January Makamba awavaa wanaosema Mwenge wa Uhuru umepitwa na wakati

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,817
4,566
1686745907616.png

Waziri wa Nishati, January Makamba amelaani tabia za baadhi ya wanasiasa wanaodai kwamba Mwenge wa Uhuru umepitwa na wakati na ni mzigo kwa Taifa.

Makamba akipinga hoja hiyo amesema Mwenge ni tunu na nembo ya Taifa ambayo inapaswa kuheshimiwa hivyo, kusema kuwa unasumbua wananchi ni kuitusi nchi.

Makamba ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Bumbuli ameitoa kauli hiyo leo Jumatano Juni 14, 2023 katika Jimbo lake baada ya Mwenge kukimbizwa kwenye jimbo hilo na kuzindua na kukagua miradi tisa yenye thamani ya Sh779.1 milioni.

"Mwenge ni tunu na heshima kubwa kwa Taifa letu, tukiwa na mawazo na mtazamo kuwa hauna maana ni sawa na kuitusi nchi yetu. Wakati tunapata Uhuru hotuba ya kwanza ya Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere alisema sasa tunawasha Mwenge ili uangaze nchi nzima," amesema.

Amesema kuwa Mwenge wa Uhuru ni kielelezo cha uhuru, utaifa na ndoto hivyo, ni kiunganishi cha Watanzania na ni kielelezo cha Mtanzania.

Pia Soma:
- Mwenge wa Uhuru upo kwa faida ya nani?

- Kwa Sasa, Mwenge una Madhara kwa Jamii Kuliko Faida.Ufutwe.
 
Huyu akili yake haiko sawa yaani moto unausababisha maambuki ya ukimwi, Kutumia fedha na muda wa kufanya kazi kwa jambo lisilo zalisha chochote ye anaona sawa....nyerere alikuwa ni mjamaa na sio mwizi mbona wao wamebadilika wamekuwa mabepari na wezi?
 
Kwa hiyo kwa mtazamoo wake na zile kasumba tulizolishwa maskulini kwa kuimbishwa zile nyimbo za kuuwasha mwenge yeye bado anazikubali na kuamini?
Yaani kuwa mwenge na kuuweka kilimanjaro, umurike ndani na hata nje ya mipaka na kuleta matumaini? Yaani mwenge umurike maadui wa nchi. Hivi kweli mtu mzima na elimu yake yote bado anaamini kasumba za nyerere? Hadi lini Tanzania tutaendelea kuabudu moto? Mwenge ni moto unapitishwa tanzania kote kila mwaka na mnaupigia makofi, vigelegele na kuuchezea ngoma kisha kuuchangia pesa za sadaka! Kila mwaka mara moja! nyerere kawapeni dini yake na hadi leo bado hamjaamka tu?
 
Mwenge wa uhuru sio tatizo, tatizo ni kutumia mabilioni kuukimbiza kila mwaka huku wamama ili wanifungue wananunua mahitaji yote ya kujifungua, wanafunzi wanatapeliwa na walimu kwa mgongo wa pesa ya tution huku serikali ikishindwa kulipa overtime za walimu
 
Back
Top Bottom