JamiiForums ilivyonibadilisha maisha

JamiiForums ilivyonibadilisha maisha

inama

Senior Member
Joined
Oct 9, 2021
Posts
181
Reaction score
356
Habari wana JF

Mimi ni kijana muhitimu wa chuo katika fani ya ufundi umeme mwaka juzi mkoani Arusha.

Nakumbuka mwaka uliopita nilipita Uzi mmoja uhusuo maswala ya wahitimu. Ama kweli JF imebadilisha maisha yangu!

Katika ule Uzi kuna mtu mmoja aliquote kwa kushauri wahitimu katika kada ya umeme. Hatimaye nimefanyia ushauri wake kazi na mpaka sasa nina ofisi yangu ya umeme inayohusiana na maswala ya motor rewinding(kusuka motor) na pump za maji yenye mwaka mmoja na maisha yanasonga mbele.

Namshukuru sana aliyetoa ushauri, abarikiwe.
 
Jamii Forum ni platform bora sana. Tunatumia fake ID ila watu wapo real sana kwa baadhi ya mambo hasa yanayohusu maisha kiujumla.

Hongera sana mkuu.

Humu kuna vingi sana kama ukiwa mtu wa kuthubutu unaweza fanya makubwa sana.
 
Habari wana JF
Mimi nikijana muhitimu wa chuo katika fani ya ufundi umeme mwaka juzi mkoani Arusha,
Nakumbuka mwaka uliopita nilipita Uzi mmoja uhusua maswala ya wahitimu ,
Amakweli JF imebadilisha maisha yangu ,katika ule Uzi kunamtu mmoja aliquote kwakushauri wahitimu katika kada ya umeme . Hatimaye nimefanyia ushauri wake kazi na mpaka sasa ninaofisi yangu ya umeme inayohusiana na maswala ya motor rewinding(kusuka motor) na pump za maji yenye mwaka mmoja na maisha yanasonga mbele.
Namshukuru sana alietoa ushauri ubarikiwe.
Barikiwa kwa mrejesho huu
 
Kweli JF pazuri yaani unajipimia unapata Manzi, Elimu, maujanja na muda mwingine mnatibuana na Mods
Kweli JF raha.
 
Account yangu yamwanzo ilipigwa burn nilikua nataka nikatoe ushuhuda kwenye ule Uzi ilanimeshindwa kuupata nkamua kuuweka apa mrejesho wangu wana JF

Labda ambae atabahatika kuuona naomba anitag niwaletee
 
Jf ni kama bahari, chochote unapata hadi waganga wa kienyeji wapo.
 
Account yangu yamwanzo ilipigwa burn nilikua nataka nikatoe ushuhuda kwenye ule Uzi ilanimeshindwa kuupata nkamua kuuweka apa mrejesho wangu wana JF

Labda ambae atabahatika kuuona naomba anitag niwaletee
Eleza tu kwa kifupi jamaa alitoa ushauri gani na hatua ambazo wewe ulichukua.
 
Hii ndomirejesho tunayoitaka,unawatia moyo hata watoa ushauri kwamba kuna vijana walio seriousu.hongera
 
Back
Top Bottom