Jamii imempora mwanamke nafasi yake

Umeenda to the extreme

Na si wanawake wote wako hivyo

Ndo mana bado wanawake wana mahusiano na wanaume na wataendelea kuwa nayo
 
kabla hujabisha hii hoja jiulize kwanza kwanini wanawake wengi wenye vipato hawajaolewa au ni masingle mother
 
Mkuu huu Uzi wako una hoja lakin haya yachukulie kama mabadiliko ya dunia. Ulishafikiria miaka elfu kumi mbele dunia itakuaje yan miaka ya 7019 au 7020 huko. Keep calm enjoy the show
 
Najua mada kama hizi ni ngumu lakini lazima tuangalie ni wapi tulipojikwaa. Feminism ilipaswa kuboresha majukumu ya mwanamke, badala yake imefanya mwanamke awe kama mwanamume.
Ukiwauliza hivi huwa mnataka haki sawa au kufanana haki ? Kwao wanaona kufanana kwa haki ndio haki sawa. Wamesahau ya kuwa haki sawa huwa zinazingatia maumbile na hali za wahusika.

Naendelea kusoma maoni ya wadau ...
 
Na hiki kinachoendelea hapa ni stress za mfumo unaopingwa kama mfa maji kutapata.
Nashauri wanaume wajipange kuwaandaa vijana wa kiume maana sasa ulimwengu unampendelea mwanamke na kama ilivyo kwa wanaume sasa mambo yanaweza kubadilika.
Sasa,hivi ushawahi kujiuliza kwanini huu ulimwengu unampendelea Mwanamke kama unavyodai ?
 
Mkuu hakika hili ni janga la ki dunia, tunakoelekea sio kuzuri, hatusemi mwanamke asipatiwe elimu la hasha, ila shida inakuja pale elimu inapotumika kumfanya mwanamke ajione ameshafanikiwa ki maisha coz anao uwezo wa kupata anachokitaka hata km hana mume,
Lakini ifahamike kuwa bado mwanume atabaki kuwa kichwa, nukuu za maandiko ya vitabu vitakatifu ukiangalia kwa sehemu kubwa hata walipokuwa wakitoa hesabu za idadi ya watu (sensa) waliainisha kundi la wanaume fulani eidha walioenda vitani ama kufanya jambo fulani hii tu inatosha kudhihirisha kuwa mwanaume kuwa kichwa ni mpango toka kuumbwa kwa ulimwengu.
 
What a Genius!!
 
Umeenda to the extreme

Na si wanawake wote wako hivyo

Ndo mana bado wanawake wana mahusiano na wanaume na wataendelea kuwa nayo
Mahusiano yapo ndiyo na ni kweli yataendelea kuwepo kwa sababu hakuna mbala wa hizi gender mbili. Kama kungekuwa na mbadala wa gender hizi mbili nina uhakika kuna watu wangeshajaribisha hiyo alternative kama inafaa zaidi ya me/ke. Uenda pia kiasi flani sitonfahamu kati ya ke na me inachangia kuongezeka kwa lesbianism hadi baadhi ya nchi na madhehebu ya dini wameshindwa kuhimili mishindo yao wakawaruhusu.
 
Pole sana hao itabidi tu ulee mwenyewe kushindwa majukumu kunapelekea ku oa wanawake wenye pesa ili watusaidie hayo ndo madhara yake jitahidi usimkorofishe mana atakuhama mpaka chumba
 
Pole sana hao itabidi tu ulee mwenyewe kushindwa majukumu kunapelekea ku oa wanawake wenye pesa ili watusaidie hayo ndo madhara yake jitahidi usimkorofishe mana atakuhama mpaka chumba
Sioni dalili za yeye kuhama mkuu. Nilishamwambia akijisikia kuondoka milango iko wazi mimi siyo mtu wa kuji-stress sana na hayo mambo. Lakini abanduki mkuu na mara nyingi tunatibuana lakini anakuwa mwepesi wa kushuka na kuomba samahani.

Labda malengo yake kwangu hayajatimia au anaogopa asije akawa muanga wa kisulisuli cha mama lwakatare maana ki- umri bado tunadai kidogo mimi na yeye. Yuko kwenye early 30s wakati mimi niko late 30s.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…