January Makamba hawezi kufanya propaganda mbele ya Rais Samia. Huu ni wakati wa vitendo, January chapa kazi

Ovyo kabisa. Amewatuma kujisafisha. Huyu mtu ni mbinafsi anafikiria mambo yake tu yajayo. Juzi tu amepewa wizara ya nishati,tunaona madhara yake. Mwendazake nilimuelewa sana kumpiga pembeni huyu mtu. Huyu toka kitambo simkubali. Ni miongoni mwa waroho wa madaraka. Hayuko kwa ajili ya wengi
We hujatumwa kumchafua
 
We hujatumwa kumchafua
Hakuna mtu mwenye akili timamu aanze kumchafua Makamba.

Makamba anahukumiwa na utendaji wake wa kazi na majibu yake mepesi kwenye maswali magumu yanayo husu uhai wa mwanadamu.
 
Yaani WaTz siku hizi waelewa sana,kilichobaki kichwani mwa WaTz ni maamuzi magumu tu. Huwezi kuwalevya na sifa za kitoto za mifuko. Kwani alifanya nini cha ajabu kwenye hiyo mifuko ya prastic?. Yeye alikuwa ni spiker tu ya kilichokubaliwa na baraza. Kipi cha ajabu alifanya?. Ulitegemea vurugu kwenye usitishwaji mifuko prastic?. Hata Kenya tu ilifanyika hivyo hakuna shida iliyotokea.

Kama makambo kuna sehemu alifanya vizuri angebaki kwenye wizara ya JPM.
 
Na bado

Ila pesa za January zinaliwa kizembe Sana. Hawa vijana wa kufanya spinning hamna kitu. Aajiri wengine

Mifuko ya plastic ni nguvu ya JPM, wananchi walikuwa wanamuogopa na kumlaumu JPM
Enzi zile kiongozi yoyote akitoa agizo Raia wanatekeleza!
Serikali ile ilikuwa imara!
Mimi ninayeandika ni mwalimu, nakumbuka kabla ya JPM tulikuwa tunawadharau waalimu wakuu, lakini huwezi amini, ndani ya utawala wa JPM sisi waalimu tuliwatii Sana waalimu wakuu

Sinario Kama hii ndio inayojitokeza huko tanesco, wafanyakazi wameacha uwajibikaji
Acha uongo
Waulize hata boda boda watakwambia ni Makamba sio JPM
 
Mifuko ya plastic nchi hii iliondolewa bila hata Mende kuguswa kitu ambacho mwendazake na serikali nzima hawakuamini. Wananchi wa Tanzania walistaajabu uwezo na akili yake na mikakati yake kufanikisha suala la mifuko bila kutumia polisi wala vyombo vingine vya Usalama. Kila moja anakumbuka wivu wa mwendazake kuwapelekea kumtoa kwenye cabinet hata hivyo hakulamba miguu.

Baada ya Rais Samia kushika madaraka na kufanya ministry audit alikua kugundua wizara ya nishat inamakando kando mengi ndio maana Waziri aliyekuwepo wakati wote alikua anatetemeka akikutana na Rais Samia.

Sasa kwa mtu makini kama Rais Samia na askari wake January Makamba watu wanaoamini katika utaalamu na suluhisho la uhakika wasingeweza kufanya mambo ya siasa kwenye mambo muhimu kama ya umeme. 5 Years hakuna maintenance, hakuna unategemea nini katika nchi kubwa kama hii.

Whether imeagizwa warekebishe mitambo ili kuzuia mitambo hio kuharibika au ni ishu ya maji kupungua bado sina mashaka na watu hawa.
Promo ya kindezi kweli kweli
 
Back
Top Bottom