Kero: Ubungo bus terminal Na wizi wa risiti

Miiku

JF-Expert Member
Oct 8, 2014
3,835
2,630
Alaani wasaalani......



wasomi, wadau na wataalamu popote pale mlipo tunaomba Msaada wenu wa elimu juu ya Hii risiti .

Leo nilienda kumsindikiza ndugu yangu aliyekuwa anasafiri katika kituo cha mabasi ubongo, tulipofika getini yule mhusika wa geti la kuingia ndani alitusimamisha na kutuomba tulipe hela Tsh. 200 kila mmoja, mimi nikauliza wote tunachangia ? Yaani Abilia na msindikizaji ?.. Akajibu ndiyo. Tukalipa ile hela kisha tukaingia ndani Huku tukizisoma zile tiketi ambazo ziliandikwa Maelezo kadhaa lakin Maelezo ya mhimu yaliandikwa Hivi " USHURU WA VYOO UBUNGO BUS TERMINAL Tsh 200" kisha nikamwambia mwenzangu " kumbe ukishikwa na haja unaonesha Hii risiti kisha unaingia kujisaidia "...

Wakati tukiendelea kusubiri bus lijae ili ndugu yangu aanze safar ghafla akahisi haja ndogo na akaenda hadi vilipo vyoo akakuta maandishi yameandikwa malipo ya kuingia chooni ni Tsh. 200 na anayepokea hela yupo dirishani. Ndugu yangu hakutaka kuleta ujuaji wa sheria kuhusu ile risiti, alichofanya ni kulipa ile hela Tsh 200 kisha akaingia kumaliza haja zake .

Ndugu yangu alipotoka akaniuliza mbona risiti imeandikwa ushuru wa vyoo na nimeenda chooni nimelipa tena ?... Pia safari Hii mbona risiti ya chooni sijapewa ?

Nikamjibu mimi na wewe hatujui lakini Ngoja tushirikishe wataalamu wa Haya maswala watufafanulie ;

1) Malipo ya risiti za getini ni Kwa ajili ya nini ?

2) Abilia na msindikizaji wote anatakiwa kunipa Tsh. 200 getini ili waingie ?

3) Ukienda chooni ukalipa ili ujisaidie unatakiwa udai risiti au sheria za pale haziruhusu udai risiti ?

Msaada wenu tafadhari

Sent using Jamii Forums mobile app
 
ubungo muasisi wa wizi huo alikufa kwa kuumwa na MIJIBWA! alikuwa hana dini yaani mpagani!
pale kichaka cha kujilia hela tena bila woga wakati huu awamu ya 5
 
Ila ukikatia tiketi ya kusafiria kabla ya kuingia ndani ukiwaonyesha ulipii Kwa yule mwenye tiketi
 
Kuongia mtu yeyote asiye na ticket ya safari ni 300 inaelekea wanatoa risiti hizo za 200 kwa ajili ya wizi. Hizo pesa wanachukua wao.
 
Siku moja nasafiri kwenda mkoa SAA 10 alfajiri tuko getin unaonesha tiketi unaingia nakaribia getini nasikia jina langu linaitwa kuwa nimepoteza ticket kujisaji kweli ticketi sina nikamfata jamaa akakaza akasema bila buku 7 za uokotaji hatoi ticket ikabid nimmpe tu
Mpaka Leo najiuliza nilidondosha kweli au walichomoa mfukoni

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Siku moja nasafiri kwenda mkoa SAA 10 alfajiri tuko getin unaonesha tiketi unaingia nakaribia getini nasikia jina langu linaitwa kuwa nimepoteza ticket kujisaji kweli ticketi sina nikamfata jamaa akakaza akasema bila buku 7 za uokotaji hatoi ticket ikabid nimmpe tu
Mpaka Leo najiuliza nilidondosha kweli au walichomoa mfukoni

Sent using Jamii Forums mobile app
Ungeenda kwenye basi lako ulilokatia tiketi wanakuwa na Copy , hakukuwa na sababu ya kuwapa hao vibaka pesa

Sent from my iPhone using Tapatalk
 
Back
Top Bottom