JamiiForums na Doris Foundation waungana kumpambania mtoto njiti (+picha)

Pascal_TZA

Member
Mar 25, 2014
17
36
Taasisi ya Kiraia ya JamiiForums pamoja na Taasisi ya Doris Mollel Foundation wameingia mkataba wa makubaliano wa kupeleka ujumbe sahihi kwa wananchi kuhusiana na watoto wanaoizaliwa kabla ya wakati (njiti).

Akizungumza katika hafla hiyo Mkurugenzi na Mhasisi wa Doris Mollel Foundation Doris Mollel amesema wao kama taasisi wanafanya kazi kushirikiana na Wizara ya Afya na tayari taarifa sahihi ambazo wanazipeleka katika jamii zimeshapitishwa na kitengo cha elimu ya afya kupitia Wizara ya Afya.

03c9d44b-f63a-4761-ac0f-d343bc2aa5ed-950x713.jpg

“Tunaamini kupitia JamiiForums tunaweza kuwafikia watu wengi wanaotumia mitandao ya kijamii na pia sisi ambao ni vijana tunaweza kuwasaidia watoto ambao wanazaliwa kabla ya wakati kwasababu kila mama anaweza kujifungua kabla ya wakati” Doris Mollel

Kwa upande wa Mkurugenzi Mtendaji wa asasi ya kiraia ya JamiiForums na Waratibu wa mtandao wa JamiiForums, Maxence Melo amesema JamiiForums ina uhakika wa kuwafikia wananchi wasiopungua Milioni 10 hivyo kuingia makubaliano na taasisi ya Doris Mollel Foundation wanaamini watawafikia wananchi wengi na kuelewa kuhusu mtoto kuzaliwa kabla ya wakati (Njiti).

ea4039ac-5964-4806-8fef-d36a30d86242-950x713.jpg

“Mtoto Njiti ilikuwa haifahamiki sana ila kupitia Dorine Molle Foundation imejitahidi kuhakikisha kwamba elimu ya Mtoto njiti inawafikia wengi na sisi tukaona kwamba kwa namna ya kipekee tumeona tuwape ushirikiano" Melo

"Hasa kwa mwezi huu wa Mwezi 11 na si kwa muda mfupi bali kwa muda wa takribani mwaka mmoja na kuhakikisha jamii inapata elimu ya kutosha kuhusu chanzo sahihi na taarifa sahihi” Melo

Nae Daktari bingwa wa magojwa ya watoto wachanga Dkt. Augustine Massawe ameshuhudia Asasi mbili za kiraia ya Doris Mollel Foundation pamoja na JamiiForums wakisaini makubaliano ya ushirikiano wenye lengo la kupaza sauti kwa jamii kufahamu kuhusiana na watoto wanaozaliwa kabla ya wakati yaani watoto njiti katika hafla iliyofanyika jijini Dar es salaam.

a4ea157a-2651-4428-b93a-1072ee636673-950x713.jpg

Aidha Dkt. Massawe amesema kuwa umri mdogo wa kubeba ujauzito na hali duni ya lishe kwa watanzania ni moja ya sababu ya watoto kuzaliwa njiti ambapo inakisiwa kila watoto kumi wanaozaliwa mmoja anakuwa amezaliwa kabla ya muda.

Daah hawa watoto huwa wanachangamoto Sana kuwakuza nilihangaika nao mapacha walizaliwa na 1kg kila mmoja then wakadrop mpaka 700g mmoja akafariki ndani ya siku moja akabaki mmoja.

Mungu mwema akasaidia uzito ulikuwa unaongezeka kwa speed ya kinyonga mtoto anafikisha miezi sita ana kiko 3.5 tu mpaka sasa dogo kakua miaka miwili na nusu ana kilo 9.5 tu.​
 
Aseee nmesisimka mwil pole kwa kumpoteza huyo mmoja na tumshkur Mungu kwa kumpigania huyo mwingne mkuu , Mungu ni mwema atukuzie akiwa na afya njema inshaallah.
 
Aseee nmesisimka mwil pole kwa kumpoteza huyo mmoja na tumshkur Mungu kwa kumpigania huyo mwingne mkuu , Mungu ni mwema atukuzie akiwa na afya njema inshaallah.
Ahsante, Mungu ni mwema yaani walikuwa na maumbo madogo kipindi nafika wodini Kama baba wa watoto naambiwa njoo uone watoto wako sikuamini.
Nikajisemea moyoni Kama Mungu kaamua hawa watoto wakue Basi watakuwa.​
 
Mtoto njiti anafahamika sema huku tunaita ndebile. Changamoto mno mwanzoni ila ukipita kipindi hicho kigumu na mwili ukakubali wanakua vizuri
 
Daah hawa watoto huwa wanachangamoto Sana kuwakuza nilihangaika nao mapacha walizaliwa na 1kg kila mmoja then wakadrop mpaka 700g mmoja akafariki ndani ya siku moja akabaki mmoja.
Mungu mwema akasaidia uzito ulikuwa unaongezeka kwa speed ya kinyonga mtoto anafikisha miezi sita ana kiko 3.5 tu mpaka sasa dogo kakua miaka miwili na nusu ana kilo 9.5 tu.​
Pole sana kwa kweli, na honey kwa kupigania nafasi yako kama baba
 
Back
Top Bottom