Pamoja na kuwa na mke bora kabisa,mwamba katuangusha sana wanaume
Kwanza niwape kongole wanawake wa Kenya,nimeona video nyingi sana wao hawana baya katika kumsapoti mwanaume wake
Wanaweza Lipa kodi za nyumba na kuhakikisha mazaga zaga yanapatikana hapo nyumbani kifupi wapo loaded
Mchongo upo hivi, mwamba yupo na manzi yake for 5 yrs,na wamejaaliwa kuwa na watoto wawili
Huyu mwanamke amegombana na wazazi wake kwasababu ya huyu mwanaume,kwasababu kama unavyojua in Kenya, ukabila ndio kila kitu, Wakalenjini hawataki kuchanganya na kabila lingine
Sasa wazazi wa mwanamke hawakutaka mahausiano yao coz mwamba sio mkalenjini,kwahiyo kwakuwa baby girl alimuelewa mwamba akaona isiwe tabu kama mbwai mbwai
Pamoja na mapenzi yote kutoka kwa mke,lakini upande wa mwanaume kuna dark story,yes dark story
Zikakutwa meseji kutoka kwa ex wa mwamba ,akimwambia huyo mwamba kwamba inabidi amsomeshe mtoto wao la sivyo atampeleka yule mtoi (mtoto) pale kwa mkewe Waka mlee
Mwamba kwanza alikaza lakini mikwala ilipozidi ikabidi alegeze nati,kama haitoshi huyo ex hataki mtoi wale asome public school,pamoja na mwamba kulalamika kwamba private ni ghali lakini wanasema waswahili hakuna mkate mgumu mbele ya chai
Mwisho wa siku ex alishinda na dogo kwenda International school
Lakini kibaya zaidi ni kwamba wazazi hawa walipokuwa wanakutana kwa ajili ya mwamba kumuona mtoto,kukazuka zile mambo za kumisiana,so kuna text zikionyesha wakiambiana kuwa wamemisiana na kupeana location
So mwisho wa siku huyu mke akaja kuujua ukweli kupitia hizo text
Hapo mke ndio akaanza kufungua code,kwamba yeye ndio humnunulia nguo jamaa,kulisha familia,lakini jamaa kila siku anasema hajalipwa hela huko kwa job
So mke ndio akahoji,so unasema huna hela kumbe unalipia mtoto international school?
View: https://youtu.be/E-7CghCLda0?si=7W9PKlTW17CCAbX9
Mwisho wa siku mke akamwambia mwamba asije tena nyumbani kwa mke,na wasijuane tena,this time mwanaume akawa ana kazi ya kumbembeleza boss lady arudishe mapenzi na kumsamehe huyo.mwamba
Alamsiki!