Jana gari langu limekufa kisa Diesel ya Big Bon - Serikali iko wapi ?

Lunyungu

JF-Expert Member
Aug 7, 2006
8,873
1,890
Juzi nilipata ajali mbaya sana kwa gari langu kuua injini baada ya kununua mafuta pale Big Bon Kariakoo yakiwa ni mchanganyiko wa mafuta ya Taa na Diesel .Nikakumbuka siku Mramba alivyo fanyiziwa kama yaliyo nikuta moto uliwaka lakini hadi sasa sijajua madai ama kesi ile imeishia wapi .

TRA na TBS sina hakika kama wako makini kiasi gani ama ndiyo mambo ya biashara za wakubwa .Baada ya gari langu kufa basi nilifika mahali nikawa nina tafuta spare na ufundi ndipo akatokea mwananchi mmoja akasema Big Bon na na visima kibao vya Waarabu na wahindi hununua tanker 2 za Diesel na kuongeza bna tanker moja ya mafuta ya taa na kuyachanganya na kuuza bei cheap .

Wanasema hii ni channel nzito ambayo wakubwa serikalini na hata ndani ya CCM ndiyo mradi wao maana ndiko ziliko posho zao .

Mnyetishaji anasema kwa mfano Big Bon huchukua mafuta toka bandarini na kuyapeleka pale mbagala huko huchanganywa na kuanza kusambazwa .

Mnyetishaji anasema TBS na TRA wanayajua haya na huzimwa kwa donge nono na wakibisha basi wakubwa huingilia kwa kupiga simu moja tu .

Haya wenye magari na weney visima hii ndiyo habari na ukweli uko nje nje .Tunaomba majibu toka TBS na TRA ama kwa wale wote wanao husika na mambo haya tujue kisa cha kuachia mafuta kuchanganywa na mafuta ya taa .
 
Mafisadi Wenye Utanzania Wenye Asili Ya Bara Jingine Ndo Wanaoimaliza Tanzania....!
 
Linyungu
Kulalamika kwingine bwana
Mchukue mkuu wa polisi nenda mkanunue hayo mafuta myapeleke TBS .Uharifu uko wazi tunapiga kelele kwenye screen huo si uwajibikaji wa kila mwananchi.
 
..kama unajipenda na huendekezi ubahili au kubana sana matumizi,usiweke mafuta katika vituo vyenye majina ya ajabu ajabu!

..bp,oryx na total zipo! big bon ndio msela gani huyo?
 
La ajabu Big Bon ndo kituo kinachoongoza tanzania kwa kweweka mafuta kwenye magari mengi - ulio haribikiwa ni wewe tu!

Hapa nafikiri gari lako lilikua na kasoro tayari!

Pole lakini kwa kuharibikiwa - ila tafuta mchawi mwengine!
 
..we paka shume, hizi data umetoa wapi? au una maana oilcom?

..halafu mambo ya kuchanganya mafuta au mafuta kuwa na maji yamekuwapo sana. madereva daladala na taxi wanalifahamu hili vizuri.
 
sisi wote tunajaza magari yetu Big Bon kwa miaka mingi na hatujawahi kupata tatizo hilo na mafuta hayasababishi injini kunock hilo ni tatizo la oil iliyonunua huko mitaani, na huyo fundi aliyekuambia gari imenock kwasababu ya mafuta ujue hujampa hela yake yakufunga engine, ndio maana kasahau kufunga ringi namba 4 ya piston na gari kunock.

MTEJA MKUBWA WA BIG BON
 
Yaani wewe kweli huna sera magari mangapi yanajaza big bon na hayajanock tafuta mchawi kwengine acha ujinga

mkereketwa wa TRA & CCM
 
La ajabu Big Bon ndo kituo kinachoongoza tanzania kwa kweweka mafuta kwenye magari mengi - ulio haribikiwa ni wewe tu!

Hapa nafikiri gari lako lilikua na kasoro tayari!

Pole lakini kwa kuharibikiwa - ila tafuta mchawi mwengine!

Mitanzania Bwana BIgborn anavituo vingapi zaidi Kariakoo na Mbagala? By theway depo yake ya kuchakachu ipo pale mbagala.
 
kama gari analotumia Rais wako liliwekewa diesel iliyochakachuliwa kule moshi na gari zikazimika....hao TRA NA TBS hawakuchukua hatua zozote, sembuse gari lako!!
 
Mimi siku hizi nikinunua mafuta nadai risti ili kama injini ikileta shida nawapeleka EWURA ingawa nao huenda wakawa mameshachakachuliwa.
 
Linyungu
Kulalamika kwingine bwana
Mchukue mkuu wa polisi nenda mkanunue hayo mafuta myapeleke TBS .Uharifu uko wazi tunapiga kelele kwenye screen huo si uwajibikaji wa kila mwananchi.

Mkuu vipi umesahau kuwa polisi na mabosi wao wamewekwa mifukoni na wafanyabiashara, kuwafuata ni sawa na kuwapelekea dili. Usipoteze muda na polisi wewe kama una madai au issue nzito kamata mwanasheria, kumbuka wengi wao hawapendi kesi, wakipigwa kusudio la kupelekwa mahakamani watakutafuta wenyewe.
 
Ukiona kituo cha mafuta cha bei poa na jamaa wa Taxi na daladala hawanunui mafuta kwenye hicho kituo hapo jua ni kimeo.
 
kwa hawa bigbon wanaowatetea sijui wanatumia kigezo gani kwa hawa jamaa ni wachakachuaji kweli mpaka kwenye gas nimenunua gas siku moja palikuwa na msongamano wa magari so wakati naangaika mlinizi akaja akachukua mtungi na pesa akaniletea mtungi akaweka kwenye gari uku naona kufika om washa gas wapi aiwaki kuangalia vizuri inatoa maji kurudi kesho yake wanaikagua jibu la kunipa akuna na alopokeaa pesa anakumbuka nikawakomalia walipo ona nakomaa wakanidain risiti nikawaeleza ilivyokuwa na alopokea pesa anakumbuka wakanipeleka kwa boss wao wakagoma kunibadilishia mpaka ni nunue tena wezi na wachakachuaji acheni kuwatetea
 
Mimi nimeazimia kunywesha mafuta gari langu pale Victoria Petrol Station. Mafuta safi kabisa. Labda niwe na dharura angalau nikimbilie BP. Ila kama mkuu mmoja alivyosema hapo juu oil ndo inaweza kusababisha kuharibika kwa injini ukilinganisha na mafuta. Kwahiyo hakikisha unaweka oil yenye ubora kwa ajili ya ubora wa injini yako.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom