Jamhuri: Pinda agongana na bilionea Dar!

Jamhuri: Pinda agongana na bilionea Dar!

hamna mtu anaeunga mkono mambo kama hayo,ila hapa logic inatufanya tusifikie conclusion...hii maelezo ya mdosi yako onesided,hakuna maelezo ya upande wa pili.

Pia evidence za kuwa sexual assaulted sidhani hata kama anazo.anavodai baada ya tukio amekimbia kujificha zenj,kwanini hakwenda polisi na kisha hospital kuchukua vipimo ili awe na evidence kuwa walimwingilia.?.
Unadhani kwa maneno tu mahakama yaweza kutia mtu hatiani?.
Isijekuwa baada ya kunyang'anywa mali na akaja na hizi story ili a get even na boss wake.
soma vizuri maelezo wacha kukurupuka
 
Mimi kuna bosi mmoja namfahamu,my ex boss,anampaka lokapu yake ndani ya ngome..ukila shoti (kupata loss)unaweka lokapu hata miezi mitano na wakati huo wapambe wanazungukia asset zako,nyumba,ng'ombe etc wanataifisha mpaka pesa irudi.
Kama huna asset wanakupeleka direct mahakamani unakuta hakimu ameshasetiwa unakula mvua fasterfaster,na hapa naongelea loss ya milion 3,4,5.
Chezea.

Get a life son; "vengeance" is not a mere vocabulary!!!!!!!!
No matter how beautiful the matress is people will never sleep for good!!!!!
 
Huyu, mdosi namfahamu sana, kamwibia sana Ally, mdosi hapa anavungavunga tu, Ally aliposhtukia wizi wa mdosi, alimwita akamuonesha ushahidi kwamba mdosi kamwibia akamwambia amrudishie alichomwibia, mdosi akajifanya mjanja, ikabidi ally atumie njia mbadala kupata chake, hapa mdosi kaongeza chumvi nyingi kwenye stori.
Kama alikuwa na ushahidi kwa nini akufuata
Sheria badala ya kujichulia mambo mkoni? Anaogopa nini kufuata sheria?

Mtazamo wangu: Wanasema, mkuki kwa nguruwe mchungu.Huyu Mwajiri alimfundisha huyu mfanyakazi wake kuwaibia watanzania na yeye akahamua kujeuzia kibao mwajiri.Kama angefuata sheria ingetokea "wewe umemwaga ugali wacha na mimi nimwage mboga".
 
Kamanda wa Kanda maalum ndugu Kova amekaa kimya kama hajasikia yeye ni kuokoteza Bendera za CDM na kuzionyesha kila siku huku watu wakatili kama hawa akiwaacha

Kesi yenyewe inahusu $10M, unadhani yeye akipewa mgao atauacha? Thubutu. Polisi wa siku hizi ni balaa, akikukuta na mzigo mnene anataka mgawane, ukigoma unakula shaba na mzigo anabeba.
 
Kwanini gazeti limehujumiwa hili ndio swali la kujiuliza kwanini lihujumiwe?

Ili haya tuliyoyajua yasiwafikie watanzania wengi ili kushindwa kazi kwa serikali kusifahamike
 
Wadhani hata Waziri mkuu angetingishika kama angekuwa Mswahili? Waswahili wangapi wamekuwa sodomised na hawa Wahindi/Waarabu koko?
'Wabantu wamezoea mateso' angewaza!
Wahindi wanasaidiana sana. Huyu lazima atakuwa anapata sapoti kutoka kwa Wahindi wenzake la sivyo angekuwa ameshambikiziwa kesi siku nyingi.

Angekuwa Mbongo labda picha yake naye ingekuwa kwenye mobile!!
 
Kesi yenyewe inahusu $10M, unadhani yeye akipewa mgao atauacha? Thubutu. Polisi wa siku hizi ni balaa, akikukuta na mzigo mnene anataka mgawane, ukigoma unakula shaba na mzigo anabeba.

Wanyonge mpaka tuzikusanye sauti zetu kwa pamoja ndio zitasikika vinginevyo tutabaki kuonewa kila siku na hao wanaodai serikali yote iko mikononi mwake
 
ndo mana wengine wanamaliza kwa tindikali kama alivyofanywa yule jamaa wa home shopping centre hatakaa aishi kama zamani tena!!!
 
Hii ni habari ya kusisimua na kuamsha hisia nzito lakini ukweli unabaki palepale: ni tukio tu katika package nzima au mfumo mzima wa uendeshaji nchi tulio nao. Maswali makubwa ambayo tumeshajiuliza tayari ni jinsi uwekezaji, uendeshaji na usimamizi wa hizi biashara kubwa unavyofanyika. Sheria zinafuatwa? Wamiliki wanajulikana? Hesabu zao ziko wazi? Mapato halisi na faida vinajulikana? Kodi halisi zinalipwa? Vinginevyo, ni mfumo wa uchumi wa ki-mafia. Na kama ni hivyo, huko ndani lazima kuwe na kila aina ya madhambi na kuchezeana rafu kama ilivyo katika mkasa huu. Kawaida huwa yanaishia humohumo. Nchi yenyewe hii, vyombo vya dola vinadhibitiwa na viongozi wa juu wa kisiasa na matajiri wanaohusiana nao. Sanasana tungeweza kusikia tu kuwa "maiti ya muasia imeokotwa, ajali imetokea..., n.k.).

Kwa muktadha huo, mimi nachukulia tukio hili kama "yaliyomo tu" na hivyo hatuna haja ya kulipotezea muda kama tumeshindwa kupata majibu ya jinsi ya kufumua mfumo mzima wa ki-mafia unaoendelea kuwatesa watanzania wengi na kuwalazimisha kujikomba au kusalimisha utu wao kwa wenye kuusimika na kuuendesha mfumo wenyewe. Kwa upande mwingine, unaweza kusema kuwa huyo tajiri (maaluni) wa Lake Oil na mhanga ("mwizi") wake wote ni sehemu ya tatizo lililokithiri nchini la biashara za kifisadi/ki-mafia zinazodhibiti uchumi na uongozi wa nchi. Hivyo, tusipoteze muda kwa tukio moja ilhali yako mengi ya aina hiyo na kuzidi yaliyotokea, yanayotokea na yatakayozidi kutokea kwa kadiri tutakavyoendelea kuwaweka na kuwachekea mabaradhuli katika safu za uongozi.
 
Japo ni mtanzania mhindi, wanaharakati ingilieni kati suala hili (intervene), this is too bad. Ndiyo maana tunasema tu-change mfumo wa maccm, look how mapoliccm wanavyo shindwa kusimamia haki.
 
Huyu mhindi kapiga kweli hela, ila mwaarabu nae katumia uhuni mkubwa.
 
Pinda jikongoje ili upambane na huyu gabachori ,asiye na hofu na mungu!
 
Hivi anaitwa Ally Awadhi au Omary Awadhi?? Kuna tanker moja huwa inapaki pale Lake Oil Petro Station iliyopo ilala Bungoni imeandikwa kwa Maandishi makubwa yaliyonakshiwa "OMARY AWADHI"
 
Hapa tatizo si Mdosi kuadhibiwa kwa wizi wa mabilioni alio muibia Ali hapa tatizo ni umiliki wa Lake oil kuhusishwa na Riz 1 laiti Lake oil ingehusishwa na Mtei au Mbowe ingekuwa stahiki ya Mdosi yalio mkuta. Huyu Mdosi ameiba pesa nyingi sana mpaka amekuwa bilionea kwa mshahara wa 6m tu kama nini nisingeishia kumlawit yeye tu ningewalawit mpaka ndugu na mjirani zake hapo upanga.
Acha upuuzi vipi huyo Mwarabu gaidi angehusishwa na Mbowe na Mtei ingekuaje serikali ya ingekalia hii kesi.?

hapa tunaongelea unyama aliofanyiwa mdosi kupigwa hadi kulatiwa kwa zam na mabaunsa wawili tena kwa zamu, kama haitoshi kumfilisi kila kitu.

hivi huyo mdosi siku akija hapo ofisini kwenu atembeze risasi ofisi nzima mtamlaumu.?
 
Ukiangalia muda alioajiriwa baada ya kumaliza masomo na mali alizonazo kama napata shida vile, pia dola 100,000 nyumbani au sijaelewa? hakuna uhalali wa kilichofanyika ila inawezekana wizi ulifanyika pia.
 
Mkuu Kapotolo nasikia Lake Oil ni mtoto wa Boss Ridhiwani!
Kanda ya ziwa yote vituo vya mafuta vimejaa, hadi Mwz!!
Labda ndio maana huyo --------- ana kiburi!!
.Nchi imeoza hii ndugu yangu!!
 
Sasa kama mtu amekuibia bilioni 16 ulitake amfanye nini? Ambembeleze amrudishie hela zake? Au ampeleke polisi? Kama ni kweli mdosi alimuibia jamaa, basi hayo matatizo amejitakia mwenyewe. Ni tamaa za kutaka kutajirika haraka haraka zimemponza. Alikuwa analipwa mshahara mzuri, na pembeni anafanya biashara ambayo nadhani ilikuwa inampa kipato ziada kizuri tuu, sasa kwa nini amuibie bosi wake (allegedly)?
 
Back
Top Bottom