Mkuu,
Gentlemen_ kwanini umeamua kunifanyia hivi? Kwani nimewahi kukukosea nini hadi uamue kunivunjia heshima kiasi hiki?
Kwa muda wote huu nimesubiri nikidhani labda zilikuwa akili za pombe na usiku ule kwamba ukishakaa sawa utarudi hapa kuomba radhi lakini naona mpaka hivi sasa uko kimya!
Ulianzia kwenye jukwaa la michezo na kauli hizi, nikavumilia sikutaka ugomvi nikaondoka ktk ule uzi, nikaja hapa ambako pia ulinifuata…
Mbona sijawahi kuwa na mazoea na wewe acha tu kuwasiliana faragha, hata majukwaani sijawahi kuwa na ukaribu na wewe kiasi cha kupata ujasiri wa kusema haya.
Niseme ukweli, umeniumiza kwa kiasi kikubwa sana. Tambua wengine tuko huku na wapenzi wetu, kauli kama hizi zinaleta ukakasi katika mahusiano.
Hata wewe sidhani kama ungependezwa kuona mwanamke wako anaambiwa haya!
Ukishindwa kujiheshimu, waheshimu walioamua kujiheshimu!