Jana nimeng'atwa na nyoka mguuni!

kibaravumba, Akhsante sana mkuu
Issue ya dawa zake kuwa gharama sana niliwahi kuisikia hivyo nilijua ninakwenda lakini ni mtiti, unayosema yanawezekana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Akhsante sana mkuu
Hilo nitalifanyia kazi kwa usalama zaidi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Shida ya hizi kitu, unaweza kukaa nazo kila mara unazicheki. Ila ikipita miaka kadhaa hujakutwa na tatizo hata kuangalia ufanisi wake unaacha. Siku la kutokea linatokea madude hayafanyi kazi,

Mfano rahisi ni kwenye Fire Extinguisher za magari, tunakaa nazo mpaka zina expire, au mwingine unakuta hata kutumia hajui.
 
Siku nyingine ikitokea fanya haya
1 ufunge mguu sumu isipande (hii nadhan ulifanya)
2 chanja mguu au sehem iliyoumwa ili ile damu iliyozuiwa na kamba iwe inatoka nje, inapotoka inatoka na sumu
3 kunywa mkojo

Halafu wahi hospital
Kuna hadithi ya kitambo sana Umenikumbusha, Tanga maeneo ya mabawa jamaa kang'atwa na nyoka... Akawa anaugulia asijue cha kufanya... Kuhu watu wengine wakijaribu kumsaidia lakini inaonekana nyoka alikuwa na sumu kali mno... Ghafla akapita bibi anauliza kinachoendelea,, kusikia kwamba jamaa kang'atwa na nyoka... Akamwambia asubiri dakika kadhaa akafuate dawa... Akamchukua binti aliyekaribu akaingia nae kwenye boma baada ya dakika chache wakarudi bibi kashikilia chupa ina maji... Jamaa anaambiwa hiyo ni dawa... Masharti yake unywe bila kuisikilizia.... Jamaa akanywa kisha akapona... Mwisho wa siku anaambiwa hiyo dawa ni mkojo.... Sikumbuki lilikuwa ni gazeti gani kati ya champion, kiu ama sani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Siku nyingine ikitokea fanya haya
1 ufunge mguu sumu isipande (hii nadhan ulifanya)
2 chanja mguu au sehem iliyoumwa ili ile damu iliyozuiwa na kamba iwe inatoka nje, inapotoka inatoka na sumu
3 kunywa mkojo

Halafu wahi hospital
Hakuna chochote hapo kinachosaidia kw mtu aliyeng'atwa na nyoka, kikubwa uking'atwa na nyoka kuwa mtulivu, uspanic maana utasababisha mapigo ya moyo kwenda haraka na hivyo sumu kuenea kwa haraka mwilini, alafu usitumie kiungo kilichong'atwa na nyoka, then straight hospital

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyo ni jini pepo kwanini hukukemea?
 
Pole sana kwa matatizo yaliyokukuta.Binafsi huwa siogopi nyoka hata kidogo nimewahi kung'atwa na nyoka Mara kadhaa lakini huyo nilipoka uhai wake.

Shukuru hakuwa black mamba/koboko kwa muda huu ungekuwa kaburini


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naam hakukuwa na anaejua kuendesha muda huo, mzee akiona naserereka kwenye kona na mia na ishirini alikuwa ananiuliza mara kwa mara najisikiaje....nadhani ni hofu ya kujua naanza kupoteza mdogo mdogo.

Sent using Jamii Forums mobile app
Pole sana mkuu, Mungu yu mwema kwa watu wake, Kuna ndugu yangu alikua anatembea usiku hivi, duh kumbe kamkanyaga nyoka ,akang'atwa akapiga kelele nimeng'atwa na nyoka, watu wanakimbia kumsaidia tayari akawa kashapoteza fahamu yani,tunashukuru alipona lkn.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dah! Si mchezo!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…