Watu wanasahau kuwa Chadema ina miaka karibu ishirini sasa ...na ilishuhudia hujuma zote zilizofanywa kwa vyama vingine, ambavyo vilikuwa na nguvu kutokana na umaarufu wa Viongozi wake. Ukiwa na kiongozi maarufu kuliko nia ya chama kuwasaidia wananchi, ni rahisi sana kukihujumu chama hicho. Maana wananchi wanakuwa hawaelewi nia ya chama kwao bali wanaelewa umaarufu wa kiongozi. Umaarufu wa kiongozi ukipotea na chama kinapotea kwa wananchi. Nia ya chama siyo rahisi kuipoteza ikishakuwa maarufu na kujulikana sawia kwa wananchi.
Hili Chadema waliliona mapema wakaweka msingi imara wa kufuata miiko ya uongozi wa chama kwa kutumia katiba ya chama na taratibu nyingine za chama. Vyote hivi vinaheshimiwa ndani ya chama, na vinasaidia sana kuipa NIA ya Chadema ya kuwaletea wananchi maendeleo kwa kufuata misingi ya kidemokrasia umaarufu hivyo kutambulika kwa wananchi kirahisi.
Kosa la kiongozi kuwa maarufu kuliko nia ya chama liliwapata NCCR-Mageuzi,kwa Mrema kuwa maarufu na kutumia umaarufu huo kukiua chama, hata alipoenda TLP... kinachojulikana sasa ni Mrema zaidi ya nia ya Chama cha TLP kwa wananchi. Kutokana na hilo pale TLP wala hakuna hata dhamira thabiti ya kuchukua dola. Nia ya TLP siyo maarufu kwa wananchi kwa namna kinavyoendeshwa hivyo si rahisi kupewa dola.
CUF...ilikumbwa na hilo pia Maalim Seif na Prof. Lipumba wamekuwa maarufu kuliko chama na hili limefanya umaaruf wao uipoteze CUF kwenye siasa za ushinda kuchukua dola. Mnajua kilichotokea Zanzibar 2010....Lipumba aliyasema yote kwenye ile video aliyorekodiwa Msikini Dar es Salaam. Nia ya CUF siyo maarufu kwa wananchi, Pale maarufu, ni Maalim Seif na Lipumba, na Hamadi Rashid alitaka kuleta mabadiliko ya kuondoa umaarufu wa viongozi pale CUF (sina hakika kama alitaka kujenga umaarufu wa nia ya CUF kwa wananchi ama la) kilichompata sote tunakijua.
Chadema waliamua kujifunza kutokana na makosa ya wenzao vizuri sana, ndiyo maana...hakuna mtu kuwa maarufu kuliko nia ya chama ya kuwaletea wananchi maendeleo kwa njia ya kidemokrasia. Nia hii ya chama ndiyo iliyo maarufu pale Chadema. Na ni kwa umaarufu wa nia Chadema kwa wananchi...watanzania wengi wanakiunga mkono chama hicho japo wengine wanakiunga mkono kwa kujificha.