Kilichonishawishi kujiunga na JamiiForums (JF)

Kilichonishawishi kujiunga na JamiiForums (JF)

Jackpiano

JF-Expert Member
Joined
Apr 19, 2025
Posts
560
Reaction score
756
Kilichonishawishi Kujiunga na JamiiForums (JF)

Karibu miaka ya 2016 hadi 2017, kipindi hicho nilikuwa bado nipo shule Nyumbani nilikuwa naaminika kiasi cha kupewa simu kwa ajili ya mawasiliano—simu ya kawaida ya Itel, zile za zamani zenye operamini ndani yake. Simu hiyo ilikuwa na apps kama Facebook, Yahoo, na JamiiForums, na pia niliweza kudownload nyimbo kupitia waptrick.com pamoja na games za Java. Nilikua naipenda sana hiyo simu.

Katika kuperuzi simu ile, niliingia kwenye JamiiForums kwa mara ya kwanza. Nilikutana na majukwaa mbalimbali, lakini lile lililovuta hisia zangu zaidi lilikuwa JF Garage, kwa sababu tangu nikiwa mdogo nimekuwa na mapenzi ya dhati na magari. Nilivutiwa pia na majukwaa mengine ya kitaalamu, elimu, na maisha kwa ujumla.

Nakumbuka kuna mwanachama mmoja jina lake nali ifadhi ambaye michango yake ilinivutia sana. Ingawa sikuwa mwanachama wa JF kwa wakati huo, nilikuwa msomaji wa uzi hadi uzi—kwa kifupi nilikuwa "mwanachama wa mtaa".

Miaka ikaenda, lakini hamu yangu ya kusoma na kufuatilia mijadala ya JF haikupungua. Hivi karibuni, nilikuwa natafuta jambo fulani kwenye Google, nikaona uzi kutoka JF ukielezea mada hiyo kwa kina. Nilivyosoma ule uzi, nikajikuta nimeshawishika rasmi kujiunga na JamiiForums. Nikaamua download app yao na kuwa mwanachama halali. Na sasa niko hapa, mwanaJF kamili!

Na wewe je?
Nini kilikushawishi kujiunga na JamiiForums? Tuambie historia yako, tushirikishane wanajukwaa! Uzi huu ni wetu sote—tiririka!
 
Back
Top Bottom