JamiiForums is the best social media in Tanzania

Bubu Msemaovyo

JF-Expert Member
May 9, 2007
3,833
2,790
Wana JF,

Hadi kufikia leo hii mimi binafsi nimeelimika sana tangu nilipojiunga na JamiiForums miaka kadhaa iliyopita.

Ni jukwaa ambalo wanachama wake ni kutoka kila fani nchini Tanzania. Kwa masuala yoyote ya Siasa, Jamii, Uchumi na Michezo; vyote vipo JF.

Ni media ambayo hufichua maovu, hukemea, na hutoa mwongozo kwa masuala ya kiuchunguzi.

JF inasomwa na watu wa kada zote toka ngazi za juu kabisa mpaka ile ya chini.

Ni fahari pale unapojiunga na JF unakunywa sikia wewe ni sehemu ya mwanachama utakao toa elimu kwa jamii.

JF ni media isiyo na woga kwani hutoa taarifa zake kwa uhuru chini ya mfumo mwanachama anaouchagua.

Hakuna Idara nyeti yoyote hapa Nchini hawapiti hapa JamiiForums kuangalia kinachoendelea yaani:-
1. Muhimili yote MITATU husoma JamiiForums.
2. Idara ya Usalama wa Taifa TISS husoma JamiiForums.
3. Wanafunzi ngazi zote Primary, Secondary, Vyuo Vikuu husoma JamiiForums.
4. Wananchi wa kawaida vijijini na mijini husoma JamiiForums.
5. Wanawake walio kwenye ndoa zenye migogoro husoma JamiiForums kujaribu kupata faraja ndani ya ndoa zao bàada ya kupata ushauri nasaha ndani ya JamiiForums.
6. Wanaume kwenye ndoa zenye migogoro hupata mafunzo ya nini wafanye ili kudumisha ndoa zao mafundisho hayo hutapata hapa JamiiForums
7. Watu wenye uraibu wa madawa ya kulevya hupata Rehah hapa JamiiForums
8. Elimu mbali mbali ya kisaikolojia yupo Mshana Jr. Hapahapa JamiiForums hutoa mafunzo hayo.
9. Ukitaka historia jinsi dunia hii ilivyoishi hadi leo hii njoo hapa JamiiForums utapata kila kitu.
10. Je unajisikia kuchoka na unataka kitu cha kujiburudisha ubongo wako njoo hapa JamiiForums nenda threads za jokes, Mahaba nk utaburudika kama sivyo ishitaki JamiiForums.
11. Unataka kujifunza masuala ya intelligence wala usihangaike njoo JamiiForums wapo walimu mahiri.
12. Unataka kuwa Wakili kama burudani yako kimaisha? Usiende kokote njoo JamiiForums wapo wanasheria mahiri.
13. Hakika hakuna lisilowezekana hapa JamiiForums kwani hata mimi Bubu Msemaovyo, nimeweza kuongea ingawa naongea kiovyo ovyo ujumbe unafika na pilipili yake.
14. Habari ya kesho kutwa inapatikana hapa JamiiForums.
15. Waongo, Wanafiki, Wakwepa kodi, Wahalifu mbalimbali hukemewa hapa na watoto wao, Baba zao, hapa JamiiForums.
16. Unataka kujua Nani yuko wapi alifanya nini wapi lini kwa nini? Usiache kusoma hapa JamiiForums, yote utapata.
17. JamiiForums ina wanachama dunia nzima kokote uendako yupo memba wa JamiiForums pembeni yako.
18. Hata FBI, CIA, MOSSAD, KGB NK Wote husoma JamiiForums, kama huamini jiulize kwanini Israel inagharimia kwa pesa nyingi sana programu ile inaitwa One Hour Translator unajua kwanini. Hahaha usiache kusoma JamiiForums.
19. Je una matatizo yoyote unataka suluhisho la uhakika, andika hapa JamiiForums wataalamu watakuja kukusaidia haraka sana.
20. Binadamu tumeumbwa na tabia tofauti nzuri, mbaya hapa JamiiForums sote hunyooka maana kuna kila aina ya wakufunzi na wataalamu wa saikolojia. Jiorodheshe kuwa mwanachama wa JamiiForums uwe wa kisasa zaidi kuliko juzi na jana.

Hivyo kama MEMBER endelea kutoa maoni yako kupitia jukwaa hili ili utoe mchango wako kwa ajili ya ustawi wa jamii.
 
Wana JF,

Hadi kufikia leo hii mimi binafsi nimeelimika sana tangu nilipojiunga na JamiiForums miaka kadhaa iliyopita.

Ni jukwaa ambalo wanachama wake ni kutoka kila fani nchini Tanzania. Kwa masuala yoyote ya Siasa, Jamii, Uchumi na Michezo; vyote vipo JF.

Ni media ambayo hufichua maovu, hukemea, na hutoa mwongozo kwa masuala ya kiuchunguzi.

JF inasomwa na watu wa kada zote toka ngazi za juu kabisa mpaka ile ya chini.

Ni fahari pale unapojiunga na JF unakunywa sikia wewe ni sehemu ya mwanachama utakao toa elimu kwa jamii.

JF ni media isiyo na woga kwani hutoa taarifa zake kwa uhuru chini ya mfumo mwanachama anaouchagua.

Hivyo kama MEMBER endelea kutoa maoni yako kupitia jukwaa hili ili utoe mchango wako kwa ajili ya ustawi wa jamii.
hakika jf ni University na imesheheni kozi za kila Aina
 
Back
Top Bottom