JamiiForums - Maboresho ya mwaka 2018

JamiiForums - Maboresho ya mwaka 2018

Mtuwekee na jinsi ya kubadili username
Kwakuwa bado tu wachache hapa jamvini hii ilisumbua kiasi chake watu kuigiliziana username. Mkuu atuwekee masharti kubadili kila baada ya Miezi 6 na Id zote ulizotumia zionekane kwenye profile yako kwa lazima. Tukiongezeka wapunguze masharti Labda.
"Nawaza tu"
Mimi na #Jf.
 
Hili huwa gumu; jaribio la kuruhusu watu kufanya hivi lilipekea watu kujiita “Mze Mwanakijiji” au “The Bos” na wengine watajiita “kulubulee”.

Tunafanya manually kubadili IDs ili pia kudhibiti wanaotaka kujiita majina yaliyo nje ya maadili

Nme-request mara kadhaa kwa Mods bila majibu na kama hivyo ndivyo nikuombe basi, E-mails zetu zijibiwe kwa wakati.
 
Pia ningependa kujua Jamii forum mnasaidia vp member wenu hasa inapotokea mtu amesahau neno lake la siri(password) wakati use name yake anaijua?maana adha hii imekumba watu wengi na kujikuta wanafungua account mpya!kwahiyo mtachukua hatua gani kwa hili ?
 
Wakuu,

Napenda kutoa taarifa mapema kuwa kutakuwa na maboresho kadhaa ili kutekeleza baadhi ya maombi ya wadau na kurekebisha kasoro kadhaa katika tovuti na app yetu.

Aidha, baada ya utafiti tulioufanya (tunawashukuru wote walioshiriki katika utafiti huu), kuna mengine yataendelea kuongezwa na kuboreshwa ndani ya siku 45 zijazo.

JF inayoonekana na kutumika sasa ilifanyiwa maboresho yaliyotokana na utafiti kwa wadau kati ya mwaka 2012 hadi 2016 ambapo Januari 2016 ilianza kutumika rasmi. Ni hii hii inayoboreshwa zaidi mwaka 2018 ili kuzidi kuifanya JF iwe rahisi kwa wengi kuitumia na kuifurahia.

Yanayotarajiwa:
1) Kuna ambao hawataona utofauti haraka kwani hatujacheza mbali na kilichozoeleka lakini wataona urahisi zaidi wa kuitumia JF
2) Kuna watakaoona baadhi ya vitu vimeondolewa - hivi vitatolewa sababu za kuondolewa kwake na kuoneshwa maboresho yaliyofanywa ili kutopoteza vitu hivyo
3) App: Waliokuwa wakikwama kwa mambo kadha wa kadha - yamerekebishwa kwa kadiri tulivyoweza
4) Mapendekezo ya wadau baada ya JF kufanyiwa maboresho haya yatafanyiwa kazi ndani ya siku hizo hizo 45

Tunawashukuru kwa uvumilivu wenu na kushiriki katika utafiti uliofanywa (nje ya mtandao) ili kuboresha jinsi mnavyoutumia mtandao huu.

Asante





Pamoja sana mkuu wetu!

Tuko nyuma yako.


Against all odds.
 
Back
Top Bottom