Jamii inayopenda kuchukua Sheria mkononi ni jamii maskini na yenye watu wenye roho mbaya

Kiboko ya Jiwe

JF-Expert Member
Apr 7, 2020
12,705
36,157
Ukifika mtaa au mji wowote wadadisi jinsi wanavyowafanya wezi wadogo wadogo wa kuku, nguo, au vitu vingine.
Ukiona wenyeji wako wanaanza kujisifu kuwa wao huua wezi hiyo jamii imejaa wajinga na wapumbavu na ina watu wenye roho mbaya a.k.a wachawi.

Hakuna maendeleo kwa watu kama hao, kuwekana misukule, chuma ulete ni jambo la kawaida sana.

Watu hao hawaijui report ya CAG, hawaijui hata bajeti ya wizara Moja. Mabilioni yanayochotwa na mafisadi wala hawana mpango nao ila mwizi wa kiswaswadu watamchoma moto haraka.
 
Mi kibaka akiniibia akatokomea nisikopaelewa aende tu salama, alichoniibia nitanunua kingine kizuri zaidi.

Na nikimkamata atapata adhabu ndogo ya kumchapa viboko na makofi ya kutosha kisha namkabidhi polisi akiwa hana majeraha makubwa na ni mzima polisi wakashughulike nae kama watamuachia ni hiari yao. Wale wanaochoma mtu moto na kumuua ni washenzi na wasiokuwa na roho ya ubinadamu
 
Hapo kuna kuna uwizi wa aina mbili!

1)kuna uwizi watu wanauona

2)na kuna uwizi ambao raia wa kawaida hauoni zaidi ya kusikia kwenye media ...maripoti ya CAG nk

Ova
 
Tatizo ni kwamba hakuna watu washenzi kama vibaka
Ukiingia anga zao kuna mawili
1.kifo
2. Ulemavu wa kudumu
Ndiyo maana wananzengo huwa hawarembi mwandiko
 
Ukifika mtaa au mji wowote wadadisi jinsi wanavyowafanya wezi wadogo wadogo wa kuku, nguo, au vitu vingine.
Ukiona wenyeji wako wanaanza kujisifu kuwa wao huua wezi hiyo jamii imejaa wajinga na wapumbavu na ina watu wenye roho mbaya a.k.a wachawi.
Hakuna maendeleo kwa watu kama hao, kuwekana misukule, chuma ulete ni jambo la kawaida sana.
Watu hao hawaijui report ya CAG, hawaijui hata bajeti ya wizara Moja. Mabilioni yanayochotwa na mafisadi wala hawana mpango nao ila mwizi wa kiswaswadu watamchoma moto haraka.
Bado hujaibiwa ukamkamata mwizi wako halafu polisi wakamwachia kimazabe mazabe
 
Mi kibaka akiniibia akatokomea nisikopaelewa aende tu salama, alichoniibia nitanunua kingine kizuri zaidi. Na nikimkamata atapata adhabu ndogo ya kumchapa viboko na makofi ya kutosha kisha namkabidhi polisi akiwa hana majeraha makubwa na ni mzima polisi wakashughulike nae kama watamuachia ni hiari yao. Wale wanaochoma mtu moto na kumuua ni washenzi na wasiokuwa na roho ya ubinadamu
Hivi nchi hii kuna jamii yenye roho mbaya na umasikini wa fikra kama polisi na wana ccm
 
Hili suala ni tata. Hao wezi wanaochomwa moto na wao wakikupata utajuta. Imagine wewe mleta uzi utajisikiaje unakuta dada yako kajeruhiwa sikio linavuja damu kisa kuna mtu alikuwa anampora hereni? Au mama kaenda sokoni kuuza maandazi halafu anajitokeza mshenzi mmoja na kumpora mauzo yake yote? Mimi sisapoti kuuana ila kama wananchi wana ushahidi usiotia shaka kuhusu vibaka basi wachome tu moto. Hakuna haja ya kuhurumia watu wanaofanya ukatili hadharani.
 
Kheeee 🤣🤣🤣 toa mapendekezo kutibu jamii hizo.
Wakikamata wezi wawafanyie nini??
 
Back
Top Bottom