Jana nimeng'atwa na nyoka mguuni!

Jana nimeng'atwa na nyoka mguuni!

Habari

Waswahili wanasema hujafa hujaumbika, lakini pia wanasema usimdharau mtu....naam haya jana niliyathibitisha katika maisha yangu.

Nilifanikiwa kukamilisha kibanda pembeni ya mji ndipo ninapoishi na sina muda mrefu sana tangu nihamie hapo, kama ilivyo sehemu kama hizo nikaona nianzishe mifugo hivyo nikawa nao kadhaa.

Jana usiku nilisikia mbuzi na kuku wanajipiga piga katika mabanda yao hali ambayo si ya kawaida, kuangalia saa ni saa nane usiku nikahisi huenda ni mbwa ninaemfuga anawafanyia tabu hivyo nikatoka na kwenda kucheki, kufika nikakuta mlango wao umefunga kama kawaida na mbwa wala hana mishe nao yupo pembeni kabisa akidumisha ulinzi.

Nikazunguka nyuma ya banda eneo lenye wavu na huko kuna giza taa haifiki, mara ghafla kufumba na kufumbua kuna kitu kikanipiga mguuni! Nikamulika tochi ya simu nakuta kidole cha mguu kinavuja damu nyeusi na kwa mbali nyoka mkubwa akitoweka!

Awali niliishiwa nguvu kutokana na presha ya tukio hilo na kuwaza kuwa hiki ni kifo lakini nikaamsha wenzangu (walikuwa wanawake na watoto tu kwani kulikuwa na shughuli za kifamilia mjini hivyo ninaoishi nao walikwenda huko) wakanipa ujasiri na wazo la kuufunga mguu ili sumu isipande.

Nilikwenda kwa jirani ambae ni mzee wa makamo mwenye familia yake, akaniambia mwanangu tuwahi hospital tusipoteze muda maana hatujui nyoka huyo limit ya kuua kulingana na sumu yake.

Niliendesha gari kama mwendawazimu saa tisa tukawa mbele ya geti la hospital, niliwahiwa kupigwa sindano ya kuondoa sumu maana hali yangu ilianza kuwa tete na kisha wakasafisha sehemu husika na kuyatoa meno, pia wameshangaa nimefikaje umbali wote huo kulinganisha na tatizo husika....nikapewa dawa kadhaa pia na kuruhusiwa. Nimeamka naendelea vema na nakanyaga kama kawaida Alhamdulillah.

Kwa nini nimesema hujafa hujaumbika? Kwa sababu mpaka usiku nakwenda kulala nilikuwa mzima wa afya hivyo sikujua kuwa linaweza kunitokea jambo la kuhatarisha uhai wangu usiku huo.

Kwa nini nimesema usimdharau mtu?
Kwa sababu wengi wanapokua na visenti, usafiri au kibanda chenye angalau katika eneo husika haswa wakiwa wageni, huwadharau wenyeji au hata kuchagua watu wa kujenga nao mazoea, tazama nimesaidiwa na mzee nilimchukulia kama baba tangu nahamia pale...mzee ambae hupata riziki zake kwa kutumia baiskeli na panga kufanikisha kubeba mizigo ya kuni porini na kwenda kuuza mjini.

Dunia si yetu hatujui siku wala saa

Sent using Jamii Forums mobile app

Mimi porini naogopa kukutana na simba au Nyoka!
 
Miaka mingi ya nyuma nilikuwa ninaishi maeneo ambayo sasa tunayaita 'uswahilini' lakini enzi zile tulikuwa tunasema 'kwa wenyeji' Hapo jirani yetu mzee mmoja wa kihaya alinunua nyumba akawa anaishi pamoja na familia yake.

Tabia zake zilikuwa akitoka kwenye biashara zake basi huenda msikitini na akitoka huko anarudi kwake hivyo hakuwa na maingiliano sana na wenyeji.

Mzee huyu alipewa majina mengi tu ambayo kwa kweli hayakuwa mazuri.
Bahati mbaya alifariki ghafla na baadhi ya jirani walikwenda msibani[ kwani naye alikuwa anafanya hivyo pia]. Ikatokea kuna bibi mmoja jirani ya nyumba ya marehemu alilia kama vile amefiwa na mwanawe na katika udadisi ikagundulika kuwa yule mzee alikuwa ndiye anamsaidia yule bibi pamoja na wajukuu zake ambao wote walifiwa na wazazi wao.

Kumbe marehemu ndiye aliyekuwa msaada wa hali na mali kwa ile familia bila ya wengine kufahamu. Mwisho wa siku wengi tu jirani ilibidi wainamishe vichwa vyao kwa kujuta kumnanga marehemu kuwa anaringa sana.'TENDA WEMA NENDA ZAKO'

Majirani huwa wana tabia ya kukupangia uishije na kukuzoea usipokuwa na msimamo utajutraaa
 
Vipi maumivu yake?na kwanin ulimuacha aende ulitakiwa umuue
Katika kitu cha kwanza unashauriwa ukiumwa na nyoka ni kuacha kufanya purukushani zozote zitakazoongeza mzunguko wa damu. Kama unavyojua mwili unapochangamka ndo mapigo ya moyo yanaongezeka na damu inakimbia zaidi hivyo unaongeza ufanisi wa sumu kusambaa.

So unapaswa kuwa calm

Usianze kumtafuta japokua kama inawezekana kumuua papo kwa papo ni vizuri na umbebe uende nae hospital ili wajue ni specie gani

Pia usikimbie kutafuta msaada tembea tu huku ukiwa ushafunga juu ya eneo ulipoumwa
 
Yaaani umezungukaaa kumtafuta boya aliyekua anakandia wenye magari hahahaaa

Nimekuona sehemu Uzi flani asubuhi hii unasema zamani gari ilikua ishu humu ndani
Nakuambia Yaan ilibidi mtu akielezea kuwa ana gari anaomba msamaha kwa chini kuwa samahani kwa kuwauzi kutaja gari

Yaan uzi ulikuwa unabadilika unachafuka muulize RRONDO
 
Habari

Waswahili wanasema hujafa hujaumbika, lakini pia wanasema usimdharau mtu....naam haya jana niliyathibitisha katika maisha yangu.

Nilifanikiwa kukamilisha kibanda pembeni ya mji ndipo ninapoishi na sina muda mrefu sana tangu nihamie hapo, kama ilivyo sehemu kama hizo nikaona nianzishe mifugo hivyo nikawa nao kadhaa.

Jana usiku nilisikia mbuzi na kuku wanajipiga piga katika mabanda yao hali ambayo si ya kawaida, kuangalia saa ni saa nane usiku nikahisi huenda ni mbwa ninaemfuga anawafanyia tabu hivyo nikatoka na kwenda kucheki, kufika nikakuta mlango wao umefunga kama kawaida na mbwa wala hana mishe nao yupo pembeni kabisa akidumisha ulinzi.

Nikazunguka nyuma ya banda eneo lenye wavu na huko kuna giza taa haifiki, mara ghafla kufumba na kufumbua kuna kitu kikanipiga mguuni! Nikamulika tochi ya simu nakuta kidole cha mguu kinavuja damu nyeusi na kwa mbali nyoka mkubwa akitoweka!

Awali niliishiwa nguvu kutokana na presha ya tukio hilo na kuwaza kuwa hiki ni kifo lakini nikaamsha wenzangu (walikuwa wanawake na watoto tu kwani kulikuwa na shughuli za kifamilia mjini hivyo ninaoishi nao walikwenda huko) wakanipa ujasiri na wazo la kuufunga mguu ili sumu isipande.

Nilikwenda kwa jirani ambae ni mzee wa makamo mwenye familia yake, akaniambia mwanangu tuwahi hospital tusipoteze muda maana hatujui nyoka huyo limit ya kuua kulingana na sumu yake.

Niliendesha gari kama mwendawazimu saa tisa tukawa mbele ya geti la hospital, niliwahiwa kupigwa sindano ya kuondoa sumu maana hali yangu ilianza kuwa tete na kisha wakasafisha sehemu husika na kuyatoa meno, pia wameshangaa nimefikaje umbali wote huo kulinganisha na tatizo husika....nikapewa dawa kadhaa pia na kuruhusiwa. Nimeamka naendelea vema na nakanyaga kama kawaida Alhamdulillah.

Kwa nini nimesema hujafa hujaumbika? Kwa sababu mpaka usiku nakwenda kulala nilikuwa mzima wa afya hivyo sikujua kuwa linaweza kunitokea jambo la kuhatarisha uhai wangu usiku huo.

Kwa nini nimesema usimdharau mtu?
Kwa sababu wengi wanapokua na visenti, usafiri au kibanda chenye angalau katika eneo husika haswa wakiwa wageni, huwadharau wenyeji au hata kuchagua watu wa kujenga nao mazoea, tazama nimesaidiwa na mzee nilimchukulia kama baba tangu nahamia pale...mzee ambae hupata riziki zake kwa kutumia baiskeli na panga kufanikisha kubeba mizigo ya kuni porini na kwenda kuuza mjini.

Dunia si yetu hatujui siku wala saa

Sent using Jamii Forums mobile app
Pole mkuu wa mvumbo. Na umshukuru mungu kupatiwa tuni ya uhai ila jitahidi kama unenshi maeneo hatarini kama hao uwe na vitu vidogo vya FIRST AID iwe vya kienyeji au vya kizungu.Ajali nyegine za kulengwa kwa majaribio
 
Umemaliza yote kiongozi sina la kuongezea

Sent from my Infinix X680 using JamiiForums mobile app
 
Pole sana kaka, mimi leo (saa hii tu) nimeua nyoka wa size tu. Nimeingia msalani ila nikiwa natoka ndio namwona corner karibu na basin ya maji, basi nikaruka high jump ingine hatari aisee mpaka nje ya choo. Faster nikatafuta gogo na nikacheza ka mimi (nikiwa makini na uwoga pia) Hawa wanyama nikiwaskia /kuwaona huwa sina amani mpaka nihakikishe amekufa. Hadi sahi kiroho chanidunda tu nikifikiria ka singekuwepo mimi ingekuwaje na home huwa kuna watoto wa shule huja jioni.
 
Nyika aina gani Kama unaweza tupia picha
 
Hatari sana.
 
Umenigusa sana kwa kumthamini huyo mzee kama ulivyosema wengi huwa tunawadharau wenyeji wetu hasa majirani kwa sababu ni masikin, hii haifai hata kidogo, tafuta muda piga nao story utakuta kuna mengi utajifunza toka kwao hasa katika eneo unaloishi hata mbinu za dawa za miti shamba
Usimdharau sababu ni masikin wapende na waonyeshe kuwaheshimu hakika hutopoteza bali utajenga na kujifunza
 
Sahihi kabisa.
 
Back
Top Bottom