Jamii imempora mwanamke nafasi yake

MKUU LIZARAZU PUNGUZA HASIRA, MAANA HATA KOKWA LA EMBE LIKIOZA LINAKUWA NDIO CHANZO CHA KUOTA MWEMBE MWINGINE
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] Kwa maana hiyo hata hapo bado ni mahali asipostahili.
 
Habari Wakuu na wachangiaji wote, Binafsi nimesoma bandiko hili na yafuatayo ndiyo maoni yangu:-

Nakubaliana na ukweli kwamba Mwanaume (Adam) ndiye aliyekuwa wa kwanza kuumbwa na baadaye Mwanamke (Eva/Hawa) alifuatia baada ya Adamu kulazwa usingizi na kutolewa sehemu ya mbavu yake ya kushoto ambayo ilitumika kumuumba aliyekuja kuwa msaidizi wake (Yaani Hawa/Eva)

Kabla ya kuumbwa Hawa/Eva. Adamu tayari alikwisha pewa mamlaka ya kuvitawala viumbe vyote vilivyopo chini ya jua (Pamoja na Hawa/Eva) pia alipewa na maagizo ya namna ya kuishi katika bustani ya Eden nini ale/afanye na nini asile/asifanye. maagizo hayo yote Adamu aliyashika na kuyaelewa ipasavyo. Binafsi nahisi hata shetani alijaribu kumshawishi Adamu lakini alishindwa.

Baada ya kuumbwa Hawa na kukabidhiwa kwa Adamu kama msaidizi ndipo vioja vilianza. Adamu aliona ya kuwa Eva/Hawa ni mzuri hivyo alichizika na uzuri wake na hatimaye kusahau kanuni na maagizo (Rules of Engagement) aliyopewa kuhusu Eden na shetani kwa kuwa alikuwa mjanja akaona kuwa Eva ni njia sahihi ya kufanikisha kusudi lake.

Baada ya Shetani kufanikiwa kumrubuni Hawa naye Hawa alikwenda kumwambia maneno hayo Adamu ambaye tayari alikwishachizika na uzuri wake jambo ambalo lilipelekea kumuamini pasina shaka. baada ya kula tunda ndipo walijikuta wakiwa uchi na kwenda kujificha. Baadae MUNGU alikuja kuwatafuta na kukuta wamejificha kwa kuwa wapo uchi alipouliza kama wamekula tunda la mti wa katikati na kwa nini ndipo Adamu akamtupia lawama MUNGU kwa kusema kuwa "Ni huyu Mwanamke uliyenipa" (kwa maoni yangu Adamu alitakiwa kukiri kosa na kuomba msamaha, kumlaumu Hawa haikuwa sahihi maana yeye ndiye alikuwa kiongozi)

Wanaume wa leo tumekuwa waoga wengi wetu tunakwepa kuwajibika na badala yake pale tunapokosea huishia kurushia lawama wanawake. Maandiko yalishatuambia kuwa wanawake ni viumbe dhaifu tuishi nao kwa akili (Kuishi nao kwa akili ni kuhakikisha wanapata mahitaji muhimu, kuwasikiliza, kuwaelekeza na kuwarekebisha pale wanapokosea) lakini baadhi ya sisi Wanaume tumeshindwa kutimiza wajibu wetu na badala yake tumekuwa watu wa kuwasonta vidole wanawake na kuwalaumu, ndiyo maana yanaibuka haya tuonayo sasa.

Kuhusu kuporomoka kwa maadili tatizo siyo Mwanamke mchawi wa mmomonyoko wa maadili ni Technologia hasa ya mawasiliano ambayo pia wagunduzi na waasisi wake ni Wanaume wenzetu wa bara la America na Asia hivyo hata wao (Wanawake) na sisi wote ni .wahanga.

Kuhusu elimu kwa mtoto wa kike siyo jambo baya japokuwa si kila aliyesoma ameelimika, Baadhi ya wanawake waliosoma kisha wakaelimika wametumia elimu yao kuisaidia familia na hakika maisha yao na waume zao ni mazuri na yenye mafanikio maana wanawake hao wamekuwa watii na kuwa wasaidizi hasa kwa wale Wanaume waliobahatika kuwaoa. Wale waliosoma wakashindwa kuelimika ndio pasua kichwa na ndio hupenda kusema "usinibabaishe nina elimu yangu".

Wito wangu ni kuwa tatizo limekwishatokea kulaumu, kukejeli na kudhihaki hakubadilishi chochote. sisi kama viongozi tunatakiwa kuangalia wapi tulikosea, turekebishe kisha tusonge mbele. Maisha ya ndoa hayahitaji uhana harakati bali nidhamu iliyotukuka na upendo wa kweli baina ya wanandoa lakini hii inatakiwa ianzishwe na mume kisha mke afuate.

NINAYO MENGI LAKINI KWA LEO NAISHIA HAPA NA WENZANGU WAENDELEE!!
 
Nime quote hii point
sasa hakuna wanawake bali watafutaji

 
pole sana mkuu

ila hiyo ndio hali haslisi kabisa mkuu

yaani nawashangaa sana vijana wa siku hizi eti katika vigezo wanavyotaka mke awe navyo ni elimu au kipato cha kutosha,ndugu yangu elimu au pesa ya mwanamke haijengi mji,haitunzi watoto hiyo

yaani mkuu kama mke anajua kazi za nyumbani vizuri kabisa huyo ndo wa kuoa na sio ana elimu kiasi gani au pesa kiasi gani,ni shida mkuu shida mnoo basi tu watu huwa hatulijui hilo au tunaamua tu kulifumbia macho

pole sana mkuu kwa shida unayoyapitia kwa sasa,kaza moyo tu mkuu labda itafika siku ambayo atashtuka kwamba anachokifanya sio sawa,plus watoto ni zawadi kutoka kwa Mungu so we endelea tu kukomaa nao wasipoteze mwelekeo,maana wakipoteza mwelekeo maumivu yake hayana kifani,keep the spirit kaka.
 
mkuu kagebby labda hujaelelewa maana niliyoipresent hapo juu

naomba nikusaidie uelewe

Mkuu nini maana ya malezi?

jukumu la malezi ni la nani?baba,mama,housegirl au baba na mama?

nini kinamsaidia mtoto kujengeka vizuri kifikra,kihisia na hata kitabia?kazi ya mama na baba? au nini kinahsukia mkuu?

tuanzie hapo kwanza ndo mengine yafuate.
 
Fanyia hivyo mabinti zako
 
Mkuu ni kweli kabisa uliyoyaandika. Asante sana kwa ushauri mzuri, nimeuchukua.
 
Nyenyere hii ni mada ambayo nashukuru kusema kuwa ndiyo mada Bora ambayo mwaka huu unaoishia masaa matatu mbele nimeiona Bora kabisa sijui uliwaza nini yaani ni unbelievable big up wachangiaji wote

Sent from my itel S32 using Tapatalk
 
jukumu la malezi ni la mwanamke, naye ameliacha na kukimbilia majukumu ya mwanamume
Sasa mwanamke huyu afanyaje endapo ana mwanaume ambaye hatimizi majukumu yake kama baba,hafanyi chochote kwa ajili ya kutunza familia yake??
 
Unapozungumzia umbaji bilashaka unaoata hii katika maandiko matakatifu ambapo Mungu alimumba Adam then akamfanyia msaidizi,Hawa

Katika hali ya kawaida neno msaidizi haliainishi aina ya kazi wala kuweka mipaka. Kimsingi utendaji kazi wa kila mmoja hutegemea na mikakati, ujuzi, elimu, tamaduni, n.k

Umesema vema kwamba Mungu akiwambia "zaeni muongezeke mkaijaze na kuitawala" it means wote wana kazi moja na jukumu moja, hakumwambia Adam pekee
 
You real touch my heart,

Umenisaidia sana wewe na mtoa mada, hili lazima niwaambie wanafunzi wangu, lazima tuongee haijalishi litapokelewa vipi and I used to tell my students as a teacher!!

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Na wamenogewa kweli kweli kiasi kwamba wanaona hata ndoa ni uzushi tu 😂😂😂
 
Maslahi ya nani inamaana haujui !?? Takwimu zinaonyesha kuwa wanawake duniani wapo wengi kuliko wanaume so kitendo cha wao kubaki nyumbani bila ya kuwa naelimu ya juu wenye dunia yao walionao kwamba Rasilimali nyingi sana zinapotea kwa wao kuweza kukosa mapato ..so wakaona kwamba endapo wanaume na wanawake wote kwa pamoja watafanya kazi pamoja Jamii itakuwa na wanataaluma na wafanyakazi wengi na serikali zitapata Kodi kwa wingi tofauti na ilivuokuwa awali ambapo kazi zilikuww zinafanya na wanaume pekee

So wenye dunia yao wao wanataka hell tu that's why waliamua iwe hivyo Kama jamii zenu zinapata hasara kwa kuzalisha jamii yenye mnyumbuliko wa kimaadili wao they don't care wanachotaka wao Ni pesa tu 😁 ili waweze kufanya mambo yao kwa wepesi
Hili linapaswa kuwa mjadala wa kitaifa na hizi taasisi za kimataifa zinazotetea huwa zinafanya hivi kwa maslahi ya nani?
 
Jina lako tu me hoi 😋😋😊
 
You real touch my heart,

Umenisaidia sana wewe na mtoa mada, hili lazima niwaambie wanafunzi wangu, lazima tuongee haijalishi litapokelewa vipi and I used to tell my students as a teacher!!

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
Pamoja mkuu Sambaza ujumbe ni muhimu sana, Western world tayari imeshatoka kwenye gender balance sasa wameingia rasmi kwenye gynocentrism, na hata sisi ndio tunakoelekea huko huko.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…