January Makamba: CCM imeshashinda majimbo 176 mpaka sasa

January Makamba: CCM imeshashinda majimbo 176 mpaka sasa

Huu mchezo wa saikolojia ambao makamba hawezi. Majimbo gani hayo??? Tume ina kigugumizi cha kutangaza matokeo hata ya hapo dar??? Isitoshe tume na jeshi la polisi wanatoa kauli gani kwa kura zinazokamatwa kwenye magari ya serikali??? Kura feki zimezagaa mpaka bar, zimetoak wapi???
 
Hadi sasa Muungano wa UKAWA unaelekea kushinda majimbo zaidi 165 kwa mujibu wa Matokeo yanayokusanywa kutoka maeneo mbalimbali huku ikithibitisha mawaziri na Manaibu Waziri zaidi ya 13 wameangushwa kwa kishindo

Ni vyema tume ya Uchaguzi sasa ikajiandaa kutangaza matokeo Rasmi kwa Haraka ili kudumisha Amani na pia tuendelee kufuatilia kinachojiri Kwenye Matokeo ya Urais Zanzibar na Muungano

Hadi Sasa Matokeo ya Zanzibar yameshajumlishwa kinachopaswa kufanyika ni itifaki ya Tume kutimia tu kama inavyoelekea kwenye Urais wa Muungano.

Ben Saanane
 
Haya bana wacha tuendelee kuwa masikini milele... nimenyoosha mikono juuu... na watatushughulikia sana mwaka huu

Mkuu nimecheka sana kauli yako maana ulikuwa front line kupigania mabadiriko. ila naona umekubali mziki. hahahha
 
Tulieni wana UKAWA sindano iingie taratibuuuuuu.............
 
ushindi wa kulazimisha, kupindisha taratibu, kutisha watu, kufanya hila na yote yanayofanana na hayo.

Ila kwanini ametangaza wakati Tume haijamaliza kutangaza? Akamatwe akatiwe adabu
 
Kama ni kweli, Ccm imepoteza Majority power bungeni na inalazimika kuunda serikal ya Mseto.Ielezwe pia amepoteza mangapi

mkuu uko serious ama unatania 176/264
then uwe umepoteza majority power
 
Naskia mnapika matokeo ya Urais. Huku mkitangaza yale ambayo CCM inaongoza na kukawia yale ambayo mmeburuzwa kundaa Psychologically wananchi kuzoea kuwa CCM itashinda. Je mnafanya huu utoto?

Wenye akili zetu hatudanganyiki.
 
CCM wamepata wapi Mandate ya kutangaza matokeo ilhali wao siyo Tume wala wasimamizi?? hivi Wengine wakijitangazia itakuwaje??

Nchi ngumu sana hii
 
Taarifa inayotolewa hivi punde na Januari Makamba ni kwamba CCM imeshapata matokeo yote ya uchaguzi. Hata hivyo, wanasubiri mamlaka husika kutangaza matokeo hayo. Hata hivyo amesema kuwa CCM imefanikiwa kushinda majimbo 176 huku ikikomboa majimbo 12 yaliyokuwa yanashikiliwa na upinzani.

Amesema pia mwenendo wa matokeo ya Urais hauna tofauti na matarajio ya wana CCM na Watanzania wengi.

Hongera CCM. Hongera Magufuli

Source: Azam Two
kwa nini tusikuamini lizaboni, hua unatoa za jikoni.
 
Hahahahaaaaa, ccm sasa ndiyo imekuwa kama chama cha upinzani, hakika watafanya kazi kwa maslahi ya wananchi sasa, tabia za ccm za zamani zote ziko ukawa
 
CCM wamepata wapi Mandate ya kutangaza matokeo ilhali wao siyo Tume wala wasimamizi?? hivi Wengine wakijitangazia itakuwaje??

Nchi ngumu sana hii

Wamechanganyikiwa hao
 
Back
Top Bottom