Januari Makamba: Wanaohoji kuchelewa Mradi wa JNHPP ni upuuzi tu

Hata mimi sikuamini mpaka nilivyosikiliza video. Hii nchi tumerogwa sio bure kama viongozi ndio hawa
Viongozi ni weupe vichwani na wanajitahd sana kuwaroga watz,

Kaz yetu kubwa ni kupasua matunguli Yao na kuwafungua watz waliofungwa. Amen
 
Leo Waziri wa Nishati, Januari Makamba amewajibu wanaohoji kuchelewa kwa Mradi wa Bwawa la Julius Nyerere JNHPP ni upuuzi tu na kama hawaamini majibu yake basi wamuue.

"Ukisema Bwawa litachelewa kwa sababu hii na hii wanasema muongo huyo, mshenzi huyo basi njooni mniue basi kama hamuamini, wote ni upuuzi tu" amesema Makamba

Chanzo: Wasafi Media


Huyu mzee hii awamu amekuja kuwa mjinga sn
 
Babako anakufunza kulamba asali ,umevimbiwa ukasahau hawa unaowaita wapuuzi ndo wamekurinia hiyo asali. Bahati mbaya system ya kiswahili ungetoa huo utoporo kwa yule mwamba ungekuwa unahemea udigoni.
 
Waziri Makamba namkubali sana kwa utendaji, sina mashaka nae, ni waziri mbunifu, makini na mchapa kazi.

Sasa Jambo la msingi ni kwa watendaji wote wa Tanesco, vhapeni kazi kwa masilahi ya watanzania, acheni majungu.
Haaaa haaaa mwizi wa paper .utamlinganisha na kijana Bashe, anachapa kazi na kiwaheshimu wananchi acha huyu janja janja
 
Makamba hauaminiki kwa sababu una majibu yasiyojitosheleza na yanayochelewa kuja kwa wakati, na mara nyingine hauna consistence kwenye majibu yako.

Leo unasema hivi, ukipingwa unabadilika kesho unasema tofauti about same thing, ni kama unaangalia uchochoro wa kujifichia kwenye majibu yako, ndio maana huaminiki.

Mfano.

1. Kuhusu ile crane ya tani 26 uliyoagiza toka nje, ukaambiwa mbona hata hapa Tanzania zipo crane zenye uzito huo? ukasema inatakiwa isiyohamishika, ok fine, mpaka leo hiyo isiyohamishika iko wapi?

2. Au kuhusu tatizo la umeme lililowahi kuwepo, ukatutangazia mgao wako nchi nzima kwa kisingizio awamu iliyopita mitambo ilikuwa haifanyiwi service, then after ukadai mgao utasahaulika, lakini wapi, mgao bado upo mpaka juzi tumetangaziwa mwingine.

Baadae ulivyoona mambo sio ukabadilika, mkatangaza sababu ya mgao wa umeme ni ukame, ghafla akatokea mtendaji bwawa la Nyumba ya Mungu akasema maji yaliyopo kule yanatosha kuwasha umeme kwa muda mrefu ujao, Makamba kimya...

Halafu hii tabia yako ya kukimbilia kuwaona wanaokuhoji ni maadui, ndio itakumaliza kabisa, usijione special usiyehojika, you are not, hicho cheo chako ni cha umma, wewe sio CEO wa private company.

Mwanzo ukihojiwa ulisema tatizo ni uwaziri wako, kama vile wewe ndie waziri wa Nishati pekee uliyewahi kutokea nchi hii.

Leo unawaambia wanaokuhoji wakuue, hii maana yake unakimbia majukumu yako, unajiona unaonewa unapoulizwa kuhusu yale yanayoihusu wizara yako, sasa kama hutaki kuulizwa wewe unataka aulizwe nani?

Anyway, tatizo ni la yule aliyekuweka hapo, amekudekeza matokeo yake unajiona kama "mtoto wa mama usiegusika", sasa kwa huu utoto wako, mtachafuka wote.
Katika watanzania huru kifikra na wewe ni mmoja wapo, anahojiwa waziri mkuu uingereza na kuwajibika sembuse huyu kambakamba wa huko machakani mbumbumbuli!
 
"Ukisema Bwawa litachelewa kwa sababu hii na hii wanasema muongo huyo, mshenzi huyo basi njooni mniue basi kama hamuamini, wote ni upuuzi tu" amesema Makamba
Huyu dogo angenyamaza achape kazi watu waone matokeo, vijembe alivyorithishwa na baba yake si kipaumbele cha watanzania
 
Hatua hii ilifanya kuwepo mabadiliko katika makubaliano ya kuanza kutengeneza mitambo tarehe 30 Mei, 2020 badala ya tarehe 16 Juni, 2019 iliyokuwa imekubalika awali. Hivyo, kuchelewa kwa miezi kumi na tatu (13);

Kwa mjibu wamaelezo hayo hapo juu, hakunashaka kua, mradi ulianza kusuasua mwanzoni mwa utekelezaji wake.
 
Ule utoto wa neno "njooni mniue" huku kwenye social media, ndio bila aibu waziri mzima anatumia kwenye majukwaa rasmi?!
Hii inaonyesha kibri na kujiamini kulikopitiliza! Ni kama vile anasema ....
Kwamba vyovyote iwavyo hapo yupo na hakuna wa kumchomoa!
 
Hilo bwawa lingeisha bei ya umeme ingepungua pia na hao watu huko kijijini ulikopeleka majiko ya gesi wangetumia majiko ya umeme. Weee nini bwana unatuon a sisi mazuzu malizia mradi weee shubamiti
Majiko ya umeme ni way of the past. But nakubaliana na wewe kwenye kupunguza gharama
 
Asijisahaulishe yaliyomtokea kaka yake Muhongo.
Alafu anaongea kwa kujichekesha ionekane haina haja saana kuuuliza!

Hivi hii wizara ilimkosea nini Mungu kwanini huwa inapata wanaofanana!
 
Hii inaonyesha kibri na kujiamini kulikopitiliza! Ni kama vile anasema ....
Kwamba vyovyote iwavyo hapo yupo na hakuna wa kumchomoa!

Kwa katiba hii anaweza kufanya ama kuongea lolote na hatafanywa lolote. Ikifika wakati wa uchaguzi wataagiza vyombo vya dola visimamie yeye kukaa madarakani.
 
Back
Top Bottom