JamiiForums imesababisha Lowassa awe jobless? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JamiiForums imesababisha Lowassa awe jobless?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Samvulachole, Feb 8, 2008.

 1. S

  Samvulachole JF-Expert Member

  #1
  Feb 8, 2008
  Joined: Oct 22, 2006
  Messages: 410
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 45
  Kama sikosei ni sisi humu JAMBO FORUMS ndio tuliokuwa wa kwanza kuwa na habari ya MIKATABA ya ubadhirifu wa jamaa zake JK

  lakini kama kawaida wale walio karibu na watawala wakaanza kuleta stori za ohhh
  LETE EVIDENCE

  mara ohhh HAMISHA PELEKA KWENYE UDAKU

  mara ohh kiko wapi?

  In the end mashambulizi yaliponoga timu ya PR ya LOWASSA ikaingia kujibu mashambulizi na MKJJ akaawa anashambuliwa left and right

  Lakini in the end common sense ili prevail THREAD HAIKUHAMISHIWA KWENYE UDAKU kama baadhi ya waliokuwa wakiguswa walivyoptaka na watu waliendelea kuijadali na wenye nyeti zaidi walizileta

  Sasa hivi waandishi wa Habari si wa Tanzania tuu bali na wale waliopo nje ya inchi including BBC wamekuwa addicted na JF kwa kujua kuwa we just dont break the news lakini we also analyze them.

  Sasa huu mwaka tumeuanza vizuri na sasa hivi kampeni iwe ni kuondoa huu upuuzi wa eti Private life za wanasiasa wanaotutawala na we should have an all out atack on their public and private life na kama kuna mtu hapendi then ale bati tuu

  Sasa stay tuned kama waziri mkuu atakuwa Anna Makinda basi mjue kuwa tunaye to the end

  Na JK akija na baraza lake la mawaziri 60 basi mjue kuwa hiyo itakuwa ni kanyaboya
   
 2. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #2
  Feb 8, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,496
  Likes Received: 81,818
  Trophy Points: 280
  He has another opportunity to raise his credibility once again, he must be careful who he nominates as the next PM. If he nominates another fisadi then CCM won't give him another opportunity in 2010.
   
 3. M

  Mpanda Merikebu Senior Member

  #3
  Feb 8, 2008
  Joined: Dec 27, 2007
  Messages: 170
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Mkuu wa Samvula Chole,

  Nakubaliana na ulichosema kuhusu tulivyobarikiwa na Mola mwaka huu kwa kutujuza kile tunachopigania. Waama mwaka umeanza vema na sijui tumshukuru Bush ambaye Muungwana anataka kumuimpress? JF itaendelea kupigania haki za watanzania bila kujali itikadi ya siasa,kabila,dini au kitu kingine chochote.

  Kuhusu Lowassa, kwa kweli ningependa nipingane nawe (kwa heshima na taadhima)ukisema kuwa tumemsababisha awe jobless. Sisi hatujamfanya jobless, tulichofanya ni kukemea uozo wake. Ufisadi wake ulianza kabla hata JF haijaundwa na ndio maana Mwalimu akamsuta na kuwaambia wale wampendao kuwa wamwalike wakanywe nae chai. Kuwa jobless ni kujitakia mwenyewe kwa upande wake (Lowassa) kwani kama waziri mwandamizi, kada wa CCM na just as being a grown up, hakuhitaji kukumbushwa kuwa cheo ni dhamana. Naamini at some point in his life aliwahi kuapa "Nitajielimisha kadiri ya uwezo wangu na kuitumia elimu yangu kwa faida ya wote". Evidently amekuwa akitumia elimu yake kwa faida yake binafsi na washkaji zake. Kwa hilo mkuu, huyu bwana amejitakia haya yote, labda alifikiri sheria, kanuni na miongozo inamuexempt yeye.

  Two words for ENL: GOOD RIDDANCE!
   
 4. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #4
  Feb 8, 2008
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,867
  Likes Received: 115
  Trophy Points: 160
  EL ni mtu tajiri sana tangu mda mrefu akipokuwa AICC na pesa za maafa Ofisi waziri Mkuu early 1990s!

  Pale Arusha tu Leopard Tours ina magari zaidi ya 50 ya Watalii! Wacha raslimali za nyumba Arusha, Dar na Account nono za mabilioni ya shilingi!
   
 5. Azimio Jipya

  Azimio Jipya JF-Expert Member

  #5
  Feb 8, 2008
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 3,370
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  JF imesababisha EL awe anapostahili. Sio kumfanya Jobless!! And that is soooo GooooD

  Hivi ukimchukua "nyoka" mchimba madini mdogo wa mirerani aliyekuwa choka mbaya.... ukamfanya PM ghafla anauza na kuwa kwenye biashra nzuri kuliko nyoka wenzake alioowaacha mashimoni...huko mirerani..huoni hujawatendea haki wale uliowaacha..mashimoni...nao watakuwa wanatamani wawe PM ili nao wauze madini yao kirahisi na biashra zao ziwe nzuri kwani watakuwa exposed.....Swali huoni kila nyoka atatamani U_PM kwa sababu za kibiashara? Hivi ni kweli U_PM ni nafasi ya kupiganiwa kibiashara? Muulize EL ..aliutumia U-PM kwa misingi ya nini? Si biashara...but is it really U_PM ni nafasi ya Biashara? Jibu ni kuwa ..Sasa aendezake akafanye Biashara..and its right time ..arude kwa nyoka na wamachainga..awagawie mitaji ya mali yote aliyoipata tangu aanze kuwa kiongozi ndani ya hili Taifa labada itakuwa ni good recociliation na Mungu wake ...!! He has to be where he belongs...!!!
   
 6. M

  Maumivu Sr New Member

  #6
  Feb 8, 2008
  Joined: Feb 5, 2008
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  JF has been a blessing from God to Tanzanians. Hili halina ubishi kabisa.
  I have been a guest here only recently I decided to register myself as a member, to join hands with people wenye kutaka kuona watanzania wanasikilizwa by being their voices.
  Nimekuwa nikifwalia threads hapa JF kwa muda mrefu, I cant mention watu wote but with all due respect napenda kumpa pongezi Mzee MKJJ, bila kuwasahau wengine wote kwa mchango wao katika hili suala la kukemea ufisadi.
  Serikali ya JK ilikuwa ikiwafanya watanzania ni kama watoto wadogo wa kudanganywa na kutishwa, but JF has been bold to stand against such acts.
  Huu ni mwanzo mzuri kwa JK, the two years of his reign have been wasted, sasa ana miaka mitatu ya kutekeleza ahadi zako, I wish him all the best, and ajue JF itakuwepo kuhakikisha kwamba hatoki nje ya mstari.
  I salute you all wana JF, your excellencies.
   
 7. Nyangumi

  Nyangumi JF-Expert Member

  #7
  Feb 8, 2008
  Joined: Jan 4, 2007
  Messages: 508
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kama ni tajiri nini kilimfanya aendelee kuwaibia Watanzania ambao hawana hata baiskeli,pesa ya matibabu na mlo shida,wengine hata kulipa bili za umeme wameshindwa achilia mbali kuvuta umeme.Sisi tulidhani kwa utajiri wake angekuwa mwaminifu kwa Watanzania.
  Sasa kwa kuwa ni tajiri na tumehakikisha kuwa hawezi(Maana Nyerere alisema hafai hata ubalozi wa nyumba kumi) kututumikia,tumempa nafasi akaendeshe hayo magari yake.
   
 8. M

  Masatu JF-Expert Member

  #8
  Feb 8, 2008
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Lakuvunda halina ubani, kibarua kishaota manyasi tena tutasota nae kwenye adha ya foleni za barabara. Mwenzie Sumaye mwanzoni alikuwa anaona noma anajifunika kwa kujifanya anasoma gazeti uso hauonekani lakini aaah sasa hivi kishazoea tunapungiana mikono kama kawaida.

  Mzee Ngoyai welcome back!
   
 9. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #9
  Feb 9, 2008
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Kama na Masatu hili kaliona kweli alikuwa anafanya mabaya .Kipimo changu kwa issue za aina hii ni Masatu .
   
 10. M

  Mugo"The Great" JF-Expert Member

  #10
  Feb 9, 2008
  Joined: Oct 7, 2007
  Messages: 263
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Wanaofikiri JF inabahatisha habari wameumbuka. JF ni zaidi ya magazeti mengi tu; JF ni zaidi ya TV zinapasha habari kwa kuangalia ukali wa habari yenyewe. Hapa JF isse kwa issue hatua kwa hatua mpaka kinaeleweka. JF itaendelea kuwaandama Mafisadi wanaobaka uchumi wa Taifa. EL ni mmojawapo, naamini bado wengi sana wapo na JF izidi kumulika ndani na nje ya mipaka ya TZ, ili NURU ya MAISHA BORA na ya HAKI iwaangazie WADANGANYIKA.
   
 11. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #11
  Feb 9, 2008
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 863
  Trophy Points: 280
  Akajaze UB-40
   
 12. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #12
  Feb 9, 2008
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  " Kweli ni huzuni, kwa kuanguka kwake morani, kulipotokea pale bungeni, akasema moyoni, nafukuzwa kazi kwa uzushi, akalia kwa huzuni, hata mwisho akachoka, pale juu kizimbani akabwaga nyanga kwa huzuni"!
   
 13. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #13
  Feb 9, 2008
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Lowassa hana cha kuhurumiwa, kwanza anaondoka akiwa anatucheka na kutuona watanzania wajinga. Kujiuzulu kwake hakuna maana kuwa ndio kunasafisha madhambi yake. Toka mwanzo Baba wa taifa alisema huyu mtu hatufai, JK akajiona kichwa ngumu na sasa ameona. For sure JF imeplay part ya kumfikisha hapo alipo, lakini vilevile tukumbuke kuwa JF haikumtuma awe fisadi, sababu kubwa iliyomfikisha hapo alipo ni ufisadi, tabia yake ya udikteta, na kulifanya bunge kama kindergaten na kuwafanya watanzania wajinga.
  Tukumbuke kuwa mafisadi si masikini au wenye mapato kidogo wanaolazimika kupokea milungula kutokana na maisha magumu, ukiangalia kama yeye si maskini ni tajiri nguli, na nafasi ya U-PM ilikuwa tosha kabisa kumhakikishia masiha hadi anakufa hakuwa na sababu ya kuendelea na ufisadi baada ya kuwa PM, lakini ndio ametokea kuwa worst PM in Tanzanian history ever, ajabu sana kama ataishia kujiuzulu, inatakiwa afikishwe mahakamani.
   
 14. S

  Samvulachole JF-Expert Member

  #14
  Jul 30, 2016
  Joined: Oct 22, 2006
  Messages: 410
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 45
  mada ya long time, but mashiko yake yana nguvu hata sasa
   
 15. Copenhagen DN

  Copenhagen DN JF-Expert Member

  #15
  Jul 30, 2016
  Joined: Oct 5, 2014
  Messages: 5,047
  Likes Received: 6,197
  Trophy Points: 280
  dah BAK kumbe ulikuwa unashusha nondo humu toka zamani
   
 16. k

  kabombe JF-Expert Member

  #16
  Jul 30, 2016
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 15,579
  Likes Received: 8,519
  Trophy Points: 280
  BAK sijui umelishwa nini siku hizi mpaka kulikumbatia fisadi,wenzako nafsi ziliwasuta
   
 17. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #17
  Jul 30, 2016
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,483
  Likes Received: 5,567
  Trophy Points: 280
  Ndio maana watu walipobadili gia angani wengine tukaamua kushuka huko huko angani badala ya hii fedheha.
   
 18. zugimlole

  zugimlole JF-Expert Member

  #18
  Jul 30, 2016
  Joined: Aug 23, 2012
  Messages: 1,661
  Likes Received: 610
  Trophy Points: 280
  Maneno yanaishi bana
   
 19. Frey Cosseny

  Frey Cosseny JF-Expert Member

  #19
  Jul 30, 2016
  Joined: Feb 4, 2015
  Messages: 1,371
  Likes Received: 812
  Trophy Points: 280
  Duh sijui km Ben Sanane amesoma hapa?
   
 20. Countrywide

  Countrywide JF-Expert Member

  #20
  Jul 30, 2016
  Joined: Mar 2, 2015
  Messages: 2,514
  Likes Received: 1,839
  Trophy Points: 280
  Leo unakana lowasa sio fisadi
   
Loading...