JamiiForums Usiku wa manane

JamiiForums Usiku wa manane

Hello. I am looking for HR and Admin Officer (Male) to work in Dar Es Salaam. Age not above 40yrs, Experience 3 and above in Logistics or hospitality nitumie inbox CV🙏.+255 689 727 999
 
SALESMAN (21 POSITIONS)

KEEWAY is inviting qualified, motivated, and results-oriented candidates to apply for the position of SALESMAN.

WORK LOCATIONS: Mkolani, Bariadi, Bunju, Korogwe, Moshi, Geita, Katoro, Kahanama, Singida, Nzega, Kasulu, Mbeya, Town, Makongolosi, Makambako, Masasi, Newala, Morogoro, Ifakara, Vikindu, Tarime and Ruangwa.

EXPECTED SALARY: TZS 300,000

HOW TO APPLY

Interested candidates should submit their updated CV to:

kwmhrdp@keewaytz.com

Subject: Application - Salesman
 
Habari , nina shida unitangazie nafasi za sales agents 300 from Dar, Arusha, Mbeya, Njombe, Kahama, Morogoro na Mwanza ( 100 kila mkoa) watume CV ONLY 0766014480 DON’T CALL ni Fintech Company Located Sky City Mall and payments mode :Based on Commission
 
Rais wa 26 wa Marekani 🇺🇸 Theodore Roosevelt aliwahi kusema kuwa "Kujilinganisha ni kujiibia furaha"

-Hii ina maana kuwa.... Unapojilinganisha na watu wengine kila wakati, unapoteza furaha na kuanza kuona mafanikio yako ni madogo na kutothamini kile ulichonacho.

-Siku zote kumbuka jambo hili muhimu kuwa mafanikio yoyote uliyonayo leo, iwe ni katika elimu,fedha, ushawishi, biashara n.k. lazima ukubali kwamba kuna mtu yuko mahali anakuzidi.

-Hii itakupa amani na utulivu wa akili kuendelea kupambania malengo yako bila presha ya kujiona kuwa umechelewa sana.

Leo, acha kujilinganisha na wengine,thamini hatua ulizopiga na endelea kujifunza.Kila mtu ana safari yake ya mafanikio,jitahidi kuwa bora kuliko ulivyokuwa jana.
-The Power Is Within You-
💥🫵


(Yona Morice Yona)
 
Benjamin Franklin,mwanasayansi, mvumbuzi na mwanadiplomasia nguli nchini Marekani aliwahi kusema kuwa "Watu wengi sana wanakufa wakiwa na miaka 25 lakini huwa wanazikwa wakiwa na miaka 75"😥

-Hii maana yake ni kuwa,kuna watu wengi duniani ambao baada ya kufikisha miaka 25+ na kuendelea huwa wanakata tamaa na kupoteza kabisa matumaini kuhusiana na kutimiza kusudi la maisha yao.

Baada ya hapo huwa wanabaki wakiishi kwa mazoea tu huku miaka ikizidi kwenda,hatimae huwa wanakuwa wazee "75+" hadi wanaondoka duniani bila kuziishi ndoto zao🤷

-Wewe hautakiwi kuwa mmoja wao,leo jiulize ni kusudi au ndoto gani ambayo unataka kuitimiza katika maisha kisha uchukue hatua,Usichelewe anza leo.
-The Power Is Within You-
💥 🫵


(Yona Morice Yona)
 
Mark Twain, mtaalamu wa mambo ya mafanikio binafsi aliwahi kusema kuwa.

"Miaka 20 baada ya leo utajutia na kujilaumu sana kwa mambo ambayo hukuyafanya"

-Hii ina maana kuwa,kiwango cha maamuzi muhimu unayoyafanya leo ndio kitajulisha kiwango cha mafanikio utakayokuwa nayo miaka ijayo⌚

-Inawezekana kuna fursa au maamuzi muhimu ambayo unatamani kuyachukua.

-Lakini kila wakati unasita una ghairisha unaona bado una muda na wakati mwingine unasema utaanza kesho.

-Ili usiwe miongoni mwa watu watakaojutia badae unatakiwa kuanza leo kwasababu kuanza sio HISIA ni MAAMUZI...✍️
-The Power Is Within You-
💥🫵

(Yona Morice Yona)
 
Una uwezo mkubwa sana ndani yako ambao bado haujawahi kuutumia:📌

Utafiti uliofanywa na Chuo Kikuu cha Stanford mwaka 2019 ulibaini kuwa watu wenye imani kubwa juu ya uwezo wao binafsi "self-efficacy"

-Wana uwezekano mkubwa mara tatu ya kuvuka changamoto ngumu na kufikia malengo yao ikilinganishwa na wale wanaojiona dhaifu.🤷

-Utafiti huo ulionyesha kuwa pale mtu anapoamini kuwa anaweza, ubongo wake huanza kutengeneza suluhisho badala ya visingizio na hapo ndipo nguvu ya ndani inapoamka.

-Kwahiyo, bila kujali umechoka kiasi gani au umekataliwa mara ngapi, kumbuka kuwa wewe ni mwenye nguvu na unao uwezo mkubwa ndani yako kuliko unavyodhani.

-Leo anza tena, inuka tena na usonge mbele, kwa sababu ndani yako kuna uwezo ambao bado dunia haijauona.
-The Power Is Within You-
🫵 ✨

(Yona Morice Yona)
 
Hasira itakutenga na watu muhimu:
-Watu wengi wamepoteza marafiki,fursa, mahusiano,ndoa,kazi n.k kwa sababu ya kushindwa kuzitawala hasira zao.

-Ni herufi moja tu ndio inaweka utofauti kati ya neno "HASIRA" na "HASARA"

-Hivyo ni muhimu sana kuwa makini na kujifunza kuwa kimya unapokuwa na hasira.😡

-Utafiti kutoka chuo kikuu cha Harvard University pamoja na maudhui ya mwanasaikolojia DANIEL GOLEMAN..

-Yanaonyesha kuwa watu wenye uwezo wa kuthibiti hisia zao za hasira hujenga mahusiano bora na kupata mafanikio zaidi katika maisha🎉

Hasira inaweza kukufanya ukose fursa muhimu😰 Mbaya zaidi ni kuwa dunia inawatu wengi wanaokera na kukukwaza.

Kuliko wanaokutia moyo, usipokuwa makini kwenye kuzi "control" hisia zako utajikuta unakosana na watu kila wakati.

Leo bila kujali umekasirishwa kwa kiasi gani,chagua utulivu kwanza ili usiwe miongoni mwa watu wanaojuta.

-Kwa kuharibu mustakabali wa maisha yao kwa kwasababu ya kushindwa kuzuia hasira zao.

Kila binadamu ana hisia za hasira ila swali la msingi ni Je wewe unazitawala vipi hisia zako?...🤷
-Mungu akusaidie badala ya hasira uchague utulivu na hekima.

Kama umeipenda makala hii weka reaction kisha mtumie mtu mmoja unayemthamini ili tuendelee kujifunza zaidi 📚✨
-The Power Is Within You-
✨ 🫵


(Yona Morice Yona)
 
Back
Top Bottom