January Makamba must go

January Makamba must go

Maisha ya watanzania wengi ni magumu sana kwa wakati huu
Upatikanaji wa umeme wa uhakika unasaidia angalau kwa kiasi fulani kuganga hela za kuendesha maisha kwa shida shida hivyohivyo

Tunapokuwa na umeme wa kubahatisha unatuweka kwenye hali gani

Lakini mbali na watanzania maskini ni hasara kiasi gani inatengenezwa kunapokatika umeme?

Makamba aondoke atuachie TANESCO yetu
Kwanini waziri Kalemani aliondolewa na alikuwa anafanya vizuri?

Kuna siri gani kati ya Rais kumuweka Makamba kwenye hii wizara?

Dunia ya mwaka 2015 kurudi nyuma siyo ya 2021 Makamba asitake kuturudisha nyuma ni jambo lisilowezekana

Kwa kipindi hicho tuliamini umeme hautoshi tukaishi maisha yale lakini kumbe tunao umeme wa kutosha kabisa ni ujinga ujinga wa makanjanja wachache tu

Mamilioni wakose umeme ili wajinga wachache wa import generators?

Mtu mwenye mawazo haya hafai hata kuwa baba wa familia watoto wake inabidi asaidiwe kulea stupid

MAKAMBA AONDOKE UWAZIRI UMEMSHINDA


Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
Shida yako hasa ni Makamba, au ni umeme? Kama ni Makamba, basi hilo litakua ni dua tu la kuku! Mpaka yule aliyemteua ajisikie kufanya hivyo unavyo taka wewe.
 
Tumpe muda mkuu,akiharibu mbona watanzania wa mwaka huu sio wale wa miaka ile...!
 
Mmhh

Mkuu jadili hoja usijadili mtu, Unasema maisha Màgumu na Mhe Nape Nnauye anasema mambo mazuri maisha rahisi

Wakati wa Magufuli watu walimjadili Magufuli anayafanya maisha màgumu, Leo hayupo maisha kumbe ni yale yale

Tambua kila mtu anafikiria tumbo lake kwanza, Kila mtu anafamilia yake

Makamba Yeye sio Tanesco wala mtunga Sera, Watunga sheria wapo Bungeni

Wakiamua Bungeni Tanesco iuzwe itauzwa tu mkuu

Mkuu wahi kwa mbunge wako ukamwambie asipitishe hoja ya Tanesco kuuzwa

Acha uwoga NBC Bank ilivunjwa Leo NMB Bank ipo kila wilaya na baadhi ya kata inasidia watu wengi

Serikali haiwezi fanya biashara lazima mashirika baadhi yauzwe

Mkuu acha uwoga, Ubepari upo
Image ya nchi inatokana na rais aliyepo
Kuanzia Nyerere mpaka Samia kila Rais ameongoza kwa namna yake na alileta impact zake kwa maana hiyo hatuwezi kujadili ng'ombe lazima tujadili hawa watu wanaopewa mamlaka

Makamba tunaona impact zake hatuna umeme wa uhakika
Lazima tuhoji
Kalemani tuliona impact zake hakukuwepo na hii shida lazima tujadili mtu

Nape hana experience na anachokiongea


Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
The man is not tactical upuuzi alioufanya ni kwenye board member kutokuweka technician wa maswala ya umeme ata mmoja na CEO ni clueless kwenye energy business; so who is going to advice him appropriately on the course of action when challenges arise.

Wengine tulisha sema huyu mtu anaji expose mapema on his abilities apparently ni clueless, hivi unaendaje sehemu kama TANESCO kwa malengo ya kupeleka mabadiliko bila ya kuwa na allies wa ndani; pili who makes changes without considering ‘change management’ strategies.

Alivyoanza TANESCO ni sawa na viongozi wa nchi za magharibi wapeleke mabadiliko kwenye proffesional sector. Changes which might be deemed unfair by workers bila ya kutafuta support ya unions zao kwanza for morale to get people on board with the changes, hiyo migomo itakayofuata utatia akili.

Bado sasa mipango yake mengine ya uwekezaji aijafanikiwa bado; the worst is yet to come trust me.

Kuna vitu mwanzoni tu unajua vinaelekea wapi.
 
Yanategenezwa mazingira ya kubinafisisha Tanesco na mabwawa ya umeme.
It won’t solve the main problem ‘quality costs’ that comes first in hierarchy of TANESCO’s solutions na ni jambo ambalo waziri na mkurugenzi hawana habari nalo kabisa; wapo busy na mambo ambayo hayana shabaha ya kutatua matatizo ya leo.

Hiyo siyo mifuko ya plastic TANESCO inataka know how za electrical engineering and business acumen particular operation strategy ya maswala ya umeme; sio sehemu ya kukurupuka tu kama alivyoanza.
 
Maisha ya watanzania wengi ni magumu sana kwa wakati huu
Upatikanaji wa umeme wa uhakika unasaidia angalau kwa kiasi fulani kuganga hela za kuendesha maisha kwa shida shida hivyohivyo

Tunapokuwa na umeme wa kubahatisha unatuweka kwenye hali gani

Lakini mbali na watanzania maskini ni hasara kiasi gani inatengenezwa kunapokatika umeme?

Makamba aondoke atuachie TANESCO yetu
Kwanini waziri Kalemani aliondolewa na alikuwa anafanya vizuri?

Kuna siri gani kati ya Rais kumuweka Makamba kwenye hii wizara?

Dunia ya mwaka 2015 kurudi nyuma siyo ya 2021 Makamba asitake kuturudisha nyuma ni jambo lisilowezekana

Kwa kipindi hicho tuliamini umeme hautoshi tukaishi maisha yale lakini kumbe tunao umeme wa kutosha kabisa ni ujinga ujinga wa makanjanja wachache tu

Mamilioni wakose umeme ili wajinga wachache wa import generators?

Mtu mwenye mawazo haya hafai hata kuwa baba wa familia watoto wake inabidi asaidiwe kulea stupid

MAKAMBA AONDOKE UWAZIRI UMEMSHINDA


Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
Kwani huwezi ukatulia, ukaandika kama mtu mwenye utulivu wa akili? Namna yako ya uandishi, utaifanya hoja yako ipuuzwe.
 
Mimi si mwanasiasa ni mtanzania tu Makamba hata akiwa Rais ni kwa faida yake siwezi kuwa na chembe ya chuki kuhusu hilo
Kwa sasa haipiti siku umeme haujakatika na ikibidi zaidi ya mara moja kama leo umeme umekatika saa tano na umerudi saa tisa jana vilevile na nikila siku tulisha sahau haya mambo wewe tuambie ni nini hiki siyo kukosa hoja na kutuambia tuna chuki kivipi

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
Uko wapi? Sisi wengine hatujashuhudia hayo.
 
Kuna siri gani kati ya Rais kumuweka Makamba kwenye hii wizara?
Kuna familia Kama mbili zinaiona hii nchi Kama ya kwao.
Huyo kapigiwa chapuo na kajaya.
Wanadai maza ndiye akamzalia kajaya risla moja ,afu maza ni binti wa mdogo aliyemfuata babaye makongoro.
Akaunti ya kigogo saivi haishambulii uongozi ulioko madarakani Mana ni wao wanafanya wanachotaka.
Muda si muda utamuona Pena naye anapeta
 
Image ya nchi inatokana na rais aliyepo
Kuanzia Nyerere mpaka Samia kila Rais ameongoza kwa namna yake na alileta impact zake kwa maana hiyo hatuwezi kujadili ng'ombe lazima tujadili hawa watu wanaopewa mamlaka

Makamba tunaona impact zake hatuna umeme wa uhakika
Lazima tuhoji
Kalemani tuliona impact zake hakukuwepo na hii shida lazima tujadili mtu

Nape hana experience na anachokiongea


Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
Kalemani aliendesha wizara kisanii na kelele nyingi. Vijiji vingi umeme uliingizwa kwenye nyumba 4 - 10, kisha anakimbilia kwenye TV kueleza vijiji vilivyopata umeme. Kodi kupitia LUKU ikamwumbua na uwongo wake.

Tunataka viongozi watendaji na siyo wapiga kelele ili waonekane. Ile awamu ya Rais kuzindua visima vya maji na madaraja ya watembea kwa miguu, imekwishapita.
 
Mmhh

Mkuu jadili hoja usijadili mtu, Unasema maisha Màgumu na Mhe Nape Nnauye anasema mambo mazuri maisha rahisi

Wakati wa Magufuli watu walimjadili Magufuli anayafanya maisha màgumu, Leo hayupo maisha kumbe ni yale yale

Tambua kila mtu anafikiria tumbo lake kwanza, Kila mtu anafamilia yake

Makamba Yeye sio Tanesco wala mtunga Sera, Watunga sheria wapo Bungeni

Wakiamua Bungeni Tanesco iuzwe itauzwa tu mkuu

Mkuu wahi kwa mbunge wako ukamwambie asipitishe hoja ya Tanesco kuuzwa

Acha uwoga NBC Bank ilivunjwa Leo NMB Bank ipo kila wilaya na baadhi ya kata inasidia watu wengi

Serikali haiwezi fanya biashara lazima mashirika baadhi yauzwe

Mkuu acha uwoga, Ubepari upo
Mashirika gani ya biashara yauzwe wakati walishauza yote kwa wezi. Yaliyobaka ni idara za serikali. Labda sasa fisadi wana mpango kuuza serikali kuanza na tanesco. And then magereza. Watu walaku hua hawashibi.
 
Back
Top Bottom