaza nia wajameni
 
. . .labda dimond kamuomba akagombee kuwa Rais wa wasafii.
 
Wewe ni Jembe go go January go... Ulivyokuwa na akili ndogo utasema hata Alinda ameniomba nigombee Urais... Lol Majanga
 
eti ooh kuna msukumo wa makundi mbalimbali kumtaka agombee! ni kina nani hao wanaomshawishi? mbona hawataji?
 
Back
Top Bottom