Januari Makamba: Wanaohoji kuchelewa Mradi wa JNHPP ni upuuzi tu

saidoo25

JF-Expert Member
Jul 4, 2022
602
1,407
Leo Waziri wa Nishati, Januari Makamba amewajibu wanaohoji kuchelewa kwa Mradi wa Bwawa la Julius Nyerere JNHPP ni upuuzi tu na kama hawaamini majibu yake basi wamuue.

"Ukisema Bwawa litachelewa kwa sababu hii na hii wanasema muongo huyo, mshenzi huyo basi njooni mniue basi kama hamuamini, wote ni upuuzi tu" amesema Makamba

Chanzo: Wasafi Media

 
Makamba hauaminiki kwa sababu una majibu yasiyojitosheleza na yanayochelewa kuja kwa wakati, na mara nyingine hauna consistence kwenye majibu yako.

Leo unasema hivi, ukipingwa unabadilika kesho unasema tofauti about same thing, ni kama unaangalia uchochoro wa kujifichia kwenye majibu yako, ndio maana huaminiki.

Mfano.

1. Kuhusu ile crane ya tani 26 uliyoagiza toka nje, ukaambiwa mbona hata hapa Tanzania zipo crane zenye uzito huo? ukasema inatakiwa isiyohamishika, ok fine, mpaka leo hiyo isiyohamishika iko wapi?

2. Au kuhusu tatizo la umeme lililowahi kuwepo, ukatutangazia mgao wako nchi nzima kwa kisingizio awamu iliyopita mitambo ilikuwa haifanyiwi service, then after ukadai mgao utasahaulika, lakini wapi, mgao bado upo mpaka juzi tumetangaziwa mwingine.

Baadae ulivyoona mambo sio ukabadilika, mkatangaza sababu ya mgao wa umeme ni ukame, ghafla akatokea mtendaji bwawa la Nyumba ya Mungu akasema maji yaliyopo kule yanatosha kuwasha umeme kwa muda mrefu ujao, Makamba kimya...

Halafu hii tabia yako ya kukimbilia kuwaona wanaokuhoji ni maadui, ndio itakumaliza kabisa, usijione special usiyehojika, you are not, hicho cheo chako ni cha umma, wewe sio CEO wa private company.

Mwanzo ukihojiwa ulisema tatizo ni uwaziri wako, kama vile wewe ndie waziri wa Nishati pekee uliyewahi kutokea nchi hii.

Leo unawaambia wanaokuhoji wakuue, hii maana yake unakimbia majukumu yako, unajiona unaonewa unapoulizwa kuhusu yale yanayoihusu wizara yako, sasa kama hutaki kuulizwa wewe unataka aulizwe nani?

Anyway, tatizo ni la yule aliyekuweka hapo, amekudekeza matokeo yake unajiona kama "mtoto wa mama usiegusika", sasa kwa huu utoto wako, mtachafuka wote.
 
Leo Waziri wa Nishati, Januari Makamba amewajibu wanaohoji kuchelewa kwa Mradi wa Bwawa la Julius Nyerere JNHPP ni upuuzi tu na kama hawaamini majibu yake basi wamuue.

"Ukisema Bwawa litachelewa kwa sababu hii na hii wanasema muongo huyo, mshenzi huyo basi njooni mniue basi kama hamuamini, wote ni upuuzi tu" amesema Makamba

Source: Wasafi Media




Kufa kwako hakuhusiani na bwawa letu. Wewe ufe au usife tunachotaka bwawa letu likamilike na kufanya kazi.
 
Leo Waziri wa Nishati, Januari Makamba amewajibu wanaohoji kuchelewa kwa Mradi wa Bwawa la Julius Nyerere JNHPP ni upuuzi tu na kama hawaamini majibu yake basi wamuue.

"Ukisema Bwawa litachelewa kwa sababu hii na hii wanasema muongo huyo, mshenzi huyo basi njooni mniue basi kama hamuamini, wote ni upuuzi tu" amesema Makamba

Source: Wasafi Media



Mara ya kwanza nilidhani mleta mada ni shihata Taga sukumagang lililokubuhu johnthebaptist
 
Leo Waziri wa Nishati, Januari Makamba amewajibu wanaohoji kuchelewa kwa Mradi wa Bwawa la Julius Nyerere JNHPP ni upuuzi tu na kama hawaamini majibu yake basi wamuue.

"Ukisema Bwawa litachelewa kwa sababu hii na hii wanasema muongo huyo, mshenzi huyo basi njooni mniue basi kama hamuamini, wote ni upuuzi tu" amesema Makamba

Source: Wasafi Media



Wachane wachane hao pimbi
 
Hatua iliyofikiwa katika utekelezaji wa Mradi wa Kufua Umeme wa Julius Nyerere wa MW 2115

Mheshimiwa Spika
, Mradi wa kufua Umeme wa Julius Nyerere wa MW 2,115 kwa kutumia maporomoko ya maji ya Mto Rufiji ulianza kutekelezwa rasmi tarehe 15 Juni, 2019. Kamati ilijulishwa kuwa, kufikia tarehe 31 Desemba, 2021 utekelezaji wa mradi katika maeneo yote ulikua umefikia asilimia 53.25 ambapo kimkataba ulipaswa kuwa umefikia asilimia 97.38 ukiwa nyuma kwa asilimia 44.13

Mheshimiwa Spika, Kamati ilielezwa kuhusu asilimia ya hatua iliyofikiwa katika utekelezaji kwa maeneo makuu manne (4) ikilinganishwa na hatua iliyopaswa kuwa imefikiwa kufikia Mwezi Disemba 2021 kama ifuatavyo;- a. Uhandisi na Usanifu (Engineering) ambao ni asilimia 3.84 ya kazi yote katika mradi kufikia Mwezi Disemba 2021 ulipaswa kuwa umefikia asilimia 3.77 hata hivyo hali halisi ilikuwa ni asilimia 3.16 ikiwa nyuma kwa asilimia 0.61; b. Manunuzi (Procurement) ambayo ni asilmia 26.93 ya mradi kufikia Mwezi Disemba 2021 yalipaswa kuwa yamefikia asilimia 26.85 hata hivyo hali halisi ilikuwa ni asilimia 12.49 ikiwa nyuma kwa asilimia 14.36; 22 c. Ujenzi (Construction) ambayo ni asilimia 68.42 ya mradi, kufikia Mwezi Disemba 2021 ulipaswa kuwa umefikia asilimia 66.61 hata hivyo hali halisi ilikuwa ni asilimia 37.40 ukiwa nyuma kwa asilimia 29.21; na d. Kumaliza na Kuwasha kituo (Commissioning and Startup) ambayo ni asilimia 0.81 ya mradi, kufikia Mwezi Disemba 2021 utekelezaji ulipaswa kuwa asilimia 0.05 lakihi hali halisi ilikuwa ni asilimia 0.00.

Mheshimiwa Spika, Kamati ilihoji ili kuhafamu sababu za kuchelewa kutekelezwa kwa mradi kwa asilimia kubwa (44.13%); na ilielezwa sababu mbalimbali zikiwemo: a. Mkandarasi kuchelewa kuleta Wataalamu wanaohitajika Kimkataba kwani kufikia Mwezi Disemba 2021 alikuwa na wataalamu (key design experts) 22 kati ya 27 na wataalamu wa ujenzi (construction execution experts) 154 kati ya 177 waliopaswa kuwepo eneo la mradi, hali iliyosababisha kazi za usanifu kusuasua na kuathiri kazi za ujenzi; b. Mkandarasi kuchelewa kuwapata watengenezaji wa mitambo ya kufua umeme kwani wakati wa zabuni, Mkandarasi aliwasilisha Kampuni mbili (2) za Andritz na Voith kuwa ndio watengenezaji wa mitambo ya kufua umeme.

Hata hivyo, maKampuni hayo mawili yalikataa kushiriki kutengeneza mitambo kwa kisingizio kwamba mradi haukidhi viwango vya Kimataifa vya mazingira, hali ambayo ilisababisha kufanya mabadiliko ili kumpata mtengenezaji mbadala ambaye ni Kampuni ya Dongfang Electric International Corporation (DEC) kutoka China.

Hatua hii ilifanya kuwepo mabadiliko katika makubaliano ya kuanza kutengeneza mitambo tarehe 30 Mei, 2020 badala ya tarehe 16 Juni, 2019 iliyokuwa imekubalika awali. Hivyo, kuchelewa kwa miezi kumi na tatu (13);

Mkandarasi kutokuwa na Wataalamu Wabobezi katika kazi za Ujenzi wa Jengo la Mitambo na Usimikaji wa Mitambo. Utendaji duni wa kazi zinazokosa ubora stahiki zimekuwa zikipelekea kurudiwa kwa kazi mara kwa mara na kusababisha maendeleo hafifu ya mradi, mfano Gati Na. 9 katika Jengo la Mitambo na daraja la Kudumu lipo chini ya viwango na kupelekea ucheleweshaji wa kazi zingine;

Mkandarasi kutokuwa na Kiongozi Mkuu wa Mradi (Contractor Representative). Kwa hali ya utekelezaji wa mradi iliyofikiwa sasa, Mkandarasi anatakiwa kuwa na Kiongozi Mkuu ambaye atashirikiana na Msimamizi Mshauri ili kutatua changamoto zinazojitokeza kwa wakati; e. Mkandarasi kuchelewa kutoa Oda ya Manunuzi ya Mitambo na Vifaa vya Mradi. Mkandarasi alichelewa kutoa idhini ya kuanza kutengenezwa kwa Mitambo na vifaa vya awali kama vile draft tube gates kutoka nchini China kwa wastani wa muda wa miezi nane.

Ucheleweshaji wa kufika kwa mitambo hiyo, kumeathiri maendeleo ya kazi za ujenzi; f. Mkandarasi kuchelewesha Usanifu na Kazi katika maeneo ya Mradi ikiwemo Kingo Ndogo za Bwawa na Eneo la kutolea Maji katika Mitambo (Tail Race Channel).

Kucheleweshwa kwa uwasilishaji wa usanifu wa ujenzi wa njia ya kutolea maji (tail race 24 channel) na kingo ndogo za bwawa (saddle dams no.1) imepelekea kazi za ujenzi wa maeneo haya kuwa nyuma ya muda uliopangwa kukamilika kulingana na matakwa ya Mkataba; g. Mkandarasi kutokuwa na mitambo/vifaa vya ujenzi vya kutosha kwa mujibu wa Mpango Kazi.

Hii imesababisha uzalishaji duni wa zege ikilinganishwa na kiasi kinachotakiwa kwa mahitaji yaliyopo ya ujenzi, hasa katika kukidhi mahitaji ya kiwango cha zege kinachohitajika kwa ujenzi kwa siku katika maeneo ya jengo la mitambo, kingo ndogo za bwawa na daraja la kudumu; h. Upungufu wa Wataalamu Wanaosimamia Mkandarasi. Kulingana na Mkataba ulioingiwa baina ya TANESCO na TECU, wataalamu waliotakiwa kusimamia kazi za mradi ni 37 lakini kwa kadri kazi zilivyoendelea kutekelezwa, ilibainika kuwa wataalamu 37 hawatoshi na upungufu huo ulikuwa unasababisha baadhi ya kazi kutosimamiwa ipasavyo.

Hata hivyo TECU imeongeza wataalamu 24; na i. Upungufu wa magari kumi na nne ya kusimamia mradi ambapo TANESCO inashughulika kutatua changamoto hii kwa kununua magari mapya.

Mheshimiwa Spika, Mradi wa Bwawa la Mwalimu Nyerere ni mradi muhimu sana hasa ikizingatiwa kuwa ni Mradi wa Kimkakati. Ni matamanio ya Kamati kuona kuwa Mradi huu unakamilika kwa wakati ili kuongeza kiwango cha umeme katika Gridi ya Taifa na kuchochea kasi ya ukuaji wa uchumi wa nchi.

Mheshimiwa Spika, Hata hivyo, Kamati hairidhishwi na kasi ya utekelezaji wa mradi huu kwani maeneo mengi yapo chini ya wastani wa utekelezaji kimkataba.

HII NI SEHEMU YA TAARIFA YA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA NISHATI ILIYOWASILISHWA BUNGENI FEBRUARI 15, 2022 AMBAO WAZIRI WA NISHATI ANATAMKA HADHARANI KWAMBA NI WAPUUZI
 
Makamba ni mwizi siku zote,kazi ya kwanza aliyoingia nayo Hapo wizarani ni kitafuta bilioni moja ili kulipa ule mkopo aliouchukua kwa mgongo wa Bumbuli.

Na ikaishia kupukutika kwenye kuusaka uraisi 2015.

Alipo Makamba na 10% ipo.

Asijione kama mtu mjanja kuliko watanzania wote.

Time Will Tell!
IMG-20220331-WA0020.jpg
 
Back
Top Bottom