Jana nimeng'atwa na nyoka mguuni!

Jana nimeng'atwa na nyoka mguuni!

Watanzania
Tujifunze First Aid

Tuwe na First Aid kits majumbani kwetu. Tuwe na antivenom majumbani kwetu na tuwafundishe wote tunaoishi nao jinsi ya kutumia hizo aid kits.

Tukifanya hivi tutapunguza vifo vingi visivyo na msingi

Sent using Jamii Forums mobile app

Mkuu naomba unitajie Orodha ya antivenom ninazotakiwa kuwa nazo nyumbani
 
Mie siku nahamia makazi yangu mapya nilihakikisha hamna wadudu wowote kama nyoka, ng'e, tandu na ujinga ujinga mwingine niliimarisha usafi ndani na mita mbili nje ya ukuta ambako majirani bado hawajaendeleza. Pia uwa napiga fumigation kila miezi sita ile kubwa kabisa. Ila kwa maajabu ya muumba juzi nimekuta nyoka wa kijani kajilaza tulii juu ya mpapai na nilikuwa naenda kuchuma papai. Tulimuua
 
Hilo lipo dhahiri kwa sababu nimepitia majaribu mengi ndani ya muda mfupi eneo hili mpaka gari iliwahi kufa bila kujulikana sababu na ukirekebisha hapa panaharibika pale, ingawa kuna watu tofauti si chini ya kumi kwa nyakati tofauti waliniambia nijiandae kwani wenye mji wataniandama tu hawataki aje mgeni haswa mwenye kubadilisha mboga.

Sent using Jamii Forums mobile app
Na shukuru Mungu gari lako liliwaka siku hiyo
 
Vuta picha huna gari sasa na nyoka ni black mamba mzee tungekuwa tumekuzika
Huyu nyoka anaonekana wa kawaida kwa sababu hakuwadhulu hata mifugo ile we ulienda ukamkanyaga au alikuwa akijihami pia na yeye akakung'ata na kwa uwoga wake akasepa zake akakimbia
Kuanzia SAA NNE mpka SAA Tisa ndio unafika hospital huyu nyoka hakuwa na sumu Kali
Ingekuwa aina ya nyoka wenye sumu Kali usingefika mda huo wote hata kama uliufunga mguu
Ungekosa nguvu au kuzimia au kufa kabisa
Kuisha na watu ni jambo zuri
Kilicho kuokoa mzee ni gari na sio kitu kingine ndio maana ulivyofika hospital hali yako ilikuwa ishaanza kubadilika kuwahi kwako ndio pona yako

Fyeka vicha vya kalibu choma moto fuga wanyama ambao ni adui wa nyoka una watoto ukiona nyoka mmoja jua wapo wengi huwa wanaishi kimakundi watakusumbua na kukuletea madhara makubwa ukizalau safisha eneo lako mkuu
TAHADHARI KABLA YA HATARI
hao watoto wanacheza nje usiku akiingia ndani na kashajua una mifugo ataludi tena Leo kwenye kidole kesho shingoni au kichwani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu hongera umezunguka Sana kutunga story tumeshajua kumbe una Gari!!!!!
 
Habari

Waswahili wanasema hujafa hujaumbika, lakini pia wanasema usimdharau mtu....naam haya jana niliyathibitisha katika maisha yangu.

Nilifanikiwa kukamilisha kibanda pembeni ya mji ndipo ninapoishi na sina muda mrefu sana tangu nihamie hapo, kama ilivyo sehemu kama hizo nikaona nianzishe mifugo hivyo nikawa nao kadhaa.

Jana usiku nilisikia mbuzi na kuku wanajipiga piga katika mabanda yao hali ambayo si ya kawaida, kuangalia saa ni saa nane usiku nikahisi huenda ni mbwa ninaemfuga anawafanyia tabu hivyo nikatoka na kwenda kucheki, kufika nikakuta mlango wao umefunga kama kawaida na mbwa wala hana mishe nao yupo pembeni kabisa akidumisha ulinzi.

Nikazunguka nyuma ya banda eneo lenye wavu na huko kuna giza taa haifiki, mara ghafla kufumba na kufumbua kuna kitu kikanipiga mguuni! Nikamulika tochi ya simu nakuta kidole cha mguu kinavuja damu nyeusi na kwa mbali nyoka mkubwa akitoweka!

Awali niliishiwa nguvu kutokana na presha ya tukio hilo na kuwaza kuwa hiki ni kifo lakini nikaamsha wenzangu (walikuwa wanawake na watoto tu kwani kulikuwa na shughuli za kifamilia mjini hivyo ninaoishi nao walikwenda huko) wakanipa ujasiri na wazo la kuufunga mguu ili sumu isipande.

Nilikwenda kwa jirani ambae ni mzee wa makamo mwenye familia yake, akaniambia mwanangu tuwahi hospital tusipoteze muda maana hatujui nyoka huyo limit ya kuua kulingana na sumu yake.

Niliendesha gari kama mwendawazimu saa tisa tukawa mbele ya geti la hospital, niliwahiwa kupigwa sindano ya kuondoa sumu maana hali yangu ilianza kuwa tete na kisha wakasafisha sehemu husika na kuyatoa meno, pia wameshangaa nimefikaje umbali wote huo kulinganisha na tatizo husika....nikapewa dawa kadhaa pia na kuruhusiwa. Nimeamka naendelea vema na nakanyaga kama kawaida Alhamdulillah.

Kwa nini nimesema hujafa hujaumbika? Kwa sababu mpaka usiku nakwenda kulala nilikuwa mzima wa afya hivyo sikujua kuwa linaweza kunitokea jambo la kuhatarisha uhai wangu usiku huo.

Kwa nini nimesema usimdharau mtu?
Kwa sababu wengi wanapokua na visenti, usafiri au kibanda chenye angalau katika eneo husika haswa wakiwa wageni, huwadharau wenyeji au hata kuchagua watu wa kujenga nao mazoea, tazama nimesaidiwa na mzee nilimchukulia kama baba tangu nahamia pale...mzee ambae hupata riziki zake kwa kutumia baiskeli na panga kufanikisha kubeba mizigo ya kuni porini na kwenda kuuza mjini.

Dunia si yetu hatujui siku wala saa

Sent using Jamii Forums mobile app
Jirani yako ndiye ndugu yako wa kwanza.
 
'Snake in the City'- NatGeo!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
maelezo ya PDF na field ni tofauti kabisa.

kijijini inapigwa yowe nyumba ya jirani tu watu wanakusanyika dk 2 tu na wanasutana nani kachelewa ili adhabu zihusike. ukizubaa unapewa kesi.

kicheche au siafu wanavamia kuku au mwizi anakaba mbuzi na kunyonga au anamkunjia kwenye gunia mzima mzima. ukisikia sauti ya mfugo kuomba msaada ukiwa usingizini, unakurupuka kama umekoswa koswa na risasi. lini utakumbuka kombati na boots!!
Pole sana mkuu!

Kwa ushauri kwa sie tunaoishi mashambani lazima uwe na nguo na viatu vya tahadhari!

Sehemu kama hizo nunua boots za kijeshi na rain boots! Pia kuwa na combact au suruali ngumu!

Ziweke sehemu ambayo ni rahisi kuvaa fastaa linapotokea jambo ili ukisikia kokoro usitoke na ndala au sendo tena!

Vipi ungekuta mwizi na yapaswa umkimbize machakani? Ungemkimbiza na ndala? Au huyo nyoka angekugonga kama ungekuwa kwenye boots?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom