Jamii forum kunyamazishwa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jamii forum kunyamazishwa?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Waberoya, Nov 26, 2008.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #1
  Nov 26, 2008
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,611
  Likes Received: 3,914
  Trophy Points: 280
  Mwisho wa vita hauwi mzuri kwa mshindwaji! lakini unakuwa wa furaha kwa washindi hasa waliopigana usiku na mchana. Watu waliotayari kupika pilau na kunywa vileo kwa kushangilia ushindi hata kama bado mwanzo mbichi, lakini dalili ya mvua si mawingu?

  Ukitaka kuua Jamii forum ni kazi ndogo, Pelekeni mafisadi jela, taifisha mali zao zote wagawie maskini!

  Ukitaka kuua jamii forums na kuwakata kauli watu, wamiliki wote wa kagoda tuwajue na hatutaki usanii wowote ule, ama sivyo jamii forum haitakufa, watu wataongea hata kama kwa ishara, tutatuma ujumbe kuanzia kuzimu mpaka kwenye sayari ya pluto.

  Nasema ukitaka kuua Jamii forums, wasizungumzie tena siasa fanya watakavyo wao, ongozeni kwa hekima na maarifa makubwa huku Haki ikitawala.

  Pengine hivi karibuni jamii forum itakufa,pale ambapo TZ itakapokuwa kama peponi ya duniani, huku kila mmoja akitamani kuishi Tanzania.

  Nasema ukitaka kuwanyamazisha hawa watu wasiongelee siasa ni rahisi sana muziki wa YONA NA MRAMBA uendelee, hata hivyo wataacha kuzungumzia siasa watazungumzia ushindi!!,Kipi bora kufurahia kwa ushindi kiduchu tunaouona au kuwa katika matumaini ya kuwakamata watuhumiwa wote wa ufisadi kesho? haitawezekana kidogokidogo namna hii ina dalili zake ati!!, wenyewe watakosana watatajana tutakaa pembeni tukiwaona wanavyoumana,
  Na hapo tutazidi kupashana kwa habari kwa furaha zaidi kuwa CCM wamemeguka hili halitakuwa la kupiga kelele watakuwa wametunyamazisha kuongea siasa na mafisadi! ila tutaongelea kuhusu ushindi huo pia!

  Au wewe unafikiri nini kifanyike Kuinyamazisha JF??

  nawasilisha

  waberoya
   
 2. Mlalahoi

  Mlalahoi JF-Expert Member

  #2
  Nov 26, 2008
  Joined: Aug 31, 2006
  Messages: 2,065
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  JF inyamazishwe ili iweje?
   
 3. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #3
  Nov 26, 2008
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 0
  wanyamazishwe na nani?

  Hivi unajidanganya kuwa watu wako bize na hili dude?

  Hivi unajua wangapi wana access ya hiyo PC? achilia mbali internet?

  please get your facts right mjomba
   
 4. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #4
  Nov 26, 2008
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,611
  Likes Received: 3,914
  Trophy Points: 280
  Kweli fasihi ngumu!!! JF is family take it man! hapo nashangilia jambo fulani

  Hivi mmekuwa wageni Yerusalemu hii, hamjui lililotokea na litakalo tokea

  lugha ya fasihi hiyo msiichukulie NEGATIVE THAT IS PURE POSITIVE

  waberoya
   
 5. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #5
  Nov 26, 2008
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,611
  Likes Received: 3,914
  Trophy Points: 280
  Kwani itanyamazishwa kwa kufanyaje?? read again!!

  waberoya
   
 6. u

  under_age JF-Expert Member

  #6
  Nov 26, 2008
  Joined: Apr 17, 2007
  Messages: 317
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  jf haina haja ya kunyamazishwa , kwa namna inavyokwenda nadhani itafika sehemu itajinyamazisha yenyewe. ni vigumu sana kuamini kwamba ile jf niliyoijua kipindi cha nyuma imekuwa tofauti na hii ya leo. aaakh inakera kisha inaudhi kuona member wa jf leo hii wamemsahau adui yao na badili yake wanakuwa maadui wao kwa wao, kila siku ukija unaona mara huyu kaaga na mara huyu kamsema kwa ubaya huyu. mmmh its not too late acheni tubadilike kwa manufaa ya taifa letu. tuachaneni na mambo ya kitoto na mambo ya kitarabu tarabu.jf ni moja na lengo lake ni moja na member tuweni kitu kimoja. tanzania lazima igomboke!
   
 7. M

  Mkuu Senior Member

  #7
  Nov 26, 2008
  Joined: Jan 1, 2007
  Messages: 127
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Nivuri kujibu hoja baada ya jusoma sio kuangalia vichwa vya habari halafu mukakurupuka tu mutaiharibu hili janvi letu tukufu waheshimiwa
  Waberoya katoa mada kwa kiswahili na kiswahili ndio lugha yetu tusijifanye hatukijui na kukurupuka tu.
   
 8. Pundit

  Pundit JF-Expert Member

  #8
  Nov 26, 2008
  Joined: Feb 4, 2007
  Messages: 3,741
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Unamfahamu BRAZAMENI wewe?

  His politiocs is greener than the environmentalists, his party card is the blue book, his religion is Latina chikas, the most apolitical brother you ever saw.

  Mafisadi, kuna watu hawana habari bwana!
   
 9. YournameisMINE

  YournameisMINE JF-Expert Member

  #9
  Nov 26, 2008
  Joined: Aug 29, 2007
  Messages: 2,451
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 145
  Sema wewe braza...tena hao ndio wapo kibwena!
   
 10. O

  Ogah JF-Expert Member

  #10
  Nov 26, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  ....ushamba unasumbua sana watu........
   
 11. Mlalahoi

  Mlalahoi JF-Expert Member

  #11
  Nov 26, 2008
  Joined: Aug 31, 2006
  Messages: 2,065
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Ahhh...JF itajinyamazisha yenyewe!?Nilidhani wenye ndoto za aina hiyo ni mafisadi pekee kumbe hata baadhi ya wana-JF wenzetu!Hivi unaweza kutoa MIFANO HAI ya namna JF inavyotumia muda mwingi kujadili members badala ya mafisadi?Hii overgeneralization sio nzuri,hasa unapodai KILA SIKU huyu anaaga baada ya huyu kamsema huyu vibaya.This is an open forum,anayejiskia kujiunga anakaribishwa na anapojiskia kuondoa (hata bila kuaga ruksa).

  JF kama forum inaweza kuwa moja lakini sio lazima members wake wawe wa aina moja kwa vile hii sio CCM ambayo kukemea ufisadi ni dhambi.Hapa kuna mkusanyiko wa watu wenye itikadi,taaluma,background,umri,imani,jinsia,etc tofauti.Katika mazingira kama hayo basi lazima tutatofautiana katika baadhi ya mambo.Na mfano hai ni huu wa wewe unayeamini kuwa JF itajinyamazisha yenyewe while mie (na well-wishers wa JF) tunaamini itadumu kwa muda mrefu.

  Tanzania haiwezi kugomboka kwa mentality hizi za ku cherry-pick mabaya (eg uliyoyaita mambo ya kitoto au taarabu taarabu) na ku-ignore mijadala mizito inayopelekea haya yanayovuma leo hii huko nyumbani.Hivi umeshawahi kujiuliza mchango wa JF kwenye scandals za EPA na Richmond,kwa mfano?Hizi sio taarabu au utoto utoto.Na laiti ingekuwa hivyo basi vichwa kama FMES,Mwanakijiji,Pundit,GT,Jasusi,etc wasingeendelea kuwepo hapa na Invisible angeshaachana na shughuli hii ilopelekea akabughudhiwa na vyombo vya dola ( badala ya real criminals like the Kagodas).

  By the way,ukiona mambo yako kinyume na matarajio yako unaweza kujichukulia likizo ya muda mrefu (au ya kudumu) kutembelea JF.I bet my last pence kwamba ukirudi utaikuta JF ikiwa as strong as ever.Nothing personal lkn hiyo overgeneralization haikustahili.
   
 12. u

  under_age JF-Expert Member

  #12
  Nov 26, 2008
  Joined: Apr 17, 2007
  Messages: 317
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  mara nyingi huwa sieleweki, si unajua sikuenda shule tena , just niwieni radhi, lakini maelezo yako naona hayapingi nilichoeleza ila yanasupport nilichoeleza , siwezi kupinga tafauti ya mawazo baina ya members na najua kwamba jf ilikuwa imara na mpaka leo ipo imara lakini je itaendelea kuwa imara? kwa namna tunavyokwenda nayo?, waswahili wanasema dalili ya mvua ni mawingu na kwengine wanasema samaki mkunje angali mbichi, najua kijiumri changu kidogo na vijimawazo vyangu vya kitoto toto lakini mmmmh hisia zimekuwa kali kuliko mawazo katika kipindi cha siku mbili tatu zilizopita hapa jf .finger crossed nataka jf iwe kitu kimoja as a team hata kama tunatofautiana kimawazo .sorry kama nimekera.
  ni ndugu yenu under age
   
 13. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #13
  Nov 26, 2008
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,611
  Likes Received: 3,914
  Trophy Points: 280
  Haa, msinichekeshe, kusemana hakutaiua JF hata siku moja!!!, mpaka sasa JF imefika umri na uwezo ambao hata mwanzilishi mwenyewe akitaka kuifunga atashangaa kesho yako kuiona JF nyingine kama hii hii inatamba tena.

  Kumsema mtu hakukwepeki kumbukeni hapa kuna watu wenye akili zo tofauti sana, nature yenyewe inawaselect hao watu na wataondoka,pengine dawa nzuri ni kutomjibu kabisa mtu ambaye taanzisha thread ya kumsema mtu mwingine!

  MMEISHAONA 'PICHA' ZA KIVITA WANAJESHI WA JESHI MOJA, HAWAPINGANI HATA SIKU MOJA, KIZURI ZAIDI NIMESHUHUDIA MWENZAKO AKIPIGWA RISASI KWENYE UWANJA WA VITA , UNAM'BEBA UNAMWEKA BEGANI MNATAFUTA SEHEMU NZURI YA KUMUHUDUMIA.

  Hawa wanaoanzisha thread za kuwasema wenzao aidha wana inferiority complex, wivu, choyo na kingine msifikiri wale maadui wa taifa letu sio member humu, wako wengi kwa lugha na majina makubwa!!! kizuri tukiwatambua tunawaweka kapuni, kuanzia kwenye mawazo yetu mpaka kubonyabonya keyboard!

  NIKIRUDI KWENYE THREAD YETU HII, NIMEULIZA SWALI! NATAKA SERIKALI IJIBU, WATU WOTE WASIOIPENDA NA WANAOIPENDA JF WAJIBU JE ILI KUINYAMAZISHA JF WATU WAFANYE NINI??

  MOTO NDIYO HUO KWANZA UMEWAKA BADO ASUBUHI SANA......

  YONA, MRAMBA...JEETU PATEL, HATA KAMA WANAZUGA , TUNAONA.....

  VITA MBELE

  waberoya
   
 14. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #14
  Nov 26, 2008
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,611
  Likes Received: 3,914
  Trophy Points: 280
  labda niwasaidie wasioielewa thread

  ili JF inyamazishwe


  1. Mafisadi wote waende jela na warudishe hela zetu
  2........

  WABEROYA
   
 15. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #15
  Nov 26, 2008
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,604
  Likes Received: 18,643
  Trophy Points: 280
  JF sio forum ya kulani- mafisadi, mambo ya vita dhidi ya ufisadi ni kipengele kimoja tuu kati ya vingi ndani ya-JF, ni Jukwaa la Siasa. Vipenhele vingine vingi bado vipo. Hata vita vikiisha mambo mengine kibao muhimu yatapata nafasi nzuri mfano ni hoja ya kila Mtanzania ni tajiri, anatakiwa kumiliki gari, kuwa na nyumba nzuri na kuishi vizuri ikiwa ni pamoja na kula vizuri na kupata starehe. Tatizo hapa sio mafisadi, ni mfumo wa uchumi uliopelekea wachache wamiliki mali na wengi wahangaike.jF inatakiwa ikusaidie wewe usie na nyumba, gari na pesa za kutosha na ziada ya kununulia stock ili kubadili maisha yako, yangu na yake kwa kifupi maisha yetu. Sio suala la ufisadi ni zaidi ya hapo,. Hii ndio JF ijayo baada ya vita na 2010 kupita salama.
   
 16. Sura-ya-Kwanza

  Sura-ya-Kwanza JF-Expert Member

  #16
  Nov 26, 2008
  Joined: Nov 17, 2007
  Messages: 561
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Hizo sababu huko juu, za kunyamazishwa jamii forum, ni mengi ya mlolongo wa siasa mbadala inavyoweza kuendeshwa na mdahalishi, kwani, hata ikitokea hizo sababu zako huko juu zikafanyiwa kazi-wengine watakuwa wanafanya mambo hayo hayo-na vile, Jamii Forums- JF Ville!!! will always DARE TO TALK OPENLY!

  Kula Breki!!!
   
 17. K

  Koba JF-Expert Member

  #17
  Nov 26, 2008
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 6,144
  Likes Received: 495
  Trophy Points: 180
  .....sloppy writing,we dont need any of that here!
   
 18. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #18
  Nov 26, 2008
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,611
  Likes Received: 3,914
  Trophy Points: 280
  Thanks man, but I dont see your Meticulous writing here! (only you!)

  waberoya
   
 19. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #19
  Nov 26, 2008
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,611
  Likes Received: 3,914
  Trophy Points: 280
  Pasco: Ebu fafanua those highlighted words, pia tufafanulie unaposema JF ijayo baada ya vita ya 2010 kupita salama! unamaana gani???
  tunasubiri

  waberoya
   
 20. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #20
  Nov 26, 2008
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,611
  Likes Received: 3,914
  Trophy Points: 280
  2. Mikataba ya madini, IPTL na mingine mingi iwe 'online' iwe wazi kwa watu wote, na kila uamuzi wa kitaifa uwe wazi for everyone!


  3......................

  waberoya
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...