BigTall
JF-Expert Member
- Mar 9, 2022
- 654
- 1,598
Ni takribani mwezi mmoja sasa maeneo mengi ya Kibaha MailiMoja kuna changamoto kubwa ya maji na majibu ya Mamlaka ya Maji yamekuwa ya kuungaunga.
Awali walitoa taarifa kuwa maji yatakoseka kwa siku chache takribani tatu hadi nne kutokana na maboresho ya mitambo yam aji, lakini ilipita wiki mbili bila maji.
Baada ya hapo baadhi ya maeneo yakaanza kupata maji mdogomdogo, wale waliokosa walipouliza wakajibiwa kuwa yatatoka ndani ya saa 24 kwa kuwa bado hayana nguvu ndio maana yanatoka kwa uchache katika baadhi ya maeneo.
Hali hiyo imeendelea hadi sasa na mwisho wake tuna wiki moja hakuna maji kabisa n ahata zile sehemu ambazo yalikuwa yanatoka mdogomdogo kwa sasa hayatoki kabisa.
Hali ni mbaya, wakazi wa MailiMoja hasa mitaa ya Mpiji, Muheza, Tankini kwa Mbonde na kwingineko tuna hali mbaya, kwani tunalazimika kutumia fedha nyingi kununua maji n ahata hayo tunayoyapata napo kazi ni kubwa.