Je, ni muda gani masega ya gari yako yanakwisha ubora na kuhitaji kubadilishwa?

geranteeh

JF-Expert Member
May 21, 2015
266
618
Heri ya siku njema ya Mwanzo wa wiki wakuu. Leo nimekuja na somo ambalo ni nadra sana kulipata. Nasema ni nadra sababu watu wemgi huwa na dhana kwamba gari yangu ikiwa na masega basi kama hayajaibiwa basi hayatakwisha ubora milele. Kiufupi hakuna kifaa cha gari yako ambacho kitakaa milele yani usipohitaji badilisha hiki basi utabadilisha kile.. Ndiyo na hii inatokana na mazingira unatumia gari yako.

Ni nini na yana kazi gani haya masega (catalyst converter)?
Matokeo ya ufanyaji kazi wa mashine ya gari yako hakika ni uchafuzi mkubwa wa mazingira kwani hewa inayotoka kutokana na ufamyaji kazi wake ni hewa chafu ambayo si salama kwa mazingira na endapo ingekuwa imeachwa bila kuwepo kwa masega basi kungekua na mabadiliko makubwa sana ya tabia nchi ambayo yamesababishwa na uchafuzi wa mazingira... Nadhani mwalimu wako wa geography alifanya kazi kubwa sana kukuelewesha umuhimu wake kama hukumsikiliza naomba mm msamaha.

Uendeshaji wa engine ya gari yako huwa inatoa hewa chafu mbalimbali kama vile Carbon dioxide, Dinitrogen na maji hizi tatu ni asilimia 78 ya uchafu wote unaotolewa katika gari yako ambao kiufupi si hatari au kwa kizungu ni harmless.

Hata hivo hata engine ya gari yako iwe mpya kutoka kiwandani bado kuna hewa chafu ambazo ni hatari zaidi kwa mazingira na hizi ndizo ambazo zimelengwa ili kuzidhibiti kama vile hydrocarbon na Nitrous oxide.

Masega yanafanyaje kazi?
Kazi kubwa ya masega ni kubadilisha dutu hizi za toxic kuwa less harmful compounds kama vile maji au carbon dioxide yani kiufupi inageuza kuwa nyoka mkali na kuwa joka la kibisa hizi compounds kwa lugha ya mtaani na inafanya hivi kabla ya kuachia kwenye sehem zinapotokea na ndiyo maana kuna time kweny bomba la moshi unakuta kuna maji kidogo yanatoka so ikiwa hivo usishangae ni moja ya sababu japo kuna sababu nyinginezo ikiwemo za hatari endapo wingi wa maji utakua mkubwa (Hiki ni somo la siku nyingine). Kiufupi ni kwamba masega ya gari yako yana uwezo wa kupunguza kwa 90% hizi dutu hatari kwa mazingira kuwa less harmfull na kwa gari za kisasa zaidi imeboreshwa mpaka 99%.

Je Masega ya gari yako yanaweza kuharibika au kupoteza ubora?
Jibu ni yes tena big yes japo watu wengi hawajui hili kwamba hata ujitahidi vipi kuyalinda still yatapoteza ubora na hii ni kwasababu mbalimbali ambazo pengine ulikua hujui.

Sababu kubwa ya kufeli kwa Masega (Catalyst converter) ni kuharibika kwa sehemu za ndani muhimu za haya masega kama vile catalyst coating. Ili nisikuchanganye na vingereza vingi kiufupi hizo sehemu za ndani za masega huaribika kutokana na dutu ambazo hazitakiwi kufika kwenye hayo masega kama vile Coolant, Oil na mafuta ambayo hayajachomwa na hii hupelekea catalyst converter yako ku overheat, najua utajiuliza hivo vyote vinafikaje huko kwenye masega?

Kiufupi kama engine ya gari yako inafanya kazi chini ya kiwango ina misfire kama zote basi lazima ipeleke shinikizo kwenye catalyst converter na hapo ndipo unapokula masega yako taratiiiiiiibu. Kumbuka masega ya gari yako yameundwa kukaa miaka mingi na kufeli au kuharibika ni mara chache sana endapo utazingatia hizi sababu zinazosababisha ifeli.

Sababu nyinginezo zinazopunguza uhai wa masega ya gari yako ni pamoja na kuwa exposed na chumvi pamoja na kemikali mbalimbali.

Lakini pia endapo umajimaji utaingia kwenye masega ya gari yako hupelekea kutu kutengenezeka na then kupoteza ubora

Masega hupungua ubora kutokana na mstuko wa either ajali au matuta (wazee wa kufukia mashimo)

Sababu ya Mwisho ni Overheating endapo joto litazidi kupita kiasi na kupelekea masega kuyeyuka.

Je Umri Sahihi wa Masega ya gari yako ni upi?
Hapa ndipo wengi mlikua mnapasubiria bila shaka kwani kila chenye mwanzo hakikosi mwisho
Kiufupi umri wa masega ya gari yako unategemea na aina ya gari yako na ubora wa masega yaliyowekwa kwenye gari yako.

Hapa ndo tunapotakiwa kukubali ukweli halisi kati ya gari za europe na japan YES katika nchi za europ wako makini sana na utunzaji wa mazingira na ndo maana wanafatilia sana suala la masega na hali hii hupelekea hata ubora wa masega yanayowekwa kwenye magari yao kuwa mkubwa sana na wana wataalamu kabisa wanaodili na masega tofauti na gari za japan ambazo wengi huwa tunazitumia hivo basi umri wa masega kuisha ni kwanzia km 80,000 mpaka 240000 km au zaidi hii ni according to wataalamu.

Na tukiipeleka kwenye umri hapa tunapata around miaka kumi.

Nitajuaje kama gari yangu masega yamekwisha muda wake?

Kikubwa huwa ni kuwaka kwa taa ya check engine na kwa gari nyingi za kisasa kama kukiwa na shida ya masega basi taa hii haizimi hata ukienda kuizima kwa mashine itazima then itarudi tu mpaka urekebishe tatizo.

Gari kukosa nguvu ambapo masega ya gari yako yata affect air flow ya kwenye exhaust ya gari yako na kupelekea ufanyaji kazi wa engine yako kuwa mbaya na hali hii huleta hata unywaji wa mafuta kuongezeka.

Mlio wa gari kubadilika na kusikia mlio wa tofauti chini ya gari yako na pia harufu ambayo si ya kawaida utaisikia pindi gari ikiwa imesimama kwani hapo ndo utaweza hisi harufu ya tofauti kumbuka lile somo la hewa mbalimbali hapo juu.

Kama unahisi gari yako ina shida ya masega unaweza nichek kwa ushauri na pia kupata masega mapya au original. Ntakuja na somo la ipi tofauti ya masega mapya na masega original wakuu. Muwe na siku njema.



IMG_20230713_095216_529.jpg
 
Back
Top Bottom