ShesRise_1
JF-Expert Member
- Aug 21, 2025
- 17,287
- 40,946
00:45 don't worry
SawaHabari za weekend, wadau waaminifu wa uzi huu wa Usiku wa Manane!
Maana wengine mkiuona tu uzi umepandishwa hewani, mnachungulia kimya kimya, mnachapa lapa na kuondoka bila hata kuacha salamu. Lakini tupo pamoja sana, hata wale wa kusoma kimya kimya tunawaheshimu.
Je, wewe unaongea vipi?
Unaongea taratibu, kwa vituo na kwa utulivu? Au unaongea harakaharaka kama cherehani iliyokanyagiwa speed ya mwisho?
Ukweli ni kwamba, kuongea vizuri ni skill ambayo tunatakiwa kujifunza. Uongeaji wa harakaharaka, kama ule wa Ertugrul Bey, wakati mwingine unaweza kuwa changamoto katika mawasiliano.
Binafsi, mimi ni muhanga mkubwa wa kuongea harakaharaka. Kuna wakati maneno yanatoka mdomoni kwa kasi kuliko akili inavyoweza kuyapanga. Sasa imenibidi kuanza kujifunza kuongea taratibu, kwa kuweka vituo na kutoa nafasi kwa msikilizaji kuelewa ninachokisema.
Hili si jambo geni. Kuna mwandishi maarufu sana wa vitabu na mzungumzaji wa kimataifa, kwa bahati mbaya nimelisahau jina lake, ambaye amewahi kueleza kwamba pamoja na kuwa amezunguka nchi mbalimbali duniani akitoa semina, ilimbidi yeye mwenyewe kwenda kwenye semina maalumu ili kujifunza namna ya kuzungumza taratibu na kwa ufasaha.
Hapo ndipo tunapojifunza kwamba hata mtu anayejulikana kwa kuzungumza mbele ya maelfu ya watu bado anaweza kujifunza na kuboresha namna yake ya kuwasiliana.
Kwa hiyo, wewe na mimi tunaweza kuanza kujifunza kuongea taratibu, kidogo kidogo. 🗣️
Kuongea kwa utulivu kuna faida kadhaa:
🔹 Kwanza, kunakupa muda wa kutafakari kabla hujatoa maneno.
🔹 Pili, kunamsaidia msikilizaji kukuelewa vizuri zaidi.
🔹 Tatu, kunaweza kukufanya uonekane mwenye kujiamini katika mazungumzo yako.
🔹 Nne, kunakupa nafasi ya kusisitiza pointi muhimu badala ya maneno yote kutoka kwa kasi moja.
Lakini pia, kila kitu kina kiasi chake. Kuongea taratibu sana nako kunaweza kuchosha na hata kuboa.
Kwa mfano, ukimsikiliza Tundu Lissu akizungumza, wakati mwingine anaweka vituo vikubwa sana na mapumziko marefu kati ya sentensi. Unaweza kujikuta unasubiri kwa hamu ajue ataendelea lini na mazungumzo.
Kwa hiyo, point yangu ni hii: tafuta uwiano.
Usiongee kwa haraka sana mpaka watu waanze kukuomba urudie kila sentensi.
Wala usiongee taratibu sana mpaka wasikilizaji waanze kujiuliza kama mazungumzo yamesimama au bado yanaendelea.
Ongea kwa kasi ya wastani, weka vituo pale panapohitajika, tafakari kabla ya kujibu na hakikisha unampa msikilizaji nafasi ya kukuelewa.
Kwa kifupi, kuongea ni skill. Na kama skill nyingine yoyote, inaweza kujifunzwa na kuboreshwa. Kama wewe ni mtu wa kuongea harakaharaka, usijione umekwama hapo milele. Anza kidogo kidogo. Punguza speed. Weka vituo. Vuta pumzi. Sikiliza unavyoongea.
Mwisho wa siku, lengo si kuongea kwa haraka wala kwa taratibu sana. Lengo ni kuongea kwa namna ambayo ujumbe wako unafika vizuri kwa hadhira yako.
Alamsiki
How was your day my dearSawa
Siku yangu imekua nzurii😊How was your day my dear
Nafurahi kusikia hivyo mtu wangu,ni night nyingine tena kama kawa kama dawa, kuna habar gani pande hizoSiku yangu imekua nzurii😊
Pande hizi safiii nime play music huku naperuzi hapa kwa MelloNafurahi kusikia hivyo mtu wangu,ni night nyingine tena kama kawa kama dawa, kuna habar gani pande hizo
Waoo safi sana,ngoma gani hizo wasikiliza if you don't mind,ila usiniambie ni taarab😂😂Pande hizi safiii nime play music huku naperuzi hapa kwa Mello
Chief ulipote sana hapa mtaani kwetu usiku wa manane2201
Nipo nimerejea MkuuChief ulipote sana hapa mtaani kwetu usiku wa manane
Karibu sana,endelea amsha amsha kama kawa,tupa pamoja sanaNipo nimerejea Mkuu
Hapo kwenye taraabu nimecheka aiseeWaoo safi sana,ngoma gani hizo wasikiliza if you don't mind,ila usiniambie ni taarab😂😂