JamiiForums Usiku wa manane

Mi ndo rapa naye flow bila beat, nayewapa verse tamu bila risiti/

Nahakikisha kila mmoja nimempa like, naenda kulala jamani nani nimkabidhi kijiti?/

Kwani huji kua usingizi kizungumkuti, yani unaota ndoto umeshika hela ukiamka huikuti/

Nawahi kulala, ili niepuke msala wa kugombea daladala/

Jumatatu kuna foleni jamani sio masihara, boss wangu mkali ukichelewa anakata mshahara/

Natamani kuacha kazi nifungue biashara, naona kama makuzi kufanya kazi na boss uchwara/

Watu8 ndani ya jf usiku wa manane, nina maongezi na wewe njoo tusemezane/

Hivi Chikwuemeka na chiqutitta kwanini wasioane?, majina yao yanafanana ndo sababu imenifanya niseme/


Oyaa mazee! mida basi na hii ndiyo post yangu ya mwisho kwa muda huu tukutane tena baadaye.....

Kila lakheri.....

It's Scars
 
Mkuu gudi naiti,tuonane kesho studio jioni maana naona unakipaji
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] dah! Umenifanya nicheke kwa sauti usiku huu lol!,

Haya bwana lala salama.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…